Socialphobia, anxiety, depression, panic attack inaniua taratibu! Msaada

Akilinjema,

Kwa njia yoyote isiyo na maumivu,

Hayo mateso ntayokutananayo huko ni bora zaidi kuliko ya hapa duniani. Kama kweli Mungu aliamua niishi maisha haya japo sikutaka niishi hivyo basi atakuwa kanikosea hata nikiwahi kwenda kwake la kujibu ninalo, nimehangaika kadri ya uwezo wangu nimeshindwa kibinadamu.

Siku zote hizo why asitoe suluhisho mapema ili nisiwahi kwenda kwake? Hajui kwamba kupona kwangu ni mafanikio ya watu wengine? Kiukweli najuta kuishi na familia ambayo haikua na mapenzi ya dhati kwangu yale ya kunijenga. I have to go, potelea mbali.
 
Maiti,

Hapana usiende ndugu!

Kumbuka aliyofanyiwa Yusuf na nduguze,
Kwanza walitaka kumuua kabisa baadae wakaamua kumuuza kwenda utumwani!

Yusuf alistahamili yote, kufika kule akapewa Kwesi ya kubaka mke wa bosi kwa kusingiziwa, akatupwa gerezani,

Angalia mtirirko wa hiyo mitihani, lakini hakuwaza kujiangamiza moyoni mwake, alimwamini Mungu,
Baadae Mungu alikuja kumuinua akawa Waziri mkuu, kukatokea baa la njaa wale nduguze walotaka kumuua na kumuuza walienda kwake Yusuf, akawapokea bila kisasi, akawalisha!

Hata wewe ukipata mafundisho sahihi ya Neno la Mungu hakika utavuka hapo,

Mungu atakuinua hao wanokuona huna maana watakuja na wajukuu zao kuomba msaada kwako!
 
sifanyi nyeto mkuu. Ni kweli oversensitive person ambae ni introvert.
Embu Google ujue kama nijue kama wewe ni empathic person?

Je unapenda mwili wako? Kabla ya kukushauri nijue hayo kwanza
 
kwa njia yoyote isiyo na maumivu,

hayo mateso ntayokutananayo huko ni bora zaidi kuliko ya hapa duniani. Kama kweli Mungu aliamua niishi maisha haya japo sikutaka niishi hivyo basi atakua kanikosea hata nikiwahi kwenda kwake lakujibu ninalo, nimehangaika kadri ya uwezo wangu nimeshindwa kibinaadam, siku zote hizo why asitoe suluhisho mapema ili nisiwahi kwenda kwake? Hajui kwamba kupona kwangu ni mafanikio ya watu wengine? Kiukweli najuta kuishi na familia ambayo haikua na mapenzi ya dhati kwangu yale ya kunijenga. I have to go, potelea mbali.
Jamani,usikate tamaa mapema..
Mshukuru Mungu kwa kila jambo japo ni ngumu
 
asante ndugu yangu.
Jitahidi sana ukiwa peke yako uwe unaongea mwenyewe.

Kuna mambo huwa unatamani watu wayajue na uwafahamishe sasa hayo mambo jitahidi ukiwa peke yako yazungumze kana kwamba unajifanya uko na watu unawaelekeza.

Watu mfano wako wanakuwa na mambo mengi wanayajua lakini wanakosa watu wa kuwaambia.hivyo kunakuwa na mrundikano wa mawazo kichwani mwako.

Lakini pia usiidanganye akili yako kwamba sababu ni wazazi hapana.

Wazazi walisha play part yao kukukuza vile ambavyo wao wanataka.

Sasa ni zamu yako kujikuza vile ambavyo unataka kwa sababu sasa ni umri wako wa kujilea mwenyewe.

KUWA VILE UNATAKA KUWA.
Una nguvu kubwa ya kuishi utakavyo,una nguvu kubwa ya kuamua wewe uwe nani,una nguvu kubwa ya kuamua kwamba uwe na furaha ama usiwe nayo.

Wazazi hawalaumiki kwa namna yeyote ile kutokana na hali yako uliyonayo.tuna akili,tuna uwezo wa kujiendesha kabisa.

Jaribu kujiuliza kwamba unadhani ni kitu gani hasa kikubwa ambacho kinakushinda wewe kujichanganya na watu na kuwa unapiga stori?

Ni kipi hasa unahisi hicho hata iwe vipi siwezi kukiepuka?
 
Embu Google ujue Kama nijue kama wewe Ni empathic person? Je unapenda mwili wako? Kabla ya kukushauri nijue hayo kwanza

Hapana sio empathic. Naupenda mwili wangu ila niko na low self esteem
 
asante kwa ushauri mkuu. Tatizo langu kwenye mazoezi ni mvivu naweza nkaanza wiki moja wiki inayofuata naacha. narudi tena pale pale.
Fanya michezo ili kuongeza hamasa ya mazoezi,kwa mfano mpira,kuogelea na muziki.
Udhulia midahalo na makongamano,warsha na mikusanyiko ya kiimani.
 
Nilishakia na tatizo.kama.lako kuna doctor (you tube channel anaitwa( dr. Daniel fox) ukitulia na kumfuatilia vizuri hilo tatizo linaisha ndani ya wiki na kwa muongozo wake haitokuja kukirudia tena.unaweza kutumia madawa lakini menhi yana (side effects) baadae utajikuta huwezi kuishi bila madawa
 
safuher,

Am sorry to say this, i hate my parents so much, unaposema waliplay part yao naona kama umependezwa na malezi yao hadi hii leo nakuja kuandika maombi ya msaada hapa JF. THEY FAILED TO RAISE ME. Wamefanya niishi maisha yakutokua mtu wa kujichanganya na watu, wamenipa adhabu ambazo sikustahili kwa wakati huo, nimekuwa so embarrased mbele ya marafiki zangu wa utotoni, wamenipa nidhamu ya uoga.

Niwapo kwenye maongezi na watu kila napotaka kuongea nashindwa maneno yanapotea kichwa kinabaki cheupe, naishiwa nguvu, natetemeka, anxiety inakuwa juu mapigo ya moyo yanakwenda kasi, pumzi navuta kwa shida its like kama zinapungua na nazihitaji, kizunguzungu kinanijia then naondoka mahali nlipo naenda sehemu safe yoyote niliyoizoea ambayo nitakuwa mwenyewe hapo ndo inakuwa pona yangu. Baada ya hapo naanza kujilaumu feelings za kulia zinanijia ila machozi hayatoki naumia ndani kwa ndani.
 
Maiti, Mkuu ninachokisema nakielewa vizuri sana.

Umri ambao wazazi wamekulea ni mchache sana ukilinganisha na umri ambao utakuja kuishi bila wazazi.
Hivyo wazazi umeishi nao kwa muda mchache tu. Muda mwingi utakuwa peke yako na utajilea mwenyewe.

"Njia bora ya kuondokana na uwoga ni kufanya kile unachokiogopa"

Usipeleke lawama kwa wazazi, utajikuta upo hapo hapo,azima ujue kwamba wazazi walikosea kukulea vile, na hapo sasa baada ya kusema walikosea sasa ujiulize je upo tayari kuishi kwa matokeo ya makosa yao? NO HAUPO TAYARI.

Sasa anza kuchukua hatua muda huu, huu ndio muda wako wa kuweka lawama pembeni na kuangalia namna gani utalitatua tatizo hilo pasi na kuwalaumu wazazi, kwani UKILAUMU SANA WENGINE INAKUFAYA UJIONE WEWE NI MSAFI SANA.

Njia ya kwanza ambayo itaweza kukutoa katika janga hili ni kwanzakuwapa wazazi UDHURU kwamba walikuwa na nia njema huenda walikosea katika matendo yao.sasa wahukumu kwa ile nia yao njema na sio yale matendo yao.
Kwani lau wangelikuwa hawana nia njema ingekuwa UMESHAKUFA ZAMANI WEWE.

Kwanini upo mpaka sasa hivi? Kwa sababu yao,hawakukutilia sumu wala kukupangia njama za kukuuwa bali walijitahidi kukufikisha hapo ulipo.

Tatizo ni wewe sio wazazi, wao wameshamaliza kazi yao na sasauko wewe ndo muamuzi nani uwe.

Unadhani ukiwa ndani ya shimo alafu ukawa unandelea kulichimba utafanikiwa? Hapana bai acha kuchima himo ukiwa shimoni.

Acha kuongeza lawama kwa wazazi wakati bado upo katika matatizo yako na unahitaji kuyatatua kwa namna yeyote ile.
 
hapana sio empathic. naupenda mwili wangu ila niko na low self esteem
Basi tatizo ni you are NOT fair to yourself, unajicompare sana na watu.

Mimi sometimes nakuwa na hisia km zako ila hazichukui zaidi ya saa 1 zinaisha,niamini mimi nakuelewa Sana yaani vyote unavyosema Mimi nishawahi kujifeel hivo nakuelewa moja kwa moja bila chenga.

Embu jaribu kukubali Kwanza upo hivo na unaweza kuwa bora zaidi ya hivo...jisemee vitu vizuri vizuri halafu usiwaze madhaifu yako kabisa.

Toka nje usikae ndani na ukiwa ndani angalia comedy movie tu.

Fanya vikazi vidogo vidogo.

Nenda beach mara nyingi uwezavyo.

Tafuta mwanamke sio kwa serious relationship bali kwa ngono tu.Hii ni tiba kabisa badala ya pombe tafuta mwanamke, wanawake Hawa ni Dawa tosha hasa wakikupa great sex.
 
Maiti, Mkuu kwanza inabidi ubadili mindset yako na kuona issue positive katika kila fikra negative iliyopo katika akili yako...

Malezi uliyopewa ni malezi ambayo wengi tumekua nayo.. Wazazi wetu kwa zamani walidhani ni njia ya kutunyoosha na kutulea kama vile walivyolelewa na wazee wao.. ilikuwa ni njia ya kukulinda japo walizidisha hadi kukutengenezea kitu kinachokusumbua hadi sasa

Kumbuka kitu kimoja... unapowaweka wazazi wako kama sababu ya wewe kuwa hivyo ni sawa na kuweka point ya kuilamu kwa kila kushindwa kwako.. Hii ndio inakuletea hali ya kuendeleza CHUKI kwako na kwa WAZAZI WAKO na kusahau sehemu muhimu zaidi "KUJIFUNZA KATIKA KILA UNAPOKWAMA".

CHUKI humla anaeibeba na wala haimuathiri sana yule anaechukiwa... HUO NDIO UKWELI... ondoa hiyo nguvu ya kumlaumu mzazi kwa maana HAIWEZI KUBADILI LOLOTE KWA SASA na ANZA KUJIFUNZA KWA KUKOSEA ILI UJIFUNZE KUWA KAMA WENGINE

Tatizo lingine unadhani kuwa watu hawana HOFU kama uliyonayo. HUU NI UONGO. Kila mtu ana hofu kwa kitu anachokifanya ila tu wale unaowaona wapo confident ni kwa sababu wamejifunza kuiendesha hofu yao kiasi cha kutoipa nafasi ya kuzuia baadhi ya shughuli zao. Hiki ndicho unachotakiwa kukifanya "JIFUNZE JINSI YA KUISHINDA HOFU YAKO"

Katika kujifunza kuna kushindwa mara nyingine. Haswa hapa naona ndipo panakuangusha maana unajihukumu kupita kiasi kwa kosa dogo. Guy nobody is perfect, wote tunakosea hivyo kuna haja gani ya kujihukumu kama mdhambi mkubwa duniani kwa kukosea.

Guy Learn to be perfect within your imperfections nd thats what i call EXCELLENCY because PERFECTION is a lie and it does not EXIST. Ukilijua hili, utaishi kwa amani kiasi fulani maana utakuwa fair kwa nafsi yako pale utapokosea.Dont be too hard on yourself
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom