Smz yaombwa kuzipatia ufumbuzi kero za muungano kabla ya katiba mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Smz yaombwa kuzipatia ufumbuzi kero za muungano kabla ya katiba mpya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Aug 10, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2][​IMG][/h]Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeombwa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya muungano yanayolalamikiwa na Zanzibar kabla ya kuanza kwa katiba mpya ya Jamhuri ya muungano Tanzania.
  Mwakilishi wa kuteuliwa Ali Mzee Ali amesema taasisi kama vile benki kuu BOT, mamlaka ya mapato Tanzania TRA na taasisi nyingine zinalalamikiwa na upande wa pili wa muungano kwa madai ya kukwamisha maendeleo ya uchumi wa Zanzibar.
  Akichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya fedha, uchumi na mipango ya maendeleo katika kikao cha baraza la wawakilishi amesema muundo wa taasisi hizo haziko katika mfumo wa muungano na kusababisha matatizo kutokana na utendaji wake kufimbiwa macho na serikali zote mbili.
  Hivyo ameiomba serikali ya mapinduzi Zanzibar kupitia vikao vya kutatua kero za muungano kuyapatia ufuimbuzi matatizo hayo kabla ya kuanza kwa katiba mpya
  Nae mwakilishi wa jimbo la Kwamtipura Hamza Hassan Juma ameiomba serikali kuingilia kukwama kwa zaidi ya gari 500 za wafanyabiashara wa Zanzibar katika bandari ya Dar es Salaam.
  Amesema tatizo la wafanyabiashara wa Zanzibar kutozwa kodi mara mbili limechangia kukwama kwa gari hizo, hivyo iko haja ya kwa serikali kulipatiwa ufmbuzi wa haraka.
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,692
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Magari ya Wazanzibari kwa nini yanapitia Dar es Salaam. Bandari yenu ina matatizo gani? Au Wazanzibari wanapitisha magari yao Dar ili kukwepa kero za Muungano Zanzibar? Nisaidieni. Kichwa kinazunguka.
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Zanzibar kama mnakumbuka wakati wa awamu ya mwinyi ilikiwa sehemu ya kupitisha vitu bila kulipia kodi hata sasa hakuna utaratibu wa kuzuia vitu visivyolipiwa kodi kupitia zanzibar na ndiyo maana bandari ya Zanzibar inapunguza umashuhuri hasa kwa wakusanya kodi. Kama Zanzibar wanataka kila kitu kiwe pande zote je muungano unamuhimu gani sasa si bora muwe na nchi inayojitegemea kwa asimila 100% TRA na BOT zitasaidia nini kwa Tanzania badala ya gharama tu?. Tusikoangalia wataanza kusema bandari ya Zanzibar ni huru haina kodi n.k huwezi kuwa na nchi moja na sheria mbili ni wakati wa kufanya uamuzi mmoja je Zanzibar inataka kuwa nchi moja ya Tanzania au inataka kuwa nchi pekee 100% na iwe na mipaka na tuachane kwa nia moja lakini huu muungano wa matatizo kila siku hausaidii nchi yeyote maana Wanzanzibar wanafikiri wanaonewa na Wabara wanafikiri wanafanya mengi bila sababu. Tuweke mipaka ya security na mikataba ya kijeshi na tutengane au tuungane kama nchi moja. Serikali mbili, tatu ni upuuzi mkubwa.
   
Loading...