Socialphobia, anxiety, depression, panic attack inaniua taratibu! Msaada

MAITI

Senior Member
May 14, 2018
154
299
Kama ni udongo Mungu kaumba basi mimi ni udongo wa mwisho kabisa tena mfinyanzi/ tifutifu.

Niombe radhi kwa aina ya uandishi mbovu, nitakayoandika hapa maana ni matokeo ya anxiety.

Mimi ni kijana mwenye umri 29, ambaye mpaka sasa siwezi kujieleza, sina confidence, sijui kipaji changu, sina marafiki, sihudhurii misiba, sherehe na shughuli zote zenye mikusanyiko ya watu (na ukinipigia simu kunialika nije basi nitatoa sababu ambazo hazina kichwa wala miguu ili mradi tu nisije ili niwe free), sina girlfriend/ mke, most of my time napenda kushinda mwenyewe, sina kazi, sina ajira rasmi.

Nilikuwa college nasoma degree ila anxiety ikanifanya nikatishe masomo yangu ili niwe free maana sikuweza kuhimili hofu ya kujumuika na wenzangu kwenye discussions/ presentation na mengine mengi yanayohusiana na kujieleza.

Nimesali sana ila sasa nimepoteza imani ya Mungu ninayemtumikia maana anaona ninayoyapitia ila anakausha so what next? It means nipo duniani kimakosa right? So sioni faida ya kuishi mpaka sasa.

Kuhusu familia naweza kusema kuwa 95% sikuwa treated right, my parents walikuwa overprotective sana sikupewa ule uhuru wa kujichanganya na wenzangu pale nilipohitaji na sikupewa ule uhuru wa kujieleza zaidi pale nilipohitaji kufanya hivo so hii iliaffect maisha yangu ya utoto kuanzia kushiriki michezo na wenzangu mitaani, darasani katika shule zote nilizopita na hadi chuo kikuu.

Hii imeathiri vipi kitaaluma? Mfano unaweza ukawa unajua kitu na wengine hawajui sasa unatamani uwajuze/ujibu ila sababu ya anxiety siwezi kufanya hivo tena so nakaa nalo moyoni hii yote sababu siko na nguvu ya kujieleza.

Niko na low self esteem/sijikubali kwa kweli na hii siyo kwa mapenzi yangu ila nahisi kuna baadhi ya stages nilipokuwa mtoto sikuzipitia vyema na hazikuwa fair kwangu na ndizo zimeleta haya nayopitia sasa.

Not talkative at all. Ni mwepesi kuchange mood haraka pale napokwazika, kinachonishangaza zaidi ni kwamba kila napokwazika au nikikumbana na situation yoyote ambayo inanilazimu nilie ili nisahau ila silii nakaa nalo moyoni na kila nikijaribu kujilazimisha kulia machozi hayatoki, ila tumboni na moyoni nasikia maumivu sana its like kama roho inalia sana ndani kwa ndani ila uso mkavu hauoneshi zaidi ya kubaki kutetemeka tu na kutokwa jasho + mapigo ya moyo kwenda kasi.

Hivi kuna binadamu anayeishi kama mimi kweli?

Mwisho niseme tu kwamba anxiety imeathiri my lifestyle/ sio mtu wa kucheka/kufurahi at all, sio mtu wa kula japo uwezo kupika/kununua chakula ninao kwa maana hiyo nimedhohofu sana kimwili. Anxiety imeathiri uwezo wangu wa kufikiri sababu sio mtu wa kujichanganya na watu so nashindwa kuwaza na kuongea vitu vya kujenga zaidi.

Anxiety imeathiri imani yangu kiroho si mkristu wala muislamu. Anxiety imenipotezea marafiki wengi wao wanahisi naringa ila ukweli ni kwamba siko hivyo, nawa/niliwahitaji sana kwenye mambo yangu ya mafanikio ila hofu imefanya kutojumuika nao.

Nimekata tamaa ya kuishi. Ni bora nilale usingizi wa milele ili niepuke tabu hizi ambazo Mungu wenu anaona ila ananikaushia tu. Wanasema 'Mungu hakupi mzigo usiouweza' pia wanasema 'What doesnt kill you make you stronger' ila kwa hii hapana kwa kweli.

Binafsi sinywi pombe, sivuti unga wala sigara sina tabia mbaya za kimakundi/wahuni kwa hilo nashukuru ila natamani nianze kunywa pombe ila naogopa sitaacha maana ndio itakuwa tabia yangu daima incase matatizo yangu nikayasahau kwa muda mfupi baada ya kulewa.

