SMZ yakana kufuja fedha kwa `mashangingi`

Mzee wa Kale

Member
Feb 7, 2009
44
0
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema haijatumia fedha za umma kununulia magari ya kifahari maarufu kama mashangingi bali yamepatikana kupitia msamaha wa madeni.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake katika Mtaa wa Vuga mjini Unguja jana.

Juma alisema SMZ baada ya kupata msamaha wa madeni kuna fedha zilipatikana na ndipo ikaamua kuondoa tatizo la huduma ya usafiri hasa kwa viongozi wa kitaifa kwa kununua magari hayo.

``Magari haya hatukununua kwa fedha mkononi bali tulinufaika na msamaha wa madeni na sehemu ya fedha zilizokuwa zipatikane tukashauriwa tunahitaji kitu gani ndipo tukapendekeza kuzitumia kwa kununua magari,`` alisema.

Alisema sehemu nyingine ya fedha hizo waliamua kununulia matrekta ili kuboresha sekta ya kilimo visiwani hapa na kupambana na umaskini.

Waziri huyo bila kutaja thamani ya magari hayo alisema yaliyonunuliwa ni 80 aina ya Toyota Prado na Rav 4.

``Kwa sasa siwezi kusema yamegharimu kiasi gani naomba munipe muda hadi hapo baadaye, isipokuwa naweza kusema serikali ipo makini katika matumizi ya fedha za umma,`` alisema.

Alifafanua kuwa hali ya huduma ya usafiri kwa viongozi serikalini ilikuwa mbaya hasa kwa Kisiwa cha Pemba na Tanzania Bara ambako baadhi ya viongozi walikuwa wakilazimika kukodi teksi kwa ajili ya safari zao.

``Mfano gari langu lilikuwa likipita mitaani likipiga kelele kama kuna panya ndani na ofisi ya Waziri Kiongozi Pemba haikuwa na gari hata moja na walilazimika kuazima Idara nyengine kwa ajili ya shughuli za kikazi``, alisema.

Tamko hilo la Serikali ya Zanzibar limekuja kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)kuilalamikia SMZ kwa kufuja fedha kwa kununua mashangingi badala ya kutumia kuboresha huduma jamii ikiwamo afya na elimu.

SOURCE: Nipashe
 
duh,siasa kweli ni matumizi mazuri ya maneno na kuyapinda pinda ili yaonekane matamu.sasa hizo madeni na fedha ambazo wamesamehewa si pia yana gusa moja kwa moja walipa kodi au ?naomba nielimishwe hapo.lakini yote hayo ni ufisadi tu na kutufanya mbumbumbu.kweli yaani tunadaganywa kama wazembe.
 
Alifafanua kuwa hali ya huduma ya usafiri kwa viongozi serikalini ilikuwa mbaya hasa kwa Kisiwa cha Pemba na Tanzania Bara ambako baadhi ya viongozi walikuwa wakilazimika kukodi teksi kwa ajili ya safari zao.

Hivi hawawezi kusema kitu bila kuingiza Tanzania Bara? Sitashangaa wakibanwa wakija sema kuwa walinunua hayo mashangingi kutokana na shinikizo kutoka serikali ya Muungano!
 
Chadema walipokua wanahutubia mkutano pale Kombawapya walienda mbali zaidi na kusema kwamba SMZ ni kama Saccos ya familia watu wanafanya wanavyojiskia kwa kuwa hakuna wanachokiogopa, katika mazingira ya Zanzibar Waziri hata ukimpa Bajaj lingemtosha na angewahi kufika ofisini na kurudi nyumbani hii walioifanya ya kununua magari ya kifahari kwakweli wamefanya kufuru.

Jumamosi ya Valentine Chadema wanaendelea na Operesheni Sangara katika Uwanja wa Kibandamaiti ngoja tuone kitu gani kitatokea maana jamaa inaonekana wamejiandaa kweli.
 
Hivi ukisamehewa madeni unalipwa feza ? Jamani aliefahamu hebu anifahamishe hapa kwenye mahesabu ya wakubwa ?
 
Mkuu Mwiba nadhani hapo kuna ufisadi wa 10% umepita, na la pili kwa kuwa wakubwa kipindi hiki ni cha mwisho wanamalizia bila shaka ukifika mwezi wa Mei 2010 watauziana magari hayo kwa Tshs 200,000?= tu.
 
Msamaha wa kodi ndio wanapeleka kwenye Mashangingi? Kweli priorities zetu ziko mrama kweli kweli.

