Samahani mkuu, nimechelewa kujibu swali lako mambo ya mwaka mpya, nimeku PM namba ya jamaa mojawapo yuko Dar wasiliana nae atakupa maelekezo na kujibu maswali yako bila malipo. Asante
Mada nzuri lakini haijalenga kuwaelimisha wanaJF. nafikiri ingekuwa vema kama kungekuwa na mwendelezo juu ya namna gani (taratibu za kufuata) ili mtu aweze kuingia kwenye hii biashara, vigezo, faida na hasara (viwekwe wazi/bayana)!
wenye maujuzi mtujuze jamani!
Mimi ninazo za NICO,frankly speaking it was a bad investment
Unachosema ni kweli mkuu, ndio maana nimewaalika wadau wamwagike zaidi. Ila ushauri wangu ni huu:-
1- Usifanye biashara ya hisa kama unataka kupata faida ya haraka, kuzungusha hela na kupata faida kwa muda mfupi.
2- Usichukue kiasi kikubwa cha mkopo benki au taasisi yeyote na kuiweka yote kwenye hisa bila kufanya utafiti wa kutosha na umakini mkubwa kwenye kampuni unayotaka kuwekeza.
3- Kwa kuwa hisa zinaongezeka thamani kutokana na ufanisi na uendeshaji mzuri wa kampuni uliyowekeza, ni vema kuweka hisa kwa hela ya ziada au usiyoihitaji kwa haraka. Ikumbukwe kwamba wingi wa hisa unakupa kiasi kikubwa cha gawio kila mwaka endapo kampuni inaenda vizuri na inapata faida.
4- Kununua hisa za kampuni fulani inamaanisha unaimiliki kwa kiwango cha hisa zake, ikipata hasara hakuna gawio na huenda bei za hisa zikashuka.
mkuu ahsante kwa mada nzuri ,ukishanunua hisa kinachofuata unapewa nini kutoka kwa kampuni husika .kuna cheti cha hisa hiki nini
Samahani mkuu, nimechelewa kujibu swali lako mambo ya mwaka mpya, nimeku PM namba ya jamaa mojawapo yuko Dar wasiliana nae atakupa maelekezo na kujibu maswali yako bila malipo. Asante
mf.nilinunua hisa za watoto fund naalikwa kwenye mikutano hiki cheti sina ,na ukiwa umenunua hisa za shilingi ngapi ili wakupe cheti hiki.unapata cheti kuonyesha umiliki wako wa hisa kuna kuwa na maelezo ya msingi ya hisa ulizonunua. Huitwa Share Warranty. Lakini kwa dhati kabisa uwekezaji wa hisa tz bado una changamoto nyingi ambazo mwisho wa siku an ordinary shareholder ana ambulia patupu. Kuna tafiti mm nafanya juu ya high yield investments kwa makampuni fulani ya nje.
unapata cheti kuonyesha umiliki wako wa hisa kuna kuwa na maelezo ya msingi ya hisa ulizonunua. Huitwa Share Warranty. Lakini kwa dhati kabisa uwekezaji wa hisa tz bado una changamoto nyingi ambazo mwisho wa siku an ordinary shareholder ana ambulia patupu. Kuna tafiti mm nafanya juu ya high yield investments kwa makampuni fulani ya nje.
Mimi ninazo za NICO,frankly speaking it was a bad investment
Hauko peke yako, hata mimi nimepoteza pesa zangu huko.
Nilipokuwa nafanya kazi nikiwa mwanachuo huko ughaibuni, kampuni ilikuwa na utaratibu wa kutoa bonus, lakini bonus hupati cash, ila unalazimika kuingia hisa kwenye makampuni makubwa NY Exchange. Bahati yangu nilikataa kuchangia kutoka mshahara wangu kwa vile sikuwa na malengo ya kubaki huko muda mrefu.
Kila robo mwaka tulitumiwa nakala ya hali halisi ya kifedha, kilichonishtua ni kudorora kwa soko pesa yangu ikaliwa 25%. Walioingia kichwa kichwa na kuchangia mishahara yao walijua kuzalia.
Mambo ya hisa kuwa makini sana, vinginevyo unaweza kutoka na kicheko cha furaha na ipo siku huzuni hata kupata ugonjwa wa moyo.
Nilikumbana na hii makala katika pitapita zangu nikiwa natafuta zaidi hii elimu ya hisa, ambayo naona hapa kwetu bado vijana na wanachi wengi kwa ujumla hauitumii vizuri. Nikaona ni vema nikishirikiana na wadau hapa JF na kwa wale wenye uzoefu na utaalam zaidi waendelee kutufahamisha....
Unapowekeza katika hisa jihadhari na makosa yafuatayo; kununua au kuuza hisa zako bila utafiti, kutokujua tofauti ya thamani ya bei, kununua kwa kuangalia jina na umaarufu wa kampuni, kutokua na malengo maalum, kununua kwa kuwa bei ni rahisi, kukosa maarifa au kutozingatia elimu ya fedha, hisa na uwekezaji, na kuwekeza fedha nyingi kwenye kampuni moja.
Shukrani SAMARITAN kwa elimu ya hisa, moja ya changamoto kubwa katika uweekezaji wa Hisa hapa kwetu TZ ni (Inflation) mfumuko waa bei, nadhani ni kuanzia 9% hadi 16%, hata kwa muda mrefu kwa kulinganisha na mapato ya hisa zilizopo inakuwa ngumu sana kufidia na kupata ziada kama faida, tafadhali nigependa ushauri/mtazamo wako kwenye hili, chukulia mfano wa CRDB...(labda km mwekezaji hana shida na hiyo pesa yake au ana surplus).
Nashukuru kwa ushauri na uzoefu wako mkuu, ndio maana tunataka wataalam na watu wenye uzoefu kwenye eneo hili watupe michango zaidi ili watu wanufaike na wasiwe wahanga wa uwekezaji kwenye hisa.
Nadhani si vibaya kama nikinukuu tena sehemu ya hiyo makala hapo juu