soko kwa ajili ya kuuza bata mzinga

Neytemu

Member
Nov 7, 2010
83
1
Salaam,
Wakuu wapi naweza kupata soko kwa ajili ya kuuza bata mzinga?kwa sasa wapo Moshi ila bado si tatizo kubwa sana kama ntapata soko Dar.
 
Salaam,
Wakuu wapi naweza kupata soko kwa ajili ya kuuza bata mzinga?kwa sasa wapo Moshi ila bado si tatizo kubwa sana kama ntapata soko Dar.

Msimu wa kununua bata mzinga umefika,wanaliwa sana wakati wa x mass na wadosi ktk jiji la dar. Sasa mimi nikushauri, nenda pale Black point ( break point) makumbusho, kuna kibanda kina aina nyingi za bata, uliza pale watakwambia kila kitu.

Hao bata wana umri gani? Mimi nawataka wa kufuga, je unaweza kuni-pm ili nione kama naweza kupata wa kufuga?
 
Asante Malila kwa maelekezo.Tafadhali nieleweshe jinsi ya ku PM nini maana ya PM yenyewe?coz naionaona tu na mi mgeni kwa hii forum.
 
Asante Malila kwa maelekezo.Tafadhali nieleweshe jinsi ya ku PM nini maana ya PM yenyewe?coz naionaona tu na mi mgeni kwa hii forum.

PM ni private message, ku PM ni kumpelekea mwenzio ujumbe, nenda ktk jina langu,click hapo, kutatokea maelezo, moja ktk maelezo lipo moja la private message, click ktk neno hilo, utafunguka ukurasa wenye nafasi ya kuandika kama kawaida. Ukimaliza kuandika send kama kawaida,itanifikia bila kuonekana ktk jukwaa kuu.

Naamini umenielewa.
 
Break point utapata directions,ila vizuri uwapige picha,ujue uzito wao kwa wastan,then tembelea kilimanjaro kempliski,moven pic,new africa hotel and sea clif,ongea na wakuu wa manunuzi jikoni,
tatizo wanapenda guarantees of quality and quantity.
vinginevyo uwaombe wakupe contacts za watu wanao supply kwao,hivyo wataweza kununua kutoka kwako then wataunganisha na bata wanao nunua sehemu zingine.
kuna kijana alipata tenda ya kuku wa kienyeji kempliski,akajakuchemsha uwezo wa kusupply ,ili bidi wampige chini.

Unauza bei gani?pia mimi ningependa bata 4 wa kufuga.wadogo
 
Thanx Newmzalendo kwa maelekezo ntayafanyia kazi.nauza laki moja ila kulingana na size bei inapungua mkuu
 
Jaribu kwenye mahoteli makubwa yenye hadhi ya nyota tano kama Kilimanjaro,Hilton huko watasha wanapenda sana kula nyama ya bata mzinga,au jaribu kuonana na utawala wa Shoprite supermarket,lazima uhangaike pia hakikisha bata wako hawana homa ya mafua kaka yaani wameangaliwa na daktari wa mifugo
 
Wangekuwa na mafua na yeye angekuwa anayo. Mbegu ndg yangu tunaihitaji. Unapotangaza wakubwa totolesha na wadogo utuuzie mbegu.
 
Duuh sikujua kama hawa Bata mmoja anaanzia laki moja

Hiyo ni bei ya bata jike, jike linaanzia 50 elfu mdogo mpaka laki moja mkubwa na dume ni laki moja mpaka moja na nusu. Tatizo hawa bata hawazaliani fasta kama wale wengine. Ukimaanisha bata mzinga analipa.
 
Thanx Malila kwa ufafanuzi makini

Hizo ni bei za kawaida kwa bata hawa.Bata wa kilo 20 anauzwa mpaka laki moja na ni kweli hawaongezeki kwa kasi ila wanapoanguliwa huwa wanakua haraka.Mayai ya bata hawa mazima (yenye jogoo) yanaweza kuanguliwa pia na kuku wa kawaida
 
Thanx Newmzalendo kwa maelekezo ntayafanyia kazi.nauza laki moja ila kulingana na size bei inapungua mkuu
ukifanikiwa usiache kutupa feedbak hapa JF.
lini utakuwa mjini kwa mauzo,mimi nitakuwa tayari kununua by end of january-february,kwa ajili ya ufugaji na pia utakuwa ubize wako umepungua kwani kipinindi hiki cha X-mass utakuwa bize kutafuta masoko na kuuza hao bata
 
Bro Mzalendo kama ulikuwepo,

Nimemwambia by january na mimi nitahitaji kwa ajili ya kuwafuga, kwa hiyo Ney kaa mkao mzuri tufanye biashara.
 
What? Laki moja za TZ au za Zimbabwe? Ana kilo ngapi huyo bata mzinga? Au unauza Mbuni? Mhhh!
hahaha, mheshimiwa, na mimi ndo naona bei hiyo kwa mara ya kwanza..nilikuwa sijui bei yake kwa hapa bongo...kwa wale walioishi kidogo america ya kaskazini...hao bata wanaliwa sana wakati wa mwezi huo ujao na huu pia...nilikuwa nakula tu vipande vidogo ila sikujua bei yake...ukienda kwenye store zingine unaweza ona paja lake kama la mbuzi mdogo, ni wakubwa sana...ila bei yake inakuwa kubwa kwasababu huwa wanaliwa kitradition zaidi kuliko kiwingi wa nyama...ni sawa na mtu kuthamini sana ndafu wakati wa harusi wakati hata kuku unaweza kumbanika ukamweka pale..au hata kondoo unawezabanika ukaweka pale, ila anaweza garimia garama kubwa alimradi awe ndafu wa mbuzi....natamani kufuga haya ili niwe nakula mayao yao..
 
Vipi kuhusu mayai ya bata mzinga yanapatikana wapi?
Mimi pia ninao ukweli yai lake moja ni sh elfu tano tu mawili elfu kumi. Ukweli hawa ndege ni watamu sana na ni bei kubwa kutokana na tamaduni za wenzetu wanazitumia sana, na pia ukuwaji wao ni shughuli kidogo kama ni mtu wa kukata tamaa haraka utaishia kuwaweka pambo tu bila kuongezeka wale ulioanza nao, maana hawataki shida. Nemyingwa Mhina
 
Uko Dar au mkoani,nijulishe tafadhali.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom