SOKO kuu la madini ya dhahabu mkoani Geita kuwahudumia wafanyabiashara wa Jumuiya ya Afrika Mashariki

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1553056501039.png


SOKO kuu la madini ya dhahabu mkoani Geita limeelezwa kuwa na uwezo wa kuwahudumia wafanyabiashara wa madini ya dhahabu wa ndani na kutoka nchi zingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hayo yalibainishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akifungua rasmi soko hilo juzi na kutoa mwito kwa wafanyabiashara wote wa dhahabu nchini na nje ya nchi kulitumia soko hilo.

Alisema kutokana na utaratibu mzuri wa huduma za uhamiaji zilizowekwa katika soko hilo pamoja na huduma za kibenki, ikiwemo ubadilishaji wa fedha za kigeni, zitawasaidia wafanyabiashara wa madini ya dhahabu kutoka nchi zingine zikiwemo za Afrika Mashariki na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuhudumiwa vizuri bila kikwazo.

“Wafanyabiashara wa madini kutoka nje ya nchi, leteni dhahabu zenu na kuziuza hapa, tunawakaribisha wafanyabiashara wote iwe kutoka DRC, Rwanda na nchi zingine kuka kuuza dhahabu zenu hapa,”alieleza Waziri Mkuu. Kwa kuwa baadhi ya mabenki ikiwemo Azania, NMB na CRDB zimeshafungua matawi yao katika soko hilo, akizungumza kwa niaba ya benki zote hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa huduma za ubadilishaji wa fedha za kigeni zinatolewa sokoni hapo kupitia benki hizo.

Nsekela alisema benki hizo zimejipanga kuhakikisha upatikanaji wa fedha kwa wateja unakuwa rahisi. Kuhusu kutoa mikopo kwa wachimbaji wadogo, Nsekela alimhakikishia Waziri Mkuu kuwa mabenki hayo yamejipanga kuanza kutoa mikopo kwa wajasiriamali wakiwemo wachimbaji wadogo wa madini. Hata hivyo, Waziri Mkuu ameyataka mabenki nchini kupunguza riba ili wakopaji wamudu kulipa mikopo hiyo.

Aidha, Waziri Mkuu aliwahakikishia wachimbaji wadogo na wafanyabiashara wa madini hayo kuwa soko hilo ni mwarobaini dhidi ya dhuluma na upunjwaji fedha uliokuwa ukifanywa na baadhi ya wanunuzi wa madini hayo hapa nchini. Majaliwa alisema soko hilo ni muhimu kwa kuwa litasaidia kuifanya biashara ya madini kuwanufaisha watu wote wanaohusika kutokana na utaratibu mzuri uliowekwa katika soko tangu muuzaji anapoingia hadi hatua ya mwisho ya kupata malipo yake.

Alisema mauzo ya dhahabu yatakuwa yakizingatia bei elekezi ya siku husika na mnunuzi hapaswi kununua dhahabu chini ya bei elekezi ambapo kwa juzi, bei elekezi ya dhahabu ilikia Sh 95,328.91 kwa gramu moja, kitu ambacho alisema kitaondoa dhuluma na kupunjwa fedha kwa wachimbaji au wauzaji wa madini hayo. Akiwa kwenye moja ya maduka ya kununulia dhahabu ndani ya soko hilo, Waziri Mkuu alishuhudia kipande kidogo cha dhahabu halisi iliyokia asilimia 95.3 kikiuzwa kwa Sh milioni 13.

“Soko hili lina faidi nyingi, litasaidia serikali kupata mapato, kujua kiasi cha dhahabu kinachozalishwa na kuuzwa nje, na kwa kuwa mlengwa mkuu wa soko hili ni mchimbaji mdogo, nawaagiza Wizara ya Madini na Tume ya Madini shirikianeni na Serikali za Mitaa, Osi ya Mkuu wa Mkoa katika kusimamia soko hili ili kudhibiti wezi na wanyang’anyi,” alieleza Waziri Mkuu. Kutokana na umuhimu wa soko hilo, Waziri Mkuu amezitaka mamlaka husika kuhakikisha ulinzi wa soko unaimarishwa wakati wote, lakini pia Watanzania walitangaze soko hilo kila mahali ndani na nje ya nchi ili lizidi kustawi kwa maslahi ya wananchi wote.
 
Back
Top Bottom