Soko huria ndiyo sababu kubwa inayofanya nchi za Kiafrika zisiendelee

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Soko huria, hasa hili soko huria la kulazimishana ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi maskini.

Kanuni ya soko huria ni kuondoa vikwazo vya biashara kati ya nchi na nchi. Watetezi wake wanadai kuwa ni njia rahisi ya kuleta maendeleo. Lakini kiukweli siyo kabisa. Nchi zote zilizoendelea zilikuwa kinyume kabisa na soko huria. Zilizuia bidhaa kutoka nje kwa kuweka kodi kubwa, kusingizia usalama, ubora na marufuku. Jambo hili lilifanya viwanda vyao vya ndani kukua.

Vilipokuwa na kuweza kushindana ndipo wakaanza kuhubiri soko huria. Hiki kipindi cha protectionism ndicho kilifanya viwanda vyao vichanga kukua. Nchi zote zilizoendelea zimepitia njia hii. Hakuna nchi imewahi endelea kwa kufuata sera za soko huria.

Sababu kuu inayofanya nchi za kiafrika zote kubaki maskini ni kuruhusu soko huria. Na mbaya zaidi nchi zilizoendelea zinazilazimisha nchi maskini kufuata soko huria. Vyombo kama WTO, WB, IMF, AGOA nk vipo kwaajili ya kuhakikisha nchi zote zinafuata soko huria.

Nchi zikienda tofauti zinaadhibiwa. Nchi za EA zilipotaka kupiga marufuku mitumba ili kukuza viwanda vya ndani AGOA ilitishia kuziadhibu.

Lakini hizohizo nchi zikiona soko linawaendea vibaya wanakwepa soko huria kwa visingizio kibao. China ilizikataa Google, Facebook na paypal kwa kusingizia usalama. Marekani imeipiga marufuku Huawei kwa kusingizia usalama.

Nchi za Afrika zitaendelea zitapotambua kuwa adui yao ni soko huria na pale zitakapopata kiongozi mwenye ujasiri wa kupingana na matajiri huku raia wake wakiwa tayari kufunga mikanda ili kukuza viwanda vya ndani.
 
Kabla hatujaenda huko kwa wazungu, adui yetu namba moja ni viongozi wetu wenyewe. Hiyo fulsa ya AGOA, tulifanya nini?kama sisi kwa sisi tu afrika tunachawiana kuhusu biashara, Kenya na Tz, tulikuwa kwenye mzozo wa kibiashara , Rwanda na Uganda hadi leo karibia mwaka wa 2, wamefungiana mipaka!

Huyo kiongozi unayemsema eti mwenye uthubutu wa kupigana na matajiri ili kukuza viwanda vya ndani, hapa si alikuwepo MEKO? kwa miaka hiyo mitano kuna nini cha maana alichokifanya? Zaidi ya kuturudisha nyuma tu?kwa sera zisizotekelezeka, viko wapi hivyo viwanda 8000, alivyosema ni vipya?

Kwanza hilo soko hulia utalikwepa vipi wakati wewe mwenyewe karibia kila kitu unategemea kuagiza?leo hii tu weka kodi kubwa kwenye sukari, mafuta ya kula, kutoka nje uone kitakachotokea?huo ni mkakati wa muda mrefu sana, ili uuweze, na kwa Afrika ni ngumu, kila kiongozi anayekuja anaanzia pale anapotaka yeye, na sio dira ya taifa?!!hapo kuna muendelezo kweli?

Miaka 60 ya uhuru, bado vyoo navyo ni tatizo, madawati, madarasa kila mwaka ni kukimbizana tu, sembuse kwenye maji huko na umeme?
Sio kila matatizo ni wazungu mengi ni sisi wenyewe, tuna WATAWALA, na sio viongozi.
 
Unavyofanya protectionism hakikisha pia unasaidia viwanda vya ndani kukua. Mfano ukipiga marufuku Sukari kutoka nje basi hakikisha unasaidia raia wako kuanzisha mashamba ya miwa na viwanda vya sukari. Baadaye raia wako wakiwa na uwezo mkubwa ndipo uanze kuhubiri soko huria. Nje zote zilizoendelea zimetumia njia hiyo. Lakini muhimu lazima raia wawe tayari au walazimishwe kufunga mikanda. Maana kutakuwa na kipindi cha mpito cha uhaba.
 
Raia wapi hao walioko tayari kufunga mkanda? 😂 Hawa hawa wabongo wenzangu au wepi hao?
Shida inakuwaga hapo. Na kwenye demokrasia ni ngumu sana kuwafungisha watu mikanda. Kelele ni nyingi Ndiyo maana vitu kama hivi vinahitaji mtu mbabe. Ndiyo maana AGOA waliposema kuwa tukipiga marufuku mitumba watatutoa kwenye huo mpango ni Kagame peke yake alibaki na msimamo. Hawa wengine walifyata.
 
Unavyofanya protectionism hakikisha pia unasaidia viwanda vya ndani kukua. Mfano ukipiga marufuku Sukari kutoka nje basi hakikisha unasaidia raia wako kuanzisha mashamba ya miwa na viwanda vya sukari. Baadaye raia wako wakiwa na uwezo mkubwa ndipo uanze kuhubiri soko huria. Nje zote zilizoendelea zimetumia njia hiyo. Lakini muhimu lazima raia wawe tayari au walazimishwe kufunga mikanda. Maana kutakuwa na kipindi cha mpito cha uhaba.
Ni kweli kabisa mkuu!!lakini kwa viongozi gani hawa tulio nao?wao akili zao ni kuweza kujihakikishia kubakia madarakani, na kuweka watu wake, tu, mtafunga mikanda hadi itakatika na hakuna la maana!!mfano awamu ya 5, si walituaminisha kuwa sasa tunaacha kutegemea wazungu pesa tunayokila kitu ni pesa yetu?

Leo hii hii wale wale wanaanza kutilia mashaka ukubwa wa deni la taifa, na thamani halisi ya hiyo miradi?!!nani atakubali kuwekeza kwenye nchi ambayo sera zake hazitabiriki?kesho anakuja huyu anasema hayo makubaliano yenu ya huko nyuma siyatambui!!!nataka hivi!!WAAFRIKA PIA TUNA UPIMBI MWINGI SANA.na huo ndio mtaji wa viongozi wetu.
 
Ni kweli kabisa mkuu!!lakini kwa viongozi gani hawa tulio nao?wao akili zao ni kuweza kujihakikishia kubakia madarakani, na kuweka watu wake, tu, mtafunga mikanda hadi itakatika na hakuna la maana!!mfano awamu ya 5, si walituaminisha kuwa sasa tunaacha kutegemea wazungu pesa tunayokila kitu ni pesa yetu??leo hii hii wale wale wanaanza kutilia mashaka ukubwa wa deni la taifa, na thamani halisi ya hiyo miradi?!!nani atakubali kuwekeza kwenye nchi ambayo sera zake hazitabiriki?kesho anakuja huyu anasema hayo makubaliano yenu ya huko nyuma siyatambui!!!nataka hivi!!WAAFRIKA PIA TUNA UPIMBI MWINGI SANA.na huo ndio mtaji wa viongozi wetu.
Waafrika Ni nyani tuliochangamka tu.
 
Wenzako wanapoweka sera za kujifungia "protectionism" huwa na bidhaa mbadala nchini mwao. Wewe unataka uzuiwe kuvaa nguo za vunja Bei kutoka China ile uvae kaniki?
 
Hapa serikali inakuwa inafanya protectionism huku ikisaidia wazalishaji wa ndani hadi pale watakapoweza kushindana kimataifa. Ni suala linalohitaji umakini na tahadhari.
 
Soko huria, hasa hili soko huria la kulazimishana ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi maskini.

Kanuni ya soko huria ni kuondoa vikwazo vya biashara kati ya nchi na nchi. Watetezi wake wanadai kuwa ni njia rahisi ya kuleta maendeleo. Lakini kiukweli siyo kabisa. Nchi zote zilizoendelea zilikuwa kinyume kabisa na soko huria. Zilizuia bidhaa kutoka nje kwa kuweka kodi kubwa, kusingizia usalama, ubora na marufuku. Jambo hili lilifanya viwanda vyao vya ndani kukua.

Vilipokuwa na kuweza kushindana ndipo wakaanza kuhubiri soko huria. Hiki kipindi cha protectionism ndicho kilifanya viwanda vyao vichanga kukua. Nchi zote zilizoendelea zimepitia njia hii. Hakuna nchi imewahi endelea kwa kufuata sera za soko huria.

Sababu kuu inayofanya nchi za kiafrika zote kubaki maskini ni kuruhusu soko huria. Na mbaya zaidi nchi zilizoendelea zinazilazimisha nchi maskini kufuata soko huria. Vyombo kama WTO, WB, IMF, AGOA nk vipo kwaajili ya kuhakikisha nchi zote zinafuata soko huria.

Nchi zikienda tofauti zinaadhibiwa. Nchi za EA zilipotaka kupiga marufuku mitumba ili kukuza viwanda vya ndani AGOA ilitishia kuziadhibu.

Lakini hizohizo nchi zikiona soko linawaendea vibaya wanakwepa soko huria kwa visingizio kibao. China ilizikataa Google, Facebook na paypal kwa kusingizia usalama. Marekani imeipiga marufuku Huawei kwa kusingizia usalama.

Nchi za Afrika zitaendelea zitapotambua kuwa adui yao ni soko huria na pale zitakapopata kiongozi mwenye ujasiri wa kupingana na matajiri huku raia wake wakiwa tayari kufunga mikanda ili kukuza viwanda vya ndani.
Huo ndio ukweli mtupu. Viongozi mazuzu ndio wanakubali huu uongo wa soko huria. Unataka kujenga viwanda ili watu wako wapate ajira halafu unakubali sukari ya brazil ishindane na ya kiwanda nchini mwako. Brazil au pakistani wanazalisha tani maelfu kwa siku sukari ikija hapa bado bei iko chini kuliko yako. Viwanda ndio maendeleo. Sasa nchi kubwa yenye resources kama tanzania tutakubali tuwe soko milele? Kila aliyeweza kuendelea alifanya protectionism. Wajinga tu ndio wanadanganywa.
Hawa wafanyabiashara wahindi wa kuagiza bidhaa lazima kupambana nao wasihujumu ukuuji wa viwanda.
 
Soko huria, hasa hili soko huria la kulazimishana ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi maskini.

Kanuni ya soko huria ni kuondoa vikwazo vya biashara kati ya nchi na nchi. Watetezi wake wanadai kuwa ni njia rahisi ya kuleta maendeleo. Lakini kiukweli siyo kabisa. Nchi zote zilizoendelea zilikuwa kinyume kabisa na soko huria. Zilizuia bidhaa kutoka nje kwa kuweka kodi kubwa, kusingizia usalama, ubora na marufuku. Jambo hili lilifanya viwanda vyao vya ndani kukua.

Vilipokuwa na kuweza kushindana ndipo wakaanza kuhubiri soko huria. Hiki kipindi cha protectionism ndicho kilifanya viwanda vyao vichanga kukua. Nchi zote zilizoendelea zimepitia njia hii. Hakuna nchi imewahi endelea kwa kufuata sera za soko huria.

Sababu kuu inayofanya nchi za kiafrika zote kubaki maskini ni kuruhusu soko huria. Na mbaya zaidi nchi zilizoendelea zinazilazimisha nchi maskini kufuata soko huria. Vyombo kama WTO, WB, IMF, AGOA nk vipo kwaajili ya kuhakikisha nchi zote zinafuata soko huria.

Nchi zikienda tofauti zinaadhibiwa. Nchi za EA zilipotaka kupiga marufuku mitumba ili kukuza viwanda vya ndani AGOA ilitishia kuziadhibu.

Lakini hizohizo nchi zikiona soko linawaendea vibaya wanakwepa soko huria kwa visingizio kibao. China ilizikataa Google, Facebook na paypal kwa kusingizia usalama. Marekani imeipiga marufuku Huawei kwa kusingizia usalama.

Nchi za Afrika zitaendelea zitapotambua kuwa adui yao ni soko huria na pale zitakapopata kiongozi mwenye ujasiri wa kupingana na matajiri huku raia wake wakiwa tayari kufunga mikanda ili kukuza viwanda vya ndani.
Hata nchi zilizoendelea zilipiga hatua kwa soko huria..
Produce quality products and you will sell.
Mawazo yako ni ya kijamaa,mfumo uliofeli big time.
 
Afrika mashariki, Kenya ipo juu kiuchumi, ukiruhusu soko huria Kenya watazidi kupeta. Mf wembe wa Tz ni 200 na wa Kenya ni 200, ila wa Tz ni butu ninunue upi?
 
Hakuna
Hata nchi zilizoendelea zilipiga hatua kwa soko huria..
Produce quality products and you will sell.
Mawazo yako ni ya kijamaa,mfumo uliofeli big time.
Katika nchi tajiri hakuna hata moja iliyoendelea kwa soko huria. Itaje kama unaijua.
 
Yap, Nimemsoma mwaka huu. Kuna huyu jamaa My Next Thirty Years alimlicommend. Ndiyo nimejionea huo ukakasi wa soko huria na mambo mengine ambayo nchi tajiri zinatulazimisha kufuata. Kitabu safi sana.
Safi Sana mkuu; Kama ukipata muda soma vitabu vyake vyote huyu bwana ha Chang.

Ukisoma vitabu vyake kwa umakini na kisha kuwaangalia viongozi wetu na wachumi wetu ni kama Unataka kukata tamaa, tutatoka kweli katika dimbwi hili la umasikini au tutaendelea kuzunguka mbuyu..

Katika maandishi yake utapata Historia walau iliyonyoka kuhusu Demokrasia,Soko huria,Mapinduzi ya Viwanda na Suzuki,toZo,ushuru na taasisi mbalimbali bila kusahau unholy Trinity" IMF WORLD BANK WTO"
 
Shukrani, nitamfuatilia. Inaonekana tunayofundishwa kwenye formal education na yanayofanya kazi duniani ni mambo tofauti kabisa. Nilivyosoma tu Bad Samaritan nikaona jinsi ambavyo situation yetu ni hopeless.
 
Back
Top Bottom