Soko kuu arusha, biashara hadi barabarani

Saharavoice

JF-Expert Member
Aug 30, 2007
3,857
2,345
Baada ya shughuli za uchaguzi mkuu kwisha, inaonekana wafanyabiashara maeneo ya soko kuu Arusha wameamua kufanyia biashara zao katikati ya barabara kiasi kwamba inakuwa vigumu kupita na gari kwenye barabara zilizo pembezoni mwa soko hilo.

Sina hakika kama Mkurugenzi wa jiji ameamua kufumba macho, au kuna mkono wa siasa ndani yake, lakini kwa kweli ni karaha kupita maeneo hayo hasa ukiwa na gari.
 
Waliruhusu wakati wa kampeni, sasa hivi wana hasira baada ya kushindwa, wanataka G.Lema aje awatoe.
 
Kama wanauza tisheti walizogawiwa wkt wa uchaguz waacheni mpaka wamalize
 
kwa kweli inatia kero...halafu leo nimegundua kitu kingine, mchana kwenye mida ya saa nane mvua ilinyesha kidogo ilivyokatika na maji kukauka ilibaki harufu ya mikojo barabara nzima huu upande wa jubilee tyres, na maeneo hayo wamama ndio hutandaza bidhaa zao chini...hivi tutapona kweli kwa mtindo huu...na huyo anayekojoa huko barabarani ni nani?
 
watu ndio watakuwa wamekojoa ..au unandani hilo kojo lililetwa ? poleni lakini
 
asante...ama kweli watu ni zaidi ya tuwajuavyo.....lakini kwa nini waende wakakojoe barabara za sokoni?
 
si vyoo vya umma havipo..ok kama vipo havifanyiwi usafi.. yote hayo ni mambo ya uongozi..halmashauri sijui nini huko wanapewa fungu au wanakata kodi ili washughulikie mambo yote haya ..hope unanainyaka sister...ninavyopapenda Arusha ..we acha tu nikisikia hivi roho inaniuma
 
Ivuga endelea kupapenda tu lkn hali ya usafi huku ni tete achilia mbali mpangilio mzima wa jiji.
 
arusha_town.jpg
 
watu ndio watakuwa wamekojoa ..au unandani hilo kojo lililetwa ? poleni lakini

Siyo watu ni miundo mbinu ya kutolea maji machafu imezidiwa na maghorofa yaliyootesha kiasi kwamba mvua kidogo tuu mitaro yote inaziba. Nadhani kwenye ule mdahalo mgombea wa TLP alilizungumzia hili tatizo kwa kirefu na ufumbuzi wake
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom