So sad: Kanitosa baada ya kujua kuwa naishi kwa dada yangu

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
17,895
25,944
Amani iwe nanyi wapendwa,

Inaniuma sana, nilikuwa na msichana mmoja mkali baraa yaani mzuri sana (kisu) hatari lakini kwa sasa siko naye tena.

Mimi naishi nyumbani lakini yule msichana nilimwambia kuwa hapa ninapoishi nimepanga na chumba nalipia laki moja kwa mwezi, shida ilikuwa inakuja pale alipokuwa ananiambia aje gheto apaone, hapo ndo shida ilipokuwa maana nilikuwa namkatalia. Nilikuwa namwambia mama mwenye nyumba hataki nipeleke msichana kwenye nyumba yake na ni mkali sana nikipeleka msichana anaweza vunja mkataba na mimi.

Hata siku nilipokuwa nataka kumpiga mikasa nilikuwa nampeleka gest maana kama unavyojua huwezi peleka msichana kwenye nyumba ya dada yako hata kidogo.

Sasa ile juzi sijui nani kamtonya kuwa mimi naishi kwa dada kafula ile mbaya kanipigia simu anaomba tuachane, ile kumuuliza sababu ndo akasema kuwa sababu ni kwa kuwa mimi ni muongo sana nilimuambiwa nimepanga kumbe naishi kwa dada.

HIVI HUYU MSICHANA ALIKUWA ANANIPENDA KWELI? MBONA KANITOSA KISA TU NAISHI NYUMBANI?

LONDON BOY
 
Alikuwa anakupenda kweli, ila ulimbukeni wako wewe ndo umefanya akuache, kwann umdanganye ulidhani ipo siku hatojua, na kama haufurahishwi na maisha ya kuishi kwa sista si fanya juhudi upange, hata ukianza na chumba cha 50/mwezi si mbaya..
Vijana muache maisha ya kuigiza, ni ujinga tu, fanya kazi, kaa chini panga mambo yako, fikiria kesho yako, huyo ex utaanza kuona anatoka na jamaa mwingine umjuaye kwakuwa ye ana malengo.
 
Kweli jamaa muongo mpaka "r" na "l" unachanganya... Jitahidi kuwa mkweli kwenye mambo ya msingi halafu tafuta uongo mtamu ambao hata ajiugundua unakuwa hauna madhara
 
Beira Boy, kumbe ndio maana ulikuwa unajiita baby. OK imetokea, pambana sasa upate kwako, pia tafuta mwanamke wa kujusaidia kwenye mapungufu yako. Msaada wa mawazo ni mkubwa sana kuliko msaada wa kifedha
 
Unamnyima shemeji yako nafasi ya kumpiga katerero sister maana kelele zake sio za nchi hii utasikia tu!Hama
 
Tatizo liko kwako uliona ugumu gani kumweleza ukweli kuwa hujapanga? Mpenzi wako ana haki ya kukuacha kwa kuwa wewe ni muongo.
 
Baada ya kuona tu
N I'd yako hata cjasoma
Maana alichoandika
N utumbo wa Kila sku
 
we kijamaa skuelewi elewi....
leo maisha yako ni h!!! kesho maisha yako ni hvi!!! kesho kutwa unakuwa hiviii!!! yani uwongo uwongo ndo dhambi yako kubwa.
 
Back
Top Bottom