Soko Kuu la Masasi linaungua moto

Mwakalinga Bujo

JF-Expert Member
Oct 22, 2008
2,719
1,440
Soko la Masasi, Mkoa wa Mtwara linateketea kwa Moto mida hii na hakuna juhudi zozoe za kuuzima mto huo.

=======Muendelezo======

Chanzo cha ajali hadi sasa hakijajulikana.Gari la zima moto ndio limeingia saa hii.

Tangia muda wa saa tano usiku huu soko kuu la Masasi (Mkuti ) linaungua kutokana na shoti ya Umeme na hadi naliport hakuna juhudi za Serikali za kuzima moto huo zaidi ya local ways zinazotumiwa na wanainchi.

Ila hata hivyo moto umewashinda na kilichobaki sio kuzima bali.ni kuokoa vichache vitavyopatikana na hasa sehemu ambazo moto haujadaka.

Moto ni mkubwa kiasi wenye mali wamelazimika kulia, na kumshukuru Mungu kwani katwaa neema yake.

IMG-20150624-WA0017.jpg

Capture.PNG
 
Halmashauri haina Fire and Rescue unit?

Maana huko foleni hamna ni kitendo cha dakika tatu gari inafika
 
Inasemekana moto ni mkubwa sana na chanzo inasadikika ni shoti ya umeme lakini kwa aliyekaribu zaidi atupe news zaidi
 
Gar la Zimamoto la halmashaur lipo lakin limegeuzwa kua gar la matangazo, pia tank la maj la gar ilo ni dogo kuliko tank la mafuta.

POLENI SANA WAFANYA BIASHARA WALIOPOTEZA MALI ZAO. INAUMA SANA
 
Tangia muda wa saa tano usiku huu soko kuu la Masasi (Mkuti ) linaungua kutokana na shoti ya Umeme na hadi naliport hakuna juhudi za Serikali za kuzima moto huo zaidi ya local ways zinazotumiwa na wanainchi.

Ila hata hivyo moto umewashinda na kilichobaki sio kuzima bali.ni kuokoa vichache vitavyopatikana na hasa sehemu ambazo moto haujadaka.

Moto ni mkubwa kiasi wenye mali wamelazimika kulia, na kumshukuru Mungu kwani katwaa neema yake.
 
jamani wana masasi poleni sana daaaaaah maisha yanarudishwa na uzembe mdogo sana yaaan
 
Inasikitisha kuona gvt haipo, huku kodi zetu zinaishia kwenye mishahara na marupurupu ya watu wasiyozidi millio 2
 
Limeungua maeneo ya vibanda vyote
Lakin maduka yameungua machache
 
Nianze Kwa Kuwapa Pole Waathirika Wa Tukio Hilo La Moto Kuunguza Sokokuu La Mkuti-Masasi.
Pili, Nitoe Rahi Kwa Watanzania. Umefika Wakati Shirika La Umeme (tanesco) Liwajibishwe Kama Kweli Itathibitika Chanzo Cha Moto Huo Kuwa Ni Umeme.
Tatu, Serikali Ijifunze Kuweka Utaratibu Wa Ku-intervine Majanga Kama Haya. Monduli Ng'ombe Walikufa Kwa Ugonjwa, Wamasai Wakalipwa. Leo Wafanyabiashara Mali Zao Zimeteketea Kwa Moto Serikali Yangu Sikivu Itawatelekeza.

Mwisho, Thamani Ya Maisha Yetu Ipo Mikononi Mwetu! "TUFANYE UAMUZI SAHIHI MWAKA HUU TUACHE KUMTAFUTA MCHAWI".
 
Poleni sana na hamna hata gari ya zima moto hopo hii serikali ya ccm ni shidaaah
 
Back
Top Bottom