Soft Copy kwa Kiswahili ni nakala laini?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
17,871
33,236
Nimeona kwenye Barua iliyoandikwa na ubalozi wetu nchini Oman na Muscat kwamba "Soft copy" Kiswahili chake ni nakala laini. Hebu wajuvi wa Lugha yetu hii adhimu tusaidieni kama tafsiri hii ni sahihi.
 
Ofisi nyingi sana wanaita hivyo, hali kadhalika "Hard copy inaitwa nakala ngumu"
Na mimi niko hapa kupata ufafanuzi
 
Nimeona kwenye Barua iliyoandikwa na ubalozi wetu nchini Oman na Muscat kwamba "Soft copy" Kiswahili chake ni nakala laini. Hebu wajuvi wa Lugha yetu hii adhimu tusaidieni kama tafsiri hii ni sahihi.
Nadhani ulitakiwa kwanza utudokeze mashaka yako unayaelekeza wapi na kwa sababu ipi?
Kumbuka Tafsiri za matini ni ngumu kulingana ila hukaribiana kimaana.
Pendekeza pia ulitaka iweje kwani mapinduzi ya msamiati katika lugha yanakubaliwa endapo haja itakuwepo.
 
Kutafsiri si kuweka maneno kandokando. Hii haina maana. Nakala laini ni kichekesho.
Ujiulize kwanza maana yake ni nini.
Hard copy - a document printed on paper (si ngumu!!! kama ingechongwa kwenye jiwe au kukatwa katika chuma ingekuwa ngumu)
Soft copy: a document available in digital format

Mandharinyuma ya lugha hii ni "hardware - software"
"Hardware" ni sehemu za kompyuta zinazofanywa na plastiki, metali nk. (hapa kuna ugumu kiasi.. kwa hiyo Kiwahili chake si "bidhaa ngumu" - ni maunzi ya kompyuta)
"Software" - neno hili lilitungwa mnamo 1958 kutaja yale ambayo yanaendesha kompyuta, yaani pogramu zake. Programu hizi kiasili ni mfululizo wa namba 0 na 1 kwa mpangilio tofautitofauti.
Siku hizi zinapatikana (bado kimsingi 0 na 1) kama data dijitali ndani ya "hardware". Kiswahili chake si "bidhaa laini" bali "programu"

Kwa hiyo ukitafuta neno la Kiswahili kwa softcopy taja yale jinsi yalivyo: Nakala dijitali.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom