"Social Economic Empowerment Program" Madrassa Yabuni Mpango wa Kijamii wa Kuwezeshanana kiuchumi

Abdul Ghafur

JF-Expert Member
Sep 18, 2017
610
733
"Social Economic Empowerment Program,." Mpango wa Kijamii wa Kuwezeshana Kiuchumi, Kwa mara ya Kwanza Tanzania. Haujawahi kutokea, duniani.

Ni mpango uliobuniwa na Madrassatul Abraar, iliopo mtaa wa Vitendo, Misugusugu, Kibaha, Pwani Tanzania.

Mpango ulianzishwa nakuasisiwa na Abdul ghafur kwa kujiwezesha kifamilia na marafiki wa karibu kutatua tatizo la kujipatia nyumba za kuishi kwa gharama nafuu.

Kwa kuwa mpango huo umekuwa ni mwema sana, na wenye mafanikio, tukaona kwanini tusiufikishe kwa jamii, tufaidike sote.

Mpango umeleta mafanikio mazuri kuanzia mwanzoni, nyota njema huonekana alfajiri, na umezaa mipango mingine midogo midogo ya kuwezeshana kijamii.

Kwa Sasa mipango tuliyonayo nafanya vyema sana ni kama ifatavyo:

1) Abraar Bricks Nyumba kwa wote
Mpango huu upo, unaendelea vizuri, unaendeshwa na Madrassatul Abraar chini ya usimamizi wa muasisi, Abdul Ghafur. Nadiriki kusema hili ni wazo la kipekee Tanzania, pengine na duniani. Binafsi sijawahi kuliona wala kusikia wapi limefanyika kama hili. Kama kuna walioliona na au lipo basi wanirekebishe na wanielimishe zaidi.

Kwa Sasa mipangotuliyonayo na inafanya vyema sana ni Abraar Bricks Nyumba kwa wote. Hii ipo na inasimamiwa na kuendeshwa na Madrassatul Abraar chini yangu.

Hili ni wazo la kipekee Tanzania, pengine na duniani. Sijawahi kuona wapi limefanyika kama hili.

Madrasaatul Abraar katika mpango huu, inakuwezesha wewe kujenga kwa kuanzia kwa Shillingi 2,500 tu.

Unaanza kwa kudunduliza kwetu kidogo kidogo, kwa maana ukijiunga tayari inakuwa umenunua kifaa cha ujenzi kimoja, nalo ni jiwe lako la msingi la ujenzi wa kisasa, ujenzi wa gharama nafuu na wenye ubora wa hali ya juu

2) Mafunzo ya kuunda vifaa vya ujenzi na ujenzi wa kisasa
Mpango huu unawezesha vijana na kina mama kujifunza kazi za ujenzi kuanzia kuunda vifaa vya ujenzi mpaka kujengea. Mafunzo yanatolewa bure na chakula posho ya chakula inatolewa kwa wanafunzi wote wanaojiunga na mpango huu.

Kwa wale ambao tayari mafundi ujenzi, tunawapa ujuzi wa ziada na tunawafundisha kutumia bidhaa mpya za ujenzi, tunawafundisha nidhamu za kazi za ujenzi. Kiufupi, tunawanyanyua kutoka mafundi wa kawaida na kuwa mafundi bora. Bure na posho ya kujikimu kwa siku, kwa siku watazokuwa wanapata mafunzo.

Mafunzo yetu ni ya muda mfupi sana na yenye matokeo chanya na mema sana kwa yeyote mwenye nia ya kujifunza ujenzi au kuongeza ujuzi wa ujenzi3.

Viwanja vya gharama nafuu kwa malipo yasiokuwa na riba.

Kwa mara ya kwanza sasa tunawezesha jamii kujipatia viwanja vya gharama nafuu kwa malipo nafuu yasiokuwa na riba.


Kama u muandishi wa habari au umeguswa japo kidogo na hayo ya juu, unaweza kutupigia simu 0625249605 Abdul Ghafur, kwa maelezo na ufafanuzi wa ziada.
 
Pelekeni watoto shule wakasome waelimike.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Madrassa ni kiarabu, kiswahili ni SHULE. Huko vijana hufundishwa elimu ya kuishi hapa duniani, jinsi gani ya kujitunza//kuwatunza Wazazi, mke na watoto/kuishi na jirani/kujali wanyama na viumbe vingine/kufanya biashara/kujitibu na mambo kibao ya Duniani. Kuelimika sio kuwa na kazi nzuri ofisini, ni kujua kuishi km Binadam.
 
Vitendo Saccos iliishia wapi?
Vitendo Saccos haijafanikiwa kabisa kuendelea kwa kukosa uongozi na zaidi ni kwa kanuni na sheria za ushirika ambazo zinalazimisha kuwe na riba kwenye saccos. Sisi tukashindwa kutilia mkazo kwa hilo kwani vitabu vya dini zetu vinatukataza kula riba.

Pia . Ilikuwa ni one man show na jambo kubwa na zito kama hilo lilikuwa linahitaji watu wazoefu wenye mawazo chanya wa kuliendesha. Ni wazo jema sana
 
Mkuu Madrassa ni kiarabu, kiswahili ni SHULE. Huko vijana hufundishwa elimu ya kuishi hapa duniani, jinsi gani ya kujitunza//kuwatunza Wazazi, mke na watoto/kuishi na jirani/kujali wanyama na viumbe vingine/kufanya biashara/kujitibu na mambo kibao ya Duniani. Kuelimika sio kuwa na kazi nzuri ofisini, ni kujua kuishi km Binadam.
Shule ni Kijerumani.

Kiswahili ni Madrassa.

Hakuna elimu bora ya kuishi duniani kama iliyomo kwenye Qur'an ambayo hufundishwa madrassa.

Umewahi kuisoma Qur'an?
 
Na ile shule imefikia wapi kwa sasa ili tuje kwenye ujenzi wa nyumba zetu
Shule ipi unaiongelea?

Kuna Abraar Nursery School ambayo ujenzi umenza tayari. Kuna shule ya sekondari ya Vitendo, ambayo ni shule ya Serikali lakini Abraar tumejitolea kuwajengea darasa moja kwa vifaa vya ujenzi vya kisasa na pia kuna Shule ya Abraar Mkuranga ambayo ipo kwenye upimaji.

Unaongelea ipi kati ya hizo?
 
Back
Top Bottom