Snura anusurika kichapo kwa kugoma kuimba wimbo wa CHURA jukwaani

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
SNURA341.jpg


STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Chura’ juzikati akiwa kwenye shoo iliyofanyika Masasi, Mtwara alijikuta katika wakati mgumu baada ya kunusurika kupigwa na mashabiki wake kisa kikiwa ni kutokuimba Wimbo wa Chura ambao umefungiwa.

Tukio hilo lilijiri mida ya usiku katika ukumbi mmoja maarufu uliopo Masasi ambapo Snura alikuwa akifanya shoo hapo na alipotaka kumaliza, mashabiki walimtaka amalize na Wimbo wa Chura ndipo kizaazaa kilipoanzia na kutaka kumpiga.

Akizungumzia tukio hilo Meneja wa Snura Hemed Kavu, amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema sio mara moja kwani imekuwa ikitokea mara kwa mara kwa Snura kukumbwa na kadhia hizo toka kwa mashabiki wake ambao wamekuwa wanataka awaimbie wimbo wa CHURA uliofungiwa na BASATA.

“Siyo tukio moja tu, tulishaenda shoo zaidi ya mbili tunakutana na dhahama hizi. Tatizo lililopo, Snura hawezi kupafomu wimbo ule kwa kuwa ulizuiliwa kutokana na video yake. Ni muda umepita video mpya imetengenezwa na kupelekwa bodi ya filamu kukaguliwa lakini hawajatoa jibu lolote zaidi ya kuzungushwa tu, mara TCRA mara Basata,” alisema Meneja wa Snura.

Ilibidi itumike nguvu ya ziada ya mabaunsa kuingilia kati na kuzima umeme kwa nguvu ili kuwatuliza mashabiki hao ambao baadhi walikuwa washaanza kurusha chupa za bia jukwaani.

Umeme ulipozima Snura aliondolewa kwa nguvu kimya kimya jukwaani na shoo kuahirishwa kwa lazima.

Source: Bongo Movie
 
teh teh teh
ulikuwa hujui huyu ni chura kweli kweli.

Sio kwenye muziki tu, mpaka kimatendo ni chura kweli

Ha ha ha ha ha ha !!!Jamani mtampa pressure bure binti wa kizaramo. Anajihesabu kama celebrity. Tena beautiful celebrity. Acheni hizo jamani.
 
Ha ha ha ha ha ha !!!Jamani mtampa pressure bure binti wa kizaramo. Anajihesabu kama celebrity. Tena beautiful celebrity. Acheni hizo jamani.
ha ha ha
mkuu yule ni mchaga mkuu.

Ni miongoni mwa wachaga wachache waliojaaliwa hizo mambo.

Nasikia wachaga wenzake wanamkana, eti hawataki kumsikia kisa "anawadhalilisha"
 
Mchaga huyo sio mzaramo ila mambo yake huwezi mzania kabisa kama ni mchaga
 
Watu wa Masasi na Nachingwea wanapenda Sana Kula vyura, isije wakamfanya kitoweo bora arudi huko.
 
Back
Top Bottom