Soko kuu la dhahabu lazinduliwa Chato, Waziri Biteko atoa maagizo

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,874
Leo katika viunga vya Chato kumezinduliwa soko kuu la dhahabu. Hivi kumbe haya masoko ni kwa kila wilaya? Maana makao makuu pale Geita napo pana mjengo wa soko la dhahabu.

Hongera Chato kwa kuyafikia maendeleo ya kweli. Unapaa kwa kasi kweli kweli.

=====

Soko kuu la dhahabu lazinduliwa Chato, Waziri Biteko atoa maagizo

Muonekano wa soko la dhahabu Chato

Muonekano wa soko la dhahabu Chato lililozinduliwa leo Ijumaa Desemba 27,2019 na waziri wa madini, Dotto Biteko.

Kwa ufupi
Wizara ya madini nchini Tanzania, Doto Biteko amezindua soko kuu la dhahabu wilaya ya Chato mkoani Geita huku akitoa maagizo kwa ofisi ya madini mkoani Geita kutoa leseni za uchenjuaji kwa wafanyabiashara wa madini zaidi ya 300 wenye mitambo ya kuchenjua dhahabu mkoani humo.

Chato.
Wizara ya madini nchini Tanzania inakusudia kuingiza biashara ya madini kwenye mfumo wa kidigitali ili kuepuka utoroshwaji wa dhahabu kwenda nje ya nchi hiyo.
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameyasema hayo leo Ijumaa Desemba 27,2019 wakati wa uzinduzi wa soko kuu la dhahabu Chato mkoani Geita lililojengwa eneo la Buseresere wilayani Chato mkoani Geita.

Amesema kuingia kwenye mfumo wa digitali kutamsaidia mchimbaji kufanya biashara kidigitali ambapo mchimbaji atatoa taarifa za kuuza dhahabu kwa kutumia ujumbe mfupi na kwamba ili liwezekane mialo yote lazima isajiliwe na kupewa namba.

Biteko ametaka shughuli ya kusajili mialo (eneo la kusafisha udongo unaosadikiwa kuwa na dhahabu) lifanyike kwa uadilifu na kuwataka wachimbaji na wafanyabiashara kuacha kuweka mialo kila eneo.

“Nia yetu ni moja, tunataka kujua dhahabu inayozalishwa imetoka wapi baada ya muda sio mrefu tunatengenea mfumo ambao mchimbaji hahitaji kutembea na makaratasi yeye atatuma tu meseji ambayo itamtambalisha akiwa popote akielekea sokoni atakua kwenye mfumo ambao yeye, ofisa madini na mtu wa wizara ndio watakua na taarifa,” amesema Biteko

Aidha ametoa siku saba kwa ofisi ya madini mkoani Geita kutoa leseni za uchenjuaji kwa wafanyabiashara wa madini zaidi ya 300 wenye mitambo ya kuchenjua dhahabu mkoani humo ambapo alisema wafanyabiashara kufanya kazi bila kuwa na leseni ni kuisababishia serikali hasara na haikubaliki.

Waziri Biteko amewataka wachimbaji kuachana na biashara ya kujionyesha kwa kupanga kreti za bia na kuwataka wachimbe kibiashara ,walipe kodi na wawekeze kwenye miradi ya kimaendeleo ili kuongeza kipato chao na jamii inayowazunguka
Akizungumzia uwepo wa masoko Geita, Biteko amesema kwa sasa yapo masoko 29 ya madini nchini huku nane kati ya hayo yakiwa mkoani Geita ambapo alisema uwepo wa masoko hayo umewezesha kuongeza mapato ya serikali kutoka Sh1 bilioni zilizokuwa zikizalishwa awali na sasa Serikali inapata zaidi ya Sh234 bilioni kwa mwezi.
Awali, Waziri wa nishati, Dk Merdad Kalemani ambaye pia ni mbunge wa Chato ameiomba wizara ya madini kutoa vibali kwa madalali wa dhahabu ili waweze kusafirisha kwenda nje ya nchi tofauti na sasa vibali vyao ni vya ndani ya mkoa pekee.
 
Leo katika viunga vya Chato kumezinduliwa soko kuu la dhahabu. Hivi kumbe haya masoko ni kwa kila wilaya? Maana makao makuu pale Geita napo pana mjengo wa soko la dhahabu.

