Ndivyo Ilivyo
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 243
- 4
Usione taabu kurudi katika mijadala ya nyuma. Ndio pale tulipokwambia kuwa Zanzibar ni Nchi, na Tanzania ni Nchi. Hivyo Jamhuri ya Muungano ina nchi mbili. Kuna Watanzania wanye haki ya kumiliki ardhi ya Tanzania (Wakiwemo Wazanzibari) na Wazanzibari wanye haki ya kumiliki ardhi ya Zanzibar (iliyomo ndani ya Tanzania). Utekelezaji wa mambo unaweza ukawa na vijikasoro vya kiutendaji (na ndiyo maana tuna kero za Muungano). Lakini sheria ya Mzanzibari imezingatia sana haja ya Muungano wetu na imetoa provision kuruhusu Mtanzania asiye Mzanzibari kujumuika na wenziwe wa Zanzibar na kuwa Mtanzania -Mzanzibar.Wapo wasukuma na Wanyamwezi kule Dole waliokaa zaidi ya miaka mitano ( na hivyo kuwa Wazanzibari) mbona wanamiliki mashamba ya migomba na matuta ya viazi bila bughudha.Tatizo dilo hilo. Kwa nini ardhi ya Sengerema iwe ruksa kwa mpemba lakini ya Dole iwe marufuku kwa msukuma? hata hicho kipengele cha kukaa mfululizo kina matatizo. Huyo Msukuma akiomba uzanzibari baada ya miaka mitano si atakumbushwa pale alivyoenda kuhani msiba Sengerema akakaa zaidi ya mwezi mmoja! Na kwa hiyo miaka mitano anapofukuzia huo uzanzibari awe analipa hizo dola 5000 kwa kila kihekta kimoja!
Kuujua huu mfumo wetu wa Muungano haumaanishi kuwa kila kitu kifanywacho chini yake ni cha haki.
Amandla......