The Monk
Platinum Member
- Oct 12, 2012
- 19,254
- 42,873
Ukidhamiria mtu binafsi kununua hisa unakuwa na uhuru wa kufanya utafiti na kuona kampuni yenye mwelekeo wa uchumi mzuri ikiwa ni pamoja na kujua historia ya maendeleo ya kampuni, hayo ni muhimu si kufuata tu matangazo ya biashara, hakuna anayetangaza biashara asiyeisifia chake kuvutia wateja, ila utafiti ndio utakaokupa ukweli.
Katika shauri langu, siku na nafasi ya kuchagua au kufanya upembuzi kwa vile nchi za kibepari makampuni ya kipepari hiyo ni njia moja wapo ya kutumia pesa za wafanyakazi kwa kuongeza ufanisi wa makampuni. Ndio maana huna nafasi ya kuchagua kwa sababu hawakupi hela, inakatwa moja kwa moja na kuingizwa huko nawe unaletewa tu account number yako.
Kuna faida yake kwa nchi kama za ulimwengu wetu wa Tanzania, kwani uchumi hauyumbi sana kama ilivyo kwa mataifa makubwa. Lakini kama ulivyosema si vema kuweka pesa yote huko, bora kuweka hizo unazoona huziihitaji kwa sasa na ambazo huna malengo ya kuchuma faida ya papo kwa papo.
Mambo ya ubia ni ya wenye kipato zaidi, kwa wa kipato cha chini ni vigumu kidogo maana kiwango kinachohitajika ni kikubwa, uzungumzie kuweka mamilioni si malaki. Hata hivyo kuna makampuni madogo siku za usoni yatakayoibuka baada ya elimu hii kuwafikia wengi.
Umemema vema mkuu, naomba nisichakachue saana pointi yako, kwenye bold namaanisha kiasi cha faida utakayopata kutokana na gawio kinakua kidogo kwa kuwa na kiwango kidogo cha shea.