Snoop Dogg na Mike Tyson waingia ubia kuwekeza kwenye kilimo cha bangi

KWEZISHO

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
7,519
6,511
Mwanandondi msataafu ameripotiwa kufanya kazi na mwanamuziki Snoop Doggy huku akijifinza kuhusu bangi.

Mwanandondi huyo mambaye kwa sasa amefungua shamba la ukubwa wa ekari 40, kwa ajili ya kilimo cha bangi, amejiweka karibu na mwanamuziki Snoop ambaye nae tayari anafanya shughuli za uzalishaji wa bangi, ili kujifunza namna sahihi ya kuendesha kilimo hicho na kupewa ushauri wa aina sahihi ya bangi anayotakiwa kulima.

Chanzo kimoja kimeeleza kuwa Snoop amemtafuta Tyson na kumpa maelekezo ya aina ipi ya bangi anayopaswa kulima.

“Alikuwa amewekeza kiasi cha dola za marekani milioni 25 kwenye bangi hata kabla ya jimbo la Carlifonia halijaruhusu matumizi yake, kwa hiyo anajua kwa undani uzalishaji wake.”

Snoop ambaye anataka kufungua maduka ya bangi aliwahi kulieleza gazeti la “Daily Star” la nchini Marekani kuwa, anaamini kuwa uwekezaji kwenye bangi unaweza kumaliza migogoro yote duniani.

Alisema “Ninahisi kwamba watu wengi wanavyozidi kuitumia ndivyo amani inavyozidi kuongezeka”

Habari zimeeleza kuwa Snoop ameungana na mghahawa wa “Jack in the Box” kuwapa wateja wake ‘ofa’ ya bangi.

Chanzo: Fahari News
 
Back
Top Bottom