Hongera Chato kwa kuyafikia maendeleo ya kweli. Unapaa kwa kasi kweli kweli.

View attachment 1304965
Tanzania ya Magufuli ni Tanzania ya Viwaaaanda
 
Jamani, tatizo liko wapi?? Mlitaka hizi rasilimali zetu ziendelee kuibwa kila siku?? Huku walijaa wakutoka nje tu. Wakaja na vifedha vyao wakavibadili mpakani kwa njia mbaya. Wakaingia humu nchini na kutunyonya. Leo mmejengewa mahali sahihi pa kuiuza dhahabu yenu wenyewe mnabeza?? Hapana, hii nasema sio vyema. Jengo la dhahabu mnataka liwe la udongo?? Tuleteeni basi michoro
 
Sijawahi kuona kiongozi mwenye uoendeleo kama tuliye naye sasa.

Hajaanza leo, kumbuka alipo kuwa waziri wa ujenzi aliwahi kupeleka taa za kuongozea magari sehemu ambayo ina magari hata 100 hayazidi.

Ni ubinafsi mkubwa , hata jengo lake ambalo ameweka tausi toka ikulu ni uhinafsi mkubwa kwa sababu ukisha chaguliwa kuwa Rais tunakupa nyumba ambayo ni ikulu na baada ya kutoka kuna utaratibu wa kujengewa nyumba , sasa yeye amejibegea jengo kama hoteli .

Tusipo angalia tutapata shida sana kwa huu utawala.

Mungu mlinde JK na mkapa na warioba , maana hawa ndio pekee wameshikilia msimamo wa katiba.

Mwinyi sijui kapewa nini katiba kesha ikanyaga, pinda ndio kabisa.. wengine hawaeleweki msimako wao.

Tunahitaji katiba mpya itakayo zuia mambo mambo kama haya.

Atatokea mtu siku moja akaingiza kwenye chama kabila lake tuu na viongozi kabila lake tuu kisha akapata urahisi wa kuikanyaga katiba kwa kigezo cha watu wanamtaka aendelee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingejengwa kaskazini usingeongea haya
 
Jamani, tatizo liko wapi?? Mlitaka hizi rasilimali zetu ziendelee kuibwa kila siku?? Huku walijaa wakutoka nje tu. Wakaja na vifedha vyao wakavibadili mpakani kwa njia mbaya. Wakaingia humu nchini na kutunyonya. Leo mmejengewa mahali sahihi pa kuiuza dhahabu yenu wenyewe mnabeza?? Hapana, hii nasema sio vyema. Jengo la dhahabu mnataka liwe la udongo?? Tuleteeni basi michoro
Jamani, tatizo liko wapi?? Mlitaka hizi rasilimali zetu ziendelee kuibwa kila siku?? Huku walijaa wakutoka nje tu. Wakaja na vifedha vyao wakavibadili mpakani kwa njia mbaya. Wakaingia humu nchini na kutunyonya. Leo mmejengewa mahali sahihi pa kuiuza dhahabu yenu wenyewe mnabeza?? Hapana, hii nasema sio vyema. Jengo la dhahabu mnataka liwe la udongo?? Tuleteeni basi michoro
Acha kupindisha mada wewe...
 
Leo katika viunga vya Chato kumezinduliwa soko kuu la dhahabu. Hivi kumbe haya masoko ni kwa kila wilaya? Maana makao makuu pale Geita napo pana mjengo wa soko la dhahabu.

Hongera Chato kwa kuyafikia maendeleo ya kweli. Unapaa kwa kasi kweli kweli.

View attachment 1304965
Naunga mkono maendeleo yote ya Chato

P
 
Kuna maoni ya baadhi ya watu wa Ufipa ukisoma unaweza jiuliza hawa wanawaza kutumia magoti Au ubongo??

Pungezeni mihemuko Vijana..

Viva JPM
Kama hata hilo hulioni kama tatizo unadhani utakuwa unafikiri kutumia nini wewe?
Ni kiungo kimoja tuu kinatoa bila kufikiri hata rangi ya kilichotoka ni nini, may be hata kufikiri unatumia hicho!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom