Soko aliloahidi Kileo na Lema kujenga choo cha kisasa laungua moto

MTENGETI

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
2,419
2,000
Wana Jamvi ,
Wakati wa Operation Ondoa Maghembe ilipokuwa inafanyika mwishoni mwa mwezi wa July 2012 Mbunge aliepo likizo wa Arusha Godbless Lema na Mbunge Mtarajajiwa wa kwa Tiketi ya CDM Anold kilewo waliahidi kujenga choo ili kuwastiri watu wanaopata na kutoa huduma katika soko la mji wa Mwanga lililopo Barabara kuu ya Dar _Arusha. Limeungua moto mnamo saa saba Usiku wa kuamkia Leo.
Ahadi hiyo ambayo ilileta mvurugano mkubwa huku CCM wakisema Choo hakitajengwa na kuahidi kuwa watakwamisha kwa uwezo walio nao ikiwemo kuhujumu hata kama HALMASHAURI ITARIDHIA UJENZI HUO.

Lakini pia mnamo mwezi Oktober Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga iliongoza Operation ya Kutaifisha Vibanda vya Masoko yote ikianzia Soko la Mji Mpya ambapo walikutana na wakati mgumu baada ya nguvu ya Umma kuzuia utaifishaji huo na hatimae vurugu kutokea huku Mweka hazina wa Wilaya akitishia kwa kutoa mifano ya kilichotokea katika masoko ya Moshi, Stand na Mbeya kuwa ndio kitakachotokea Mwanga kwa siku za baadae.

Nadhani alichoahidi DT ndio hicho kilichoanza jana usiku katika soko la Old Mwanga.
Bado tunafanya tathmini ya hasara iliyotokea kwani hasara ni kubwa mno kuna maduka ya jumla na rejareja mengi ambayo yameungua usiku wa kuamkia leo.

Naomba kuwasilisha
 

taamu

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,936
2,000
dah choo tu ndio wachome soko bado kidogo tz itzingirwa na damu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom