Soko kuu la Njombe limejengwa kwa viwango duni sana

King Bill

JF-Expert Member
Feb 8, 2021
685
1,000
Nipo mjini Njombe kwa zaidi ya wiki moja sasa. Njombe ni mji mzuri wenye shughuli nyingi za uchumi. Shughuli za uzalishaji wa mbao, kilimo cha parachichi na vanilla ni miongoni mwa zile zinazobamba mno.

Nimetembelea soko kuu la Njombe ambalo jiwe la msingi la ujenzi wake liliwekwa na Mh Jafo, Agosti mwaka jana 2020. Ujenzi wa soko hili umekamilika na limeshaanza kutumika. Design ni nzuri likiwa na mifumo ya kisasa ya kuzima moto na jenereta mbili za umeme wa dharura.

Hata hivyo,workmanship ni very poor! Sakafu na plaster zimeanza kubomoka! Kwa ujumla,kwa kuangalia tu kwa macho,viwango havijazingatiwa kabisa.

Halikadhalika, jenereta za dharura hazifanyi kazi! Jazijawahi kufanya kazi! Wafanyabiashara wa soko hilo wanadai waliambiwa zinafua umeme mkali hivyo zikiwashwa zitaunguza vifaa vyao.

Kwa kuwa mradi huu umegharimu mabilioni, fedha za walipakodi au mikopo ambayo watalipa wananchi wa Tanzania,nimuombe waziri Ummy Mwalimu aunde tume ya kuchunguza mradi wa ujenzi huu, na wale wote watakaobainika kuhusuka na uzembe/ufisadi huu wachukuliwe hatua. Kwa performance hii, mkandarasi aliyetekeleza mradi huu asipewe kazi yoyote tena na serikali ya Tanzania.

Kazi iendelee.....
 

Afande Tanzania

JF-Expert Member
May 3, 2020
460
1,000
Hiyo mwka 2020 ulikuwa ni utawala wa shujaa! Hakuna jema, hakuna alilofanya bila kuiba, iwe yeye binafsi au kupitia watendaji wake! Tulipigwa sana na mwendakuzimu.
 

ANKOJEI

JF-Expert Member
Nov 11, 2010
1,000
2,000
yaani mwendazake hakuna aliachokifanya, nchi ilikaribia kufa, wafanyakazi walipata mishahara tarehe46
 

Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,715
2,000
Haaaaa eti umeme mwingi utaunguza vitu
Halafu generator haifanyi kazi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom