Software Piracy - Safari Imeanza

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
214
Leo katika pita pita zangu kati kati ya jiji nilifanikiwa kutia mguu katika duka la Prince Samora – karibu na Twiga house hapo mlangoni kuna tangazo kwa herufi kubwa HATUWEKI PROGRAMU BANDIA – MADHARA YA PROGRAMU BANDIA NI – KUKOSA UPDATES NA FACILITIES ZINGINE – HAPA TUNA WINDOWS XP GENUINE , WINDOWS VISTA AINA MBALI MBALI ZOTE NI GENUINE .

Tangazo hili limekuja siku chache baada ya kuepelekewa barua pepe katika maduka kadhaa kuambiwa kwamba wanatakiwa wawaambie wateja wao ukweli kuhusu programu wanazowawekea na ambazo wanazo ili kutoa lawama toka kwao linapotokea tatizo au matatizo kama hayo yanayohusiana na piracy .

Pia nimeona duka la Mitsumi computer garage nalo wakiwa na tangazo linalofanana na ilo ingawa wao walianza kuweka siku nyingi sema tu katika workshop yao kuna copy za cd zingine zimeandikwa win xp sp2 , 1 win 200 au 2003 hii inatia mashaka kidogo kama kweli wanatekeleza majukumu yao ipasavyo .

Kingine maduka au wauzaji hawa wanachotakiwa kufanya ni kuweka tangazo pale kuelezea udhibitisho kama kweli wao ni reseller wa hizi programu la sivyo itaweza kuzusha maswali zaidi hapo mbeleni .

Katika hili ukienda mfano computer connections pale utaona makombe , medali na vyeti vinavyodhibitisha hili kwa mapana na zingine wamesharenue , au ukipita katika duka la pc solutions pale kisutu napo unaona vyeti hivi vya reseller .

Lakini ukifika mfano duka kama la mudy tech – morogoro road hakuna matangazo haya lakini wanainstall na kufanya shuguli zote ambazo unaweza kufanyiwa katika workshop zingine kutumia cd ambazo ni batili .

Kwahiyo kuna watu na biashara zao wamepiga hatua kubwa katika kuhakikisha wateja wao wanapata kile wanachotakiwa kupata ambazo ni haki zao kama watumiaji wa vifaa au programu zile .

Mwisho kabisa tujiulize kama maduka haya yanadata base ya kuhifadhi zile licence zote wanazotoa au kuuza kwa wateja wao , mfano mteja amepoteza yake au imefutika afanyaje ? nimeona kuna ambao wanapoteza sticker za product key na wanashindwa wafanye nini wakati wangerudi katika duka lile wanatakiwa wapatiwa nakala hiyo kwa sababu alinunua hapo
 
Pia nimeona duka la Mitsumi computer garage nalo wakiwa na tangazo linalofanana na ilo ingawa wao walianza kuweka siku nyingi sema tu katika workshop yao kuna copy za cd zingine zimeandikwa win xp sp2 , 1 win 200 au 2003 hii inatia mashaka kidogo kama kweli wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.
Shy, naomba uelezee vizuri hapo juu kwenye wekundu, sijakuelewa, Asante.

Katika hili ukienda mfano computer connections pale utaona makombe , medali na vyeti vinavyodhibitisha hili kwa mapana na zingine wamesharenue , au ukipita katika duka la pc solutions pale kisutu napo unaona vyeti hivi vya reseller .

Lakini ukifika mfano duka kama la mudy tech – morogoro road hakuna matangazo haya lakini wanainstall na kufanya shuguli zote ambazo unaweza kufanyiwa katika workshop zingine kutumia cd ambazo ni batili.
Kwenye hili Shy itabidi uwe umejaribu mwenyewe/au rafikiyo na kuthibitisha. Otherwise ni accusation kubwa, maana evidence ya software ipo kwa wateja wao na Microsoft East Africa wanaweza kutoa tangazo tu hapo kwa wateja wao (something unlikely though), but nasema hivyo kukukumbusha kuwa madai mengine ni lazima uwe umethibitisha kabla ya kuyatoa. Maana njia za kuyafatilia ni rahisi.

Kumbuka inawezekana kabisa mtu akatumia copy ya cd (nukuhu/burned) badala ya original na kutumia genuine licence. Mtu anaruhusiwa kutengeneza copy za software zake kama back up. Hapo hapo unaruhusiwa kuinstall software kutoka backup copy yako alimradi licence iwe genuine. Lakini kumbuka pia kuwa Microsoft wanaruhusu kupata licence online baada ya installation. Hivyo basi kuhusiana na hilo duka, inawezekana kabisa kuwa wana bulk licence ambazo wamenunua kama OEM na hawahitaji kutumia original copy kwa wateja wao kwenye installation process.

Kwahiyo kuna watu na biashara zao wamepiga hatua kubwa katika kuhakikisha wateja wao wanapata kile wanachotakiwa kupata ambazo ni haki zao kama watumiaji wa vifaa au programu zile .

Mwisho kabisa tujiulize kama maduka haya yanadata base ya kuhifadhi zile licence zote wanazotoa au kuuza kwa wateja wao , mfano mteja amepoteza yake au imefutika afanyaje ? nimeona kuna ambao wanapoteza sticker za product key na wanashindwa wafanye nini wakati wangerudi katika duka lile wanatakiwa wapatiwa nakala hiyo kwa sababu alinunua hapo
Samahani, hapo juu naona utakuwa unachemsha, maduka kama reseller hawako obliged to store database ya licence. They are simply outlet of the products. Licence zinatakiwa ziangaliwe na licence issuer (who can be a distributor or software producer and sometimes software designer). Local trading authority na software producer ndiyo wanaotakiwa wawaweke resellers kwenye check ili wasikiuke sheria au agreement za mauzaji ya bidhaa hizo.

Mteja akipoteza licence, ataweza kuipata kwa distributor wa hizo software au producer na siyo reseller. Reseller anaweza kufanya hivyo tu kwa goodwill yake. Lakini pia unaweza kuta sheria nyingi hazimtaki reseller abakie na copy ya license. Ndiyo maana mara nyingi ukinunua software kutoka dukani unapatiwa card ya kuregister au option ya kuregister online. Hii ni kwa ajili ya kukuprotect wewe kama mteja ili kama waliokuuzia ni wakweli au wezi tu, lakini pia (mara nyingi) inakupatia guarantee ya wewe kama unapoteza au kuharibikiwa na computer yako kuweza kupata hiyo licence pale unapofanya reinstallation.

Hata hivyo Shy, kuna kitu hapo una raise, ambacho ni cha muhimu sana. Maana kinaweza kupunguza adha zitokanazo na mambo ya ununuzi wa software. Natoa mfano wa Microsoft kama leader wa software nyingi zinazotumika hapa Bongo. Nacho ni kwamba; Sijui representative wa Microsoft hapa Tanzania, nadhani wana represantative office Nairobi.... basi, kwa kampuni kubwa kama hii, (kama kweli hawana office ya kuwakilisha bongo) mimi naona wanachemsha big time.

Ukienda kwa reseller wengi hapa Bongo nakutaka kununua software genuine, bei zao utafikiri unanunua kutoka ulaya!! Hivyo kutokuwepo kwa office za masoko au utendaji hapa karibu kuna fuel ongezeko la software fake. Kukiwepo na office kama hizi kutasaidia udadisi wa masoko ya hapa na kuwawezesha Microsoft kuleta bidhaa ambazo ziko discounted kwa ajili ya masoko yetu. Programmes kama hizi za 'third world' discounted software wanazo. Kwa kiwango cha uchumi tulio nao Bongo ni muhimu software zinazoletwa hapa zisitegemee wafanyabiashara ambao wananunua software hizo kutoka nchi ambazo ziko discounted lakini wanaziuza hapa Bongo utafikiri ni licence zilizotolewa kwa ajili ya masoko ya Ulaya na Marekani.

Kuwepo kwa local representative kutasaidia pia watu kucheck u-genuine wa licence au software wanazonunua kwa kupiga simu locally hivyo kuendeleza mambo ya hati miliki.

SteveD.
 
Shy, naomba uelezee vizuri hapo juu kwenye wekundu, sijakuelewa, Asante.

Mkuu nafikiri anamaanisha kwamba ameona kuna copy za Windows XP ambazo ziko combined na Service Park 2 ambayo ni baada ya ile ya Serice Park 1.

Pia nafikiri unazijua hizi Service Parks ila kwa faida ya wanaJF wengine, hii ni program ambayo inasaidia computer kuweza kupata updates zote muhimu automatically ikiwemo ya security pale PC au laptop au Server inapokuwa online.

Vitu vote hivi hufanzika bila mwenye computer kulipa chochote kile.

Unajua hapo kabla Service Park ilikuwa ni ya ku-download kutoka website ya microsoft lakini baadae wakaamua kuiongeza katika package nzima ya XP, Windows 2000 na 2003 na sasa Vista ambazo hizi zina Service Park 1 tu.

Vista nayo sasa ina Service Park 1.

Ila natoa ushauri kwa Shy kuwa mwangalifu unapoelezea tuhuma fulani fulani dhidi ya mtu au watu na biashara zao maana watakuhitaji utoe ushahidi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom