SMZ yazidi kuubomoa Muungano yataka bara walipe kodi ya ardhi

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza mkakati mpya wa kuwataka wawekezaji na watu wenye asili ya Tanzania Bara kusajiliwa na kuanza kulipa kodi ya ardhi ya dola za Marekani 5000 (Sh6.5 milioni), kila mwaka kwa kila hekta moja ya ardhi.

Hata hivyo, SMZ ilisema mwekezaji mwenye asili ya Zanzibar atapaswa kulipa dola 500 (Sh650,000).

...te-he!

ndipo mtapotambua Zanzibar ni Nchi au Mkoa! ...tena hapo kwenye 'mwenye asili ya Zanzibar kulipa dola 500 (sh650,000)' ...mwandishi angeongeza Tu!

Zanzibar ni njema, atakaye na aje!
 
i say hiyo achana nayo wao wakitaka kura watatupa kadi ya raia hapo kwa wapemba kula jiwe tu subiri uchaguzi unakuja hakuna kula chi chi mm tuone jeuri
 
kulipa kodi its okay......najaribu kuangalia/ kufikiria US$ 5000 kwa mwaka!!....virtually only Chenge et al will own/lease/rent land in visiwani
 
Habari ndio hiyo, nashangaa huyo mwandishi wa habari alivyoipamba hii habari kwa kichwa cha kibaguzi na ni kama ni kitu kipya sana! Na humu wengi wameingia mkenge na kuanza kutoa maneno ya chuki!

Lakini Tz kuna tatizo la wananchi wake kulipa kodi... zile dezo za miaka ile zimelipeleka Taifa katika hali mbaya!

Tatizo si kodi bali ni hizo tofauti ya viwango. Zanzibar wametumia haki yao kueleza wazi kuwa mtanzania bara akiwa kwao ni sawa na mfilipino. Hii ni haki yao lakini wahenga walisema kuwa ukila na kipofu.......!
 
Tukimaliza Wahindi na Muiran, Zanzibar you are NEXT.
Niite Mbaguzi, poa tu. Ila watu kama mimi ni muhimu kwa kila nchi.
Sisi ndiyo tunaitwa WAFANYA KAZI CHAFU.
 
Hebu tulia kwanza. Haya maneno ya Nyerere hapa hayafanyi kazi maana siyo sisi tueanza kuuvunja Muungano na kutenga watu. Tumelilia sana turekebishe mambo na tubaki pamoja. Tumeitwa majina ya ajabu sana, tumenyanyaswa na sasa tunaanza kutengwa waziwazi.

Nyerere huko juu, nafikiri utakuwa na sisi wakati tukiruhusu Wazenji KULA NYAMA YA MTU. Wao ndiyo wataendelea kulana. Kwani sisi kuna kabila linataka kujitenga Tanganyika? Au kuna mtu kasema kabila fulani inabidi litengwe? So longer Wanyamwezi/Wasukuma bado hawana noma, Tanganyika itasimama pamoja.
 
Urgently Inabidi ku-revisit mambo muhimu ya Muungano.......ili uendelee......ama sivyo.....what a time BOMB............tik tak tik tak!!!!
 
Muungano unatia kichefuchefu.....kwa nini Kila nchi isende kivyake??? Wananchi wengi wameishaonyesha wazi kukinaishwa na Muungano......ni wakati sasa kila m2 afe kivyake....kila m2 achukue kilicho chake....
 
Huo ndio utakua mwisho wa Muungano. Sijui kati ya Bara na Visiwani ni wepi watakaoumia.
Hautakuwa mwisho wa muungano kama walipitisha wimbo wao wa taifa na bendera yao unafikiri hili litawasitua wabara.Unaelewa wabara tunapenda sana sifa.na wengi wao hawana uzalendo na nchi hii.Hebu fikiria baada ya kuruhusu wawekezaji kwenye kilimo kutoka nje sheria ya ardhi ilipitishwa na kuongeza umiliki wa ardhi toka miaka 33 hadi 99.
 
Nemegundua sasa kumbe dhamira yenu wazanzibar wafe njaa, mnataka wasiwe na hata kamradi hivi ka kujiingizia? wasubiri mgao wa muungano tu mgao wenyewe mpaka mafisadi wajigawie kwanza aaaa mtu kimfaacho chake bwana, kwahili semeni mpaka mdate kama hamtaki kulipa mtahama.
watakufanye njaa huku wamejazana bara wanalima mashamba makubwa wanaendesha biashara kubwa za kila aina tatizo hawapeleki pesa zanzibar bari kule kwa mjomba.
 
..kunaweza kukawa na viwango vya kodi wa wa-Zenj.

..halafu kikawekwa kiwango kingine kwa wa-Bara wanaotaka kuweka makazi na uwekezaji Zenj.

..haki itatendeka kama baada ya muda fulani wa kuishi Zenj, m-Bara akawa na haki sawa kama wa-Zenj, na kuruhusiwa kulipa kiwango cha kodi kinacholingana na wa-Zenj wengine.
 
Hebu tulia kwanza. Haya maneno ya Nyerere hapa hayafanyi kazi maana siyo sisi tueanza kuuvunja Muungano na kutenga watu. Tumelilia sana turekebishe mambo na tubaki pamoja. Tumeitwa majina ya ajabu sana, tumenyanyaswa na sasa tunaanza kutengwa waziwazi.

Nyerere huko juu, nafikiri utakuwa na sisi wakati tukiruhusu Wazenji KULA NYAMA YA MTU. Wao ndiyo wataendelea kulana. Kwani sisi kuna kabila linataka kujitenga Tanganyika? Au kuna mtu kasema kabila fulani inabidi litengwe? So longer Wanyamwezi/Wasukuma bado hawana noma, Tanganyika itasimama pamoja.

Mbona unaleta CHANO hata pepo bado hajataja jina ?.....Mungano ni kama mapenzi ni jambo la hiyari na huwezi kulazimisha .umesahau pale Rais aliposema ndani ya Bunge wakati ule wa mjadala wa upatanishaji wa mpasuko kule zanzibar na wajumbe wa CCM kutoka ZANZIBAR wakatowa maneno ambayo yalishangaza bunge na hata kufikilia kusema wapo tayari warudi na ASP yao. Hakukuwa na mtu hata mmoja aliyeweza nyanyuwa mdomo wake kuikemea kauli ile, sasa jiulize kauli kama hii nani anaweza ingilia wakati imo ndani ya katiba ya SMZ.Tukirudia kauli ya kule bungeni hata Rais Kikwete aliwatetea wajumbe kutoka CCM ZANZIBAR, kwa kusema wajumbe wale wametumia haki yao kikatiba ,sasa na kwa kauli yao hii wanatumia haki yao kikatiba na kama hupendezewi ni vizuri ukanyamaza tu kwani wewe huzimi ,na wala huwashi inapokuja mamuzi yao serekali ya ZANZIBAR.
 
Mzalendohalisi,

Huyo Mkuu wa kodi wa Zanzibar ametoa vipengele vya sheria yao, yuko makini sana huyo mtu. Kwa nini umkosoe kiongozi anaetekeleza sheria? Wa-bara mnaotaka Serikali itoe tamko kuwafurumusha wapemba Buguruni ni lazima mjiulize kama mnayo sheria. Katiba imewaruhusu Wanzanzibar wawe na sheria zao, za mambo yao. Sisi tulikubaliana nao kwamba chetu chao, chao chao.

Tulikuwa tunaambiwa eti ni hatari kuwa jirani na kisiwa kinaelea elea tu, tukichukue tukimiliki. Hii ndio bei ya haka ka kisiwa, ka nchi kadogo hata Masasi kubwa mara tano unawapa Vice President na Mawaziri na nafasi zaidi ya hamsini kwenye Bunge la majimbo 232. Wamejaa Bungeni, Cabinet, Uongozi wa Vyama, wamejaa Buguruni, Namanga, wamejaa Kariakoo, kila kona. Lakini kwao wao tusijae, kwa mujibu wa sheria. Tulitaka wenyewe hiki ki ndoa hiki, sio Zanzibar ndio tatizo, ni sisi ndio tulijiingiza kwenye huu mkenge.

Naam na huu muungano uchwara unalindwa kwa kila hali na the so called viongozi wa chama na serikali ili kulinda maslahi yao. Watanganyika hatuutaki maana ni muungano ambao una kasoro chungu nzima ambazo viongozi hao wa chama na serikali wanazifumbia macho na pia hauna maslahi yoyote kwa Watanganyika, kwa mfano Z'bar pia imechangia sana katika matatizo ya TANESCO kwa kukataa kulipa mabilioni ya bills za umeme ambayo walitakiwa wayalipe kwa TANESCO.
 
Nadhani walichotakiwa kufanya katika kupanga gharama ya kodi ni kuweka makundi matatu, yaani wazanzibari, watanganyika(watanzania ambao sio wazanzibari) na wageni. Kuweka mgogo kundi moja na mjerumani si sahihi kisiasa. Ni vyema gharama hizi zipitiwe upya.
 
Back
Top Bottom