Wakulonga
JF-Expert Member
- Oct 29, 2012
- 762
- 772
Habari wana JF
Kila siku najiuliza bila kupa majibu. Hivi soko la Dunia lipo nchi gani? Kama kuna mtu anjua lilipo anifahamishe Maana ni muda najiuliza bila kupata majibu
====
Majibu
Kila siku najiuliza bila kupa majibu. Hivi soko la Dunia lipo nchi gani? Kama kuna mtu anjua lilipo anifahamishe Maana ni muda najiuliza bila kupata majibu
====
Majibu
Hahahahaha swali zuri sana
Anyway ipo hivi, soko tunajua ni sehemu bidhaa zinapouzwa. Yaani mfano mtu ukitaka kununua viatu unaenda kariakoo, ukitaka kununua ndizi unaenda soko la mabibo, ukitaka mchele unaenda mbeya au Morogoro, ukitaka korosho utazipata Mtwara.
Kwa hiyo ina maana soko la bidhaa fulani ni mahali ambapo unaweza kuipata bidhaa ile kwa wingi na ambapo utaipata kwa bei yenye ufanisi kwa kuwa ndipo inapopatikana kwa wingi.
Kwa hiyo soko la dunia sasa, ni popote pale kwenye nchi tofauti tofauti ambapo bidhaa fulani inakuwa inazalishwa kwa wingi.
Mfano Thailand wanalima mchele kwa wingi kuliko nchi yoyote duniani, hivo basi unaposikia soko la dunia la mchele maana yake hilo soko lipo Thailand. Na hata bei elekezi unayoiona hapo ina maana ndo bei iliyopo kule Thailand.
Ki urahisi kabisa, wewe shika tu kwamba soko la dunia la kitu fulani linapatikana pale ambapo bidhaa hiyo inapatikana kwa wingi. Kwa sababu huko ndipo kutakuwa kuna muhimili imara wa ku determine bei ya soko iwe vipi.