kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
Papic raia wa Serbia hajalipwa mishahara ya miezi miwili hadi mitatu na mara kadhaa amewaambia rafiki zake wa karibu kuwa ataondoka na kurejea kwao Ulaya baada ya mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya St Eloi Lupopo iliyochezwa Jumamosi iliyopita mjini Lubumbashi.
Jana, Championi Jumatano lilimsaka na kufanya naye mahojiano maalum naye alisema hivi, Kweli kwa sasa sina tena sababu ya kuficha, sina raha tena hapa Yanga. Ninastahili kuondoka na kuangalia sehemu nyingine.
Unatambua kuwa mambo mengi sana yaliyo katika mkataba wangu na Yanga yamevunjwa. Lakini sikuona sababu ya kuanza kuanika kila kitu mapema kwa kuwa tulikuwa na jukumu kubwa mbele yetu la kuingoa Lupopo, bahati mbaya hatukuweza, alisema Papic baba wa watoto wawili, Todor na Natas na kuongeza.
Kweli sielewi wananichukulia vipi, siwezi kuishi hapa nikifanya kazi halafu fedha ya kuendesha maisha natumiwa kutoka Ulaya. Lakini pia suala la fedha kwangu si kubwa sana hata kama nafanya kazi ili nizipate. Ile hali ya heshima tu, mimi ninaamini wananidharau na kuninyanyasa, wangenilipa ili kuonyesha tu wanajali.
Kila mwezi hadithi ni zile zile, hakuna mabadiliko na ndiyo maana nimewaambia kesho lazima tukutane na uongozi na kulijadili hili. Kama hawatataka kufanya hivyo, sitakuwa na kinyongo, nitabeba mizigo yangu na kuondoka. Ni nguo mbili zilizo nje ya begi langu hadi sasa, alisema Papic akionyesha kuwa na hasira.
Nasema imetosha! Imetosha! Dharau hii siwezi kuivumilia, mkataba wangu umevurugwa, mshahara silipwi na hakuna anayeonyesha kushtuka, alisema kocha huyo aliyeleta mabadiliko makubwa Yanga katika kipindi kifupi ambaye pia amewasilisha maombi ya kuinoa Taifa Stars.
Mkutano huo wa uongozi wa Yanga na kocha huo ndiyo pekee unaoweza kubadili mambo ingawa, hali halisi inaonyesha Papic hatakuwa na muda mrefu ndani ya Yanga kwa madai ya kukasirishwa na hali ya kuonyesha kumdharau.
Papic aliyewahi kuzinoa klabu kubwa kama Enyimba, Lobi Stars (Nigeria), Kaizer Chiefs, Orlando Pirates (Afrika Kusini) alichukua nafasi ya Dusan Kondic raia wa Serbia pia ambaye pia alilazimika kushitaki Yanga TFF ili kulipwa fedha za mshahara wake. Kondic alisema alilipwa dola 18,000 badala ya zaidi ya dola 30,000 alizokuwa akidai.