Niombe radhi kwa mwandiko wangu mbovu dunia nzima utadhani nimezaliwa Rwanda huko kumbe ni Mtanzania na mDar es salaam wa hapa hapa!

Yaani hapa nilivyoandika hivi najisikia amani sana its like kama kuna kamzigo nimekatua hivi mwilini mwangu.

Niwashukuru wale wote mlio/mnaoshirikiana nami kwenye maisha yangu ya kawaida/ mtaani, college na mitandaoni.

Anaejua sumu nzuri inayoua kwa haraka bila kutumia nguvu anijuze kupitia PM tafadhari maana nshajaribu 3 aina tofauti imeshindikana naishia kuharisha. Watu wengine tumekuja duniani kimakosa sana Itabidi turudi tulikotoka ili tuwaachie mliokuja duniani na furaha. Wale mlionishauri nitumie kamba nimeshasema narudia tena kamba unatumia nguvu nahitaji dawa isiyotumia nguvu lets say nife nikiwa usingizini or something like that.

Asanteni.

MICHANGO YA WADAU:
Mkuu Nina tatizo Kama lako,

Siwezi kukaa kwenye makundi ya watu wengi, muda mwingine unajilazimisha kupiga stori na watu unaona kama hawakusikilizi unaona isiwe tabu naondoka zangu ila nikifika kwangu nakua na amani zaidi, Basi hapo nitacheza games nitaangalia movie nitasikiliza album za Eminem karibu zote mara giza lishaingia, alafu usingizi hauji kwahiyo nitapitapita Jamii Forums mpaka saa 8 ndio najaribu kulala, halafu naamka mapema kama ni wikiendi ni mwendo wa muvi yaani bandika bandua.

Nina marafiki wachache sana Ila hata ukiwaambia watakuona wa ajabu unanyamaza kimya sababu hakuna atakaye kusikiliza akakuelewa, muda mwingine unajaribu kuwa normal Kama wale ili uendane na mazingira lakini wapi tabia yako itabaki palepale,

Nikajua peke yangu ndio naishi hivi kumbe tupo wengi, ila Mimi sitojaribu kujiua never
sababu naona kawaida japo watu wananiona Kama nalinga Mara huyu kaka mpole Sana, ila watu wakiniambia nalinga roho inaniuma sana sema nawapotezea tu , ila wakati mwingine Hali hii inachosha mpaka unajiuliza kwanini mimi.

Ushauri wangu
Kwakua hupendi kuishi hivyo huna budi kujitoa, ila Mimi imeshindikana nimeamua kujikubali nilivyo maisha yanaenda.
========
Maiti,

Fortunately, una tatizo ambalo linaweza tibia hospital
1) Psychotherapy
2) Anti-Depressants(anti-anxienty): Amitryptilline au Fluoxetine

The only place utapata msaada trust me ni hospital na kama upo Dar watafute ma psychologist na ma psychiatrist unaweza mpaka kuomba private sessions kama hauwezi kwenda hospitali

Kikubwa uwe na Good insight kukubali kuwa unaumwa na ugonjwa wako unawezwa ponywa na maelezo niliyoyatoa!
========
Nimewahi kupitia changamoto kama hiyo; suluhisho kama wewe ni mkristo tafuta kanisa lenye wokovu ambalo unaweza kusikilizi habari njema; sikilizi audio za watumishi na watu wanaotia moyo kwenye Youtube zipo nyingi sana, hakikisha muda wote unasikiliza habari njema tu, ukiona mtu anakuchanganya au anakusema vibaya mpuuze kabisa, hakikisha unavaa vizuri kama mtoto wa mfalme; vaa uvutie hasa, ukipata nafasi ya kwenda out nenda sehemu kama jangwani beach clubs
Unacheza mziki hata kama hunywi we jichanganye tu utazoea.

Hakikisha chumba chako ni kisafi na kuna muziki mzuri na kama unaweza kuwa na tv nzuri na vitu vingine vya ndani vizuri kuwa navyo automatic hapo utapata mwanamke anayefanana nawe; utaanza kupata mtu wa kumsikiliza then hakikisha unapata chalula kizuri unachopenda hapa nakushahuri wekeza kwenye ulaji wa matunda na asali pia; kwa hayo tu naamini wasiwasi utaisha kwa asilimia kubwa

=======
Mimi nikajua shida kuuubwa kumbe hako tu. Kifupi background yako haijaathiri chochote kwenye hiyo hali, hivyo usisingizie aina ya malezi uliyopata. Kama hakuna mtu mmoja wa kukusaidia, basi angalia yanayowezekana hapa.

- Jiunge na jeshi/mgambo, lengo ni mazoezi kuweka akili active maana wewe peke yako umeshindwa. Au vipi weka ratiba ya mazoezi asubuhi na jioni, au jiunge na kikundi cha mazoezi ya aerobics chochote.

- Tafuta mwanamke, bila shaka hata kutongoza huwezi ila jitoe tu ufahamu hata upate rafiki wa kike. Wanawake ni dawa nzuri ya akili ya mwanaume, Mungu aliliona hilo ndio maana akasema Adam asiishi peke yake ampatie msaidizi wa kufanana naye. Hata tusio na wanawake, ile kuongea tu au kuchat na good girl friends mkacheka huwa inaleta hali fulani nzuri kwenye mind.

- Usiisahau nafasi ya Bwana Mungu wako.

- Kula vizuri, kula mlo kamili. Ingia hata google tafuta vyakula vyenye Vitamin B6 nyingi na Magnesium nyingi, uhakikishe havikosekani mezani.

- Tafuta hobby yako ni nini, jaribu kuangalia mpira hata vibanda umiza, jaribu movies, jaribu music, kote huko uone kipi kitakutuliza akili.

NB: Kuwa mwanaume bob, jikubali. Jione hakuna mwingine kama wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
========
Maiti,
Kwa maono tatizo lako nahisi ni sababu ya malezi mabovu ya wazazi.

Mara nyingi wazazi ambao unakuta ni too protective huishia kuwaharibu watoto wao kisaikolojia. Unakuta mzazi anazuia mtoto asicheze na watoto wenzie kwa kuhisi watamuharibu bila kujua anapocheza nao anajifunza mengi sana na anapata amani moyoni.

Kuna wazazi wengine kwao kila kitu wanajua hawawapi nafasi hata watoto wao waonyeshe wanachojua, badala yake kama ni daktari atalazimisha kwa vyovyote vile mwanae awe daktari wakati sio, madhara yake mtoto anapoteza nguvu ya kujiaminj na kuwa na tendency ya kuogopa kudhubutu.

Ili kuondokana na tatizo lako ni wewe mwenyewe kujikubali na kutamani kubadilika. Itakuwa ngumu ila jaribu kuacha kujifungia ndani. Penda tembea tembea kama unaweza pata hela ya kutumia penda basi kutoka toka. Ukiwa na pesa basi kwenda bar au beach mara moja moja sio mbaya.

Sio lazima uwe na mtu unaenda zako bar unaagiza hata kiwine unavuta masaa. Kadri siku zitavyozidi akili yako itajityune utapata watu wakuongea nao.

Penda kufanya mazoezi sana. Sio lazima kwenda gym. Na mazoezi mazuri kwangu ni kupenda kukimbia. Kama unaona aibu anza kwa kuruka kamba hata chumbani.

Nina wasiwasi unawachukia sana wazazi wako. Basi fanya hivi kama uko karibu nao, jaribu tafuta sehemu ya mbali uishi ili uweze wasahau.

Mwisho sio wewe peke yako katika dunia hii. Tuko wengi tu ambao tumepitia katika hali hiyo na wazazi wa namna hiyo. Ubaya sasa unakuta hata pale unapotaka kujitegemea bado atataka akuendeshe vile vile.

Mara nyingi mtu wa namna hiyo unajikuta unashindwa jiamini kwa lolote, inafikia hatua unaona huwezi fanya lolote mpaka mzazi asaidie.
 
Pole sana kijana. Kwanza badilisha hilo jina unalotumia humu, unamkufuru hata Mwenyezi Mungu.

Uzuri ni kwamba wewe tayari tatizo lako unalifahamu vizuri sana, na umeweza kulieleza kwa ufasaha kabisa kiasi cha ku pin point kwamba kiini ni nini.

Unahitaji kuchukua hatua moja tuu ya ziada ambayo itakua a turning point kwa maisha yako. SEEK HELP!! Tafuta msaada kuhusiana na hiyo hali yako kwa wataalamu au mtu mzima unaemuamini na kuona kwamba anaweza kuwa msaada kwako.

Nenda hata hosiptali, ingia chumba cha daktari mwambie wewe huna tatizo physically, ila tu unahitaji mtu ambae anaweza kukusikiliza.

Unahitaji tu kuongea na mtu na yeye anachotakiwa kufanya ni kukusikiliza tuu, na kukufanya uongee zaidi, Basi!

Uko mkoa gani kijana? I can conect you with someone who might help you out. Natamani ningekuwepo mkoa uliopo, ningekusaidia mimi mwenyewe bila kuhitaji chochote kile kutoka kwako.

Pia kijana, unatakiwa kujikumbusha kwamba wewe mwenyewe nie mwamuzi wa kile ambacho kitatokea katika maisha yako; na sio mtu au kitu kingine chochote. At this point in your life, kitu kitakachotokea baada ya hapa, kitaamuliwa na WEWE MWENYEWE.

Je, unaweza kuongea vizuri lugha ya kingereza? Na ni mpenzi wa kusoma vitabu? Kama jibu ni ndiyo, kuna kitabu nataka nikupatie ambacho nadhani kinaweza kukusaidia.
Maiti
 
Asante mkuu wangu Dr. Wansegamila kwa kunipa moyo, unaweza kunipa link ya hiko kitabu nikisome ila nisikudanganye tu, hiko kitabu sina uhakika kama kitabadili chochote kwenye maisha yangu maana nimesoma vingi na nimetoka kapa.

Its like kama akili yangu ishakubali kilichotokea na haiko tayari kubadilika. naweza nikafanya changes leo ila kesho nikarudi vile vile nilivyokuwa mwanzo. Alafu hospitali nyingi wako after money so nimekata tamaa kwa hilo pia.
 
asante mkuu wangu kwa kunipa moyo, unaweza kunipa link ya hiko kitabu nikisome ila nisikudanganye tu, hiko kitabu sina uhakika kama kitabadili chochote kwenye maisha yangu maana nimesoma vingi na nimetoka kapa. Its like kama akili yangu ishakubali kilichotokea na haiko tayari kubadilika. naweza nikafanya changes leo ila kesho nikarudi vile vile nilivyokuwa mwanzo. Alafu hospitali nyingi wako after money so nimekata tamaa kwa hilo pia.
Nime attach hicho kitabu hapa; kinaitwa "The Secret"; Kinajaribu kueleza kwamba chochote ambacho kinakutokea kwenye maisha yako, YOU are the one who attracted it to your life. CHOCHOTE KILE. Ni kitabu kizuri.

Pia, kama unafikiri kuwa hospitali ziko after money, well and good. Just find ANYONE to talk to. Unahitaji hicho kwa sasa kuliko kitu kingine chochote kile. Tafuta mtu uongee nae, ufunguke kuhusu kila kitu unavyojisikia, your disappointment, your failures, kila kitu. Itakusaidia sana. Maiti
 
Attachments

  • The Secret by Rhonda Byrne.pdf
    4.1 MB · Views: 146
Nime attach hicho kitabu hapa; kinaitwa "The Secret"; Kinajaribu kueleza kwamba chochote ambacho kinakutokea kwenye maisha yako, YOU are the one who attracted it to your life. CHOCHOTE KILE. Ni kitabu kizuri.
Pia, kama unafikiri kuwa hospitali ziko after money, well and good. Just find ANYONE to talk to. Unahitaji hicho kwa sasa kuliko kitu kingine chochote kile. Tafuta mtu uongee nae, ufunguke kuhusu kila kitu unavyojisikia, your disappointment, your failures, kila kitu. Itakusaidia sana. Maiti

asante sana mkuu ntajitahidi nifanye hivo
 
Samahani Maiti Naomba unijibu maswali yangu kidogo..umezaliwa tarehe ngapi na mwezi gani, maana kuna watu wanaathirika na depression kutokana na miezi waliozaliwa wanasema kipindi cha mwezi ukiwa full moon
Mkuu hilo ni jina la kimtandao tu, haliwezi kubadili chochote juu yangu so usitishike kaka. Feel free ongea chochote ntakusikia na ntajaribu kufanyia kazi hata kama kitaniumiza sitajali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Samahan maiti..Naomba unijibu maswali yangu kidogo..umezaliwa tarehe ngapi Na mwezi gani, maana kuna watu wanaathirika Na depression kutokana Na miezi waliozaliwa wanasema kipindi cha mwezi ukiwa full moon

Sent using Jamii Forums mobile app

Hello Mkuu Tuchki kwa sababu za kiprivacy sitoweza kuweka tarehe yangu hapa in public labda in private. ila nyota yangu ni kaa
 
Hatua nzuri uliyonayo ni kwamba umeshagundua Tatizo basi unayo nafasi nzuri ya kutatua

Njia za kutatua hilo tatizo ndio utata unapokuja. Inshort sijui ni mtu gani sahihi wa kumueleza matatizo yangu akanielewa na kutunza privacy yangu maana wengi wao siwaamini. Najihisi ni mtu wa ajabu kuwahi kutokea duniani.
 
Nime attach hicho kitabu hapa; kinaitwa "The Secret"; Kinajaribu kueleza kwamba chochote ambacho kinakutokea kwenye maisha yako, YOU are the one who attracted it to your life. CHOCHOTE KILE. Ni kitabu kizuri.
Pia, kama unafikiri kuwa hospitali ziko after money, well and good. Just find ANYONE to talk to. Unahitaji hicho kwa sasa kuliko kitu kingine chochote kile. Tafuta mtu uongee nae, ufunguke kuhusu kila kitu unavyojisikia, your disappointment, your failures, kila kitu. Itakusaidia sana. Maiti

What if watu wanaomzunguka sio wasiri? Yaani akiwaelezea matatizo yake wanaweza kuyatangaza kwa wengine.. Una ushauri gani juu ya hilo?
 
What if watu wanaomzunguka sio wasiri? Yaani akiwaelezea matatizo yake wanaweza kuyatangaza kwa wengine.. Una ushauri gani juu ya hilo?

Asante mkuu. Hiyo ni moja ya sababu kubwa inayonifanya nikae kimya. Na nivyokuwa mkimya zaidi ndipo nazidi kuathirika anxiety inakuwa kubwa zaidi naishia kujifungia nyumbani.
 
Sioni tatizo kubwa kama unavyolielezea mkuu. Binadamu katika ulimwengu wa Nafsi yaani (Utashi hisia na akili) tupo wa aina mbili yaani 1. Extrovert ambao ni wanadamu wengi sana waongeaji wachangamfu 2. Wakimya yaani Introvert kundi ambalo hupo wewe.

Kuwa Introvert kuna changamoto ambazo wewe umetafsiri vibaya tu. Nitafute inbox

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Njia za kutatua hilo tatizo ndo utata unapokuja. Inshort sijui ni mtu gani sahihi wa kumueleza matatizo yangu akanielewa na kutunza privacy yangu maana wengi wao siwaamini. Najihisi ni mtu wa ajabu kuwahi kutokea duniani.

Pole sana kwa mitihani inayokuandama, ila futa hio dhana kichwani mwako kwamba wewe ni binadamu wa ajabu, wewe sio wa ajabu wala hujaonewa, I know it hurts ila you have to be Strong, matatizo tumeumbiwa wanadamu. Kila mmoja ana majanga yake tukianza kuelezea matatizo yetu kila mmoja yanamshinda mwenzie, kuwa na Subira na umlilie Mungu wako akuondolee mitihani inayokukabili.
 
Maiti,
Kwa maono tatizo lako nahisi ni sababu ya malezi mabovu ya wazazi.

Mara nyingi wazazi ambao unakuta ni too protective huishia kuwaharibu watoto wao kisaikolojia. Unakuta mzazi anazuia mtoto asicheze na watoto wenzie kwa kuhisi watamuharibu bila kujua anapocheza nao anajifunza mengi sana na anapata amani moyoni.

Kuna wazazi wengine kwao kila kitu wanajua hawawapi nafasi hata watoto wao waonyeshe wanachojua, badala yake kama ni daktari atalazimisha kwa vyovyote vile mwanae awe daktari wakati sio, madhara yake mtoto anapoteza nguvu ya kujiaminj na kuwa na tendency ya kuogopa kudhubutu.

Ili kuondokana na tatizo lako ni wewe mwenyewe kujikubali na kutamani kubadilika. Itakuwa ngumu ila jaribu kuacha kujifungia ndani. Penda tembea tembea kama unaweza pata hela ya kutumia penda basi kutoka toka. Ukiwa na pesa basi kwenda bar au beach mara moja moja sio mbaya.

Sio lazima uwe na mtu unaenda zako bar unaagiza hata kiwine unavuta masaa. Kadri siku zitavyozidi akili yako itajityune utapata watu wakuongea nao.

Penda kufanya mazoezi sana. Sio lazima kwenda gym. Na mazoezi mazuri kwangu ni kupenda kukimbia. Kama unaona aibu anza kwa kuruka kamba hata chumbani.

Nina wasiwasi unawachukia sana wazazi wako. Basi fanya hivi kama uko karibu nao, jaribu tafuta sehemu ya mbali uishi ili uweze wasahau.

Mwisho sio wewe peke yako katika dunia hii. Tuko wengi tu ambao tumepitia katika hali hiyo na wazazi wa namna hiyo. Ubaya sasa unakuta hata pale unapotaka kujitegemea bado atataka akuendeshe vile vile.

Mara nyingi mtu wa namna hiyo unajikuta unashindwa jiamini kwa lolote, inafikia hatua unaona huwezi fanya lolote mpaka mzazi asaidie.
 
Similar Discussions

20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom