SMZ yazidi kuubomoa Muungano yataka bara walipe kodi ya ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMZ yazidi kuubomoa Muungano yataka bara walipe kodi ya ardhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makaayamawe, May 10, 2009.

 1. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  SMZ yazidi kuubomoa Muungano yataka bara walipe kodi ya ardhi
  Na Salma Said, Zanzibar

  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imetangaza mkakati mpya wa kuwataka wawekezaji na watu wenye asili ya Tanzania Bara kusajiliwa na kuanza kulipa kodi ya ardhi ya dola za Marekani 5000 (Sh6.5 milioni), kila mwaka kwa kila hekta moja ya ardhi.


  Hata hivyo, SMZ ilisema mwekezaji mwenye asili ya Zanzibar atapaswa kulipa dola 500 (Sh650,000).

  Mpango huo umetangazwa jana na Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB), Mohammed Hashim Ismail kufuatia bodi hiyo kupewa uwakala wa kusimamia na kukusanya kodi ya ardhi.

  Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Zanzibar ya mwaka 1992, Mzanzibari tu ndiye mwenye haki ya kumiliki ardhi, lakini wageni wote wanapaswa kukodishwa wakiwemo watu wenye asili ya Tanzania Bara.

  “Hatua hii itatuwezesha pia kuwafahamu wamiliki wote wakubwa na wadogo wadogo wa vipande vyote vya ardhi hapa Zanzibar pamoja na wale ambao wanatajwa kuhodhi maeneo kinyume na utaratibu,” alisema kamishna huyo.

  Alisema hatua hiyo itawasaidia kuwatambua wasiokuwa Wazanzibari na kuishauri serikali kuchukua hatua zinazofaa.

  Kamishna huyo alisema viwango vya malipo vitapitiwa upya ili viende na wakati na kuishauri serikali juu ya hatua sinazostahili kuchukuliwa.

  Alisema ardhi ni suala muhimu katika kupambana na umasikini na kukuza uchumi wa Zanzibar, ndio maana serikali imeamua kuhakiki upya viwanja vya makazi kupitia mradi wa SMOLE.

  Kamishna huyo alisema kupitia mradi huo taarifa zote zitaingizwa katika mfumo wa kompyuta ili kuweza kuwatambua watu wote waliokodishwa ardhi.

  Hashim Ismail alisema kwamba bodi ya mapato imeanza kujitayarisha kwa ajili kukusanya fedha hizo pamoja na kuwatambua waliopewa ardhi kinyume cha sheria. Hata hivyo zoezi hilo linatarajiwa kuibua mjadala mkubwa kutokana na ukweli kwamba, inachochea ubaguzi kati ya Watanzania Bara na Wazanzibari hivyo kuendelea kuudhoofisha muungano.
   
  Last edited by a moderator: May 10, 2009
 2. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hiki kibao wakigeuziwa Wazenji/Wapemba, pale Buguruni vile vibanda vya mbao naona vitatoweka.
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hivi Wapemba/waunguja nao tukuanza kuwabagua bara: nchi itakalika kweli?
   
 4. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huo ndio utakua mwisho wa Muungano. Sijui kati ya Bara na Visiwani ni wepi watakaoumia.
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hawa wazenji bwana..anyway wacha tuone
   
 6. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hiizi habari sometime zinakuwa kama movie vile, hivi swala kama hili linawezaje kufika public na serikali ya muungano ikakaa kimya?. Kama ndivyo, mii naona hakuna haja ya kulazimisha urafiki, tuwape uhuru wao tumewanyanyasa vyakutosha lakini tamko hilo liwe two way traffic, hivyo hata wapemba walioko bara watozwe ushuru wanamna hiyo
   
 7. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  SMZ (CCM) walisha wahi sema kuwa wao hawana waafuwasi huku bara wale wafanya biasha ni wafuwasi wa CUF ambao ni wapemba sasa ukianza kuwashambulia wapemba wanaofanya biasha na kuishi hapa Dar au bara utakuwa unakoseya
   
  Last edited: May 10, 2009
 8. Black Jesus

  Black Jesus JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2009
  Joined: Mar 7, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  SMZ (CCM) walisha wahi sema kuwa wao hawana waafuwasi huku bara wale wafanya biasha ni wafuwasi wa CUF ambao ni wapemba sasa ukianza kuwashambulia wapemba wanaofanya biasha na kuishi hapa Dar au bara utakuwa unakoseya
   
 9. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hili ndiyo tatizo ya serikali mbili. Zanzibar wana platform ya kutoa madai yao. Zenji wana ZRA iliyo baki ni TRA which is ya muungano. Sasa ukiwatoza wazenji wanaokaa bara utawa tozaje wakati TRA ni Tanzania siyo Tanganyika Revenue Authority. Kungekua na serikali tatu at least yote haya isinge kua shida. Tatizo ni kwamba Zanzibar imekua ya wazanzibar na Tanganyika imekua ya Tanzania. Simply put the situation now on the point of view of Zanzibaris ni changu ni changu na chako ni chetu. It's sad but its the truth. Wazanzibarr wana mamlaka zao inayo shugulikia mambo yao wenyewe lakini Tanzania bara hakuna, kila kitu ni muungano.
   
 10. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mzalendohalisi,

  Huyo Mkuu wa kodi wa Zanzibar ametoa vipengele vya sheria yao, yuko makini sana huyo mtu. Kwa nini umkosoe kiongozi anaetekeleza sheria? Wa-bara mnaotaka Serikali itoe tamko kuwafurumusha wapemba Buguruni ni lazima mjiulize kama mnayo sheria. Katiba imewaruhusu Wanzanzibar wawe na sheria zao, za mambo yao. Sisi tulikubaliana nao kwamba chetu chao, chao chao.

  Tulikuwa tunaambiwa eti ni hatari kuwa jirani na kisiwa kinaelea elea tu, tukichukue tukimiliki. Hii ndio bei ya haka ka kisiwa, ka nchi kadogo hata Masasi kubwa mara tano unawapa Vice President na Mawaziri na nafasi zaidi ya hamsini kwenye Bunge la majimbo 232. Wamejaa Bungeni, Cabinet, Uongozi wa Vyama, wamejaa Buguruni, Namanga, wamejaa Kariakoo, kila kona. Lakini kwao wao tusijae, kwa mujibu wa sheria. Tulitaka wenyewe hiki ki ndoa hiki, sio Zanzibar ndio tatizo, ni sisi ndio tulijiingiza kwenye huu mkenge.
   
  Last edited: May 10, 2009
 11. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Tatizo Tanganyika yenu mumeivisha koti la Tanzania mlizani huo ndio ujanja wa ku-ikoloni. Wazenj wamesha tambua janja ya Tanganyika nawao sasa wanakuja kivyengine
   
 12. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Naona wadanganyika wanaanza chuki..lol
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Dilunga umeliweka vizuri hili suala ila umamelizia na chuki na jazba..(kama kawa ya wadanganyika,lol)

  Wazanzibari wana sirikali yao na sheria zao..hili umeliweka vyema. Serikali ya Znz imeonelea ni vyema iwatoze wamiliki wa ardhi yake, ktk malengo ya kufuta umaskini na pia kuhakikisha wamiliki wa ardhi wote wanajulikana. Hakuna ubaya ktk hili. Kama wadanganyika mmeshindwa kulifanya hili kwenu, basi pole zenu lakini msilete chuki zenu kwenye anga za wengine..

  Haya nasubiria chuki zaidi ..lol
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kheeeeee heeeeeee heeeeeeh! Hii ni kodi ya kawaida tu, ilitakiwa iwe inakusanywa na baraza la manispaaa, lakini kwa kuwa wao ni wachovu ilishindikana. Lakini sio suala jipya na halina uhusiano wowote na Muungano.

  Hata huko Tanganyika kodi kama hii kuna baadhi ya watu wanalipa, sio kule kwenye ujenzi holela!
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Baambie hao..

  Mbona hata bara kuna kodi za viwanja, majengo blah blah..Hili hawalioni..lol
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Habari ndio hiyo, nashangaa huyo mwandishi wa habari alivyoipamba hii habari kwa kichwa cha kibaguzi na ni kama ni kitu kipya sana! Na humu wengi wameingia mkenge na kuanza kutoa maneno ya chuki!

  Lakini Tz kuna tatizo la wananchi wake kulipa kodi... zile dezo za miaka ile zimelipeleka Taifa katika hali mbaya!
   
 17. M

  Mtwike Senior Member

  #17
  May 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Theoreticaly, yes, cha wazanzibari chao ni chao, cha muungano chetu! lakini practicaly kwa Muungano, chetu ni chetu (mf. gesi) na chenu ni chetu!
   
 18. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #18
  May 10, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Yawezekana wazanzibar wana fanywa koloni na Tanganyika ,maana binafsi sioni kwanini kuwa ng'anga'ania namna hiyo.Mtu mruhusu kwa kile anachoona kwake ni bora na kumkatilia atakacho huo ni UBEBERU.

  Wazanzibar waachiwe nchi yao wapewe uhuru wao wanautafuta .Kigezo ama sababu zile sijui ni za kweli ama uongo eti za kiusalama leo Hazina mwanya tena.
   
 19. S

  Stone Town Senior Member

  #19
  May 10, 2009
  Joined: May 28, 2007
  Messages: 108
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  asalamu alaykum.

  wanasiasa na wasomi mara kadhaa wameshasema mfumo huu wa muungano upitiwe upya hauna maslahi kwa pende mbli bali wa wachache sisi watanzania tumebakia kushbikia mambo tusioyajua sasa hii ndio gharama yake. zanzibar wamenukuu vifungu vya sheria kuwa mtu asiyekuwa mzanzibari hana haki ya kumiliki ardhi zanzibar na kweli sheria inasema hivyo sasa kamishna afanye nini wakati sheria inasema hivyo cha msingi ni kurejea katika katiba ufanyiwe marekebisho au kubaki na sheria hizo hizo mbaya na zenye kuwanufaisha wachache.

  watu wanapojadili muungano wanatokea wengine kujifanya ndio waumini wazuri wa muungano na kuwaona wengine ni wajinga sasa hizi ndio gharama ama tuzikubali ama tuzikatae mwisho wa yote watanzania ndio waamuzi kama wataendelea kulala basi waendelee la hawataki kulala waanzishwe majadiliano na makongamano ya kuuzungumzia mfumo wa muungano kwa maslahi ya pande mbili.

  kila la kheri.
   
 20. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #20
  May 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Nemegundua sasa kumbe dhamira yenu wazanzibar wafe njaa, mnataka wasiwe na hata kamradi hivi ka kujiingizia? wasubiri mgao wa muungano tu mgao wenyewe mpaka mafisadi wajigawie kwanza aaaa mtu kimfaacho chake bwana, kwahili semeni mpaka mdate kama hamtaki kulipa mtahama.
   
Loading...