Hiyo misamaha ni kwa ajili ya shule na mambo ya maendeleo na sio Mashangingi.
 
Mwiba,
Unaona RAHA YA KUUWA MUUNGANO? Umepiga kelele wee jinsi tunavyowaibia na kusema sisi Wabara tulivyo wa ovyo. Sasa hata hii hamkujua kama siyo CHADEMA. Kama mnafikiri Muungano ukifa basi UFISADI utaisha Zenji, kwa kweli mlie. Kwa hili swla NAIPONGEZA SMS kwa kuonyesha waziwazi kuwa UFISADI hauna Ubara wala U-Zanzibar.
Nashindwa kujua kwa nini wasingelinunua RAV4 80 na Prado 4. Halafu magari hayo yote ni lazima yanunuliwe kwa mpigo? Ili yaishe yote? Hapo utakuta wamenunua Matrekta 3 ili kusema tumenunua magari na matrekta. Duu, uchaguzi unakaribia. Wakiuziana kwa bei chee, na baadaye wayauze kwa bei juu, zitatosha kwenda kiwandani na kushonesha T-SHIRT za kijani na mashati yenye alama ya JEMBE NA NYUNDO.
Na hapo subirini MAFUTA yapatikane. Wataanza kununua hadi ndege/helkopita za serikali kwani kuja Dar kuna foleni kubwa sana BAHARINI.
 
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Alisema sehemu nyingine ya fedha hizo waliamua kununulia matrekta ili kuboresha sekta ya kilimo visiwani hapa na kupambana na umaskini.

Hayo matrekta mbona hatuyaoni? Waziri mbona anataka kudanganya umma? Hizo gari zote zilipokuja zilifikia karakana iliyopo pale Mbweni karibu na Idara ya Kilimo (ASSP), hakukuwa na trekta japo la kudanganyia watu!!!

Gari zipo nyingi tu but SMZ imegubikwa na lindi la ufisadi, kuna SHIRIKA LA BIASHARA YA MAGARI LA SMZ. Hili shirika linakaribia kufa kwa kukosa kazi za kufanya zaidi ya kukopesha vespa,baiskeli na cherehani. Kuna wafanyakazi chungu nzima wa gereji ya hilo Shirika la Biashara ya Magari hawana kazi yoyote wanayofanya but kila mwisho wa mwezi wanaenda kukinga mshahara ambao hawakuufanyia kazi yoyote zaidi ya kupiga soga, kucheza draft, saa 7 ikifika msikitini na akirudi huko anaingia mtaani.

Hili shirika kama lingekuwa linathaminiwa lingekuwa mkombozi mzuri sana wa magari ya serikali (smz) na yale ya mashirika ya umma (SLS); kwani lina wataalamu wazuri sn waliobobea ktk fani ya utengeneza wa kila aina ya magari.

Mfano mdogo tu; Pale Ofisini kwa huyo Waziri kuan gari zaidi ya tatu, likiwemo Pajero Intercooler lipo ktk hali nzuri kabisa but ni bovu limewekwa halina kazi yoyote, sanasana gharama ya kifaa ukiulizia utashangaa kwamba serikali haiwezi kununua hicho kifaa? But kwa hapa visiwani unaweza kulia kwa jinsi fedha za walipa kodi zinavyochezewa na kutafunwa hali kuna hali duni ktk shule (a.k.a skuli), hospital na ktk vuo vya elimu ya ufundi na uuguzi.

Thnx
 
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema haijatumia fedha za umma kununulia magari ya kifahari maarufu kama mashangingi bali yamepatikana kupitia msamaha wa madeni.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake katika Mtaa wa Vuga mjini Unguja jana.

Juma alisema SMZ baada ya kupata msamaha wa madeni kuna fedha zilipatikana na ndipo ikaamua kuondoa tatizo la huduma ya usafiri hasa kwa viongozi wa kitaifa kwa kununua magari hayo.

``Magari haya hatukununua kwa fedha mkononi bali tulinufaika na msamaha wa madeni na sehemu ya fedha zilizokuwa zipatikane tukashauriwa tunahitaji kitu gani ndipo tukapendekeza kuzitumia kwa kununua magari,`` alisema.

Alisema sehemu nyingine ya fedha hizo waliamua kununulia matrekta ili kuboresha sekta ya kilimo visiwani hapa na kupambana na umaskini.

Waziri huyo bila kutaja thamani ya magari hayo alisema yaliyonunuliwa ni 80 aina ya Toyota Prado na Rav 4.

``Kwa sasa siwezi kusema yamegharimu kiasi gani naomba munipe muda hadi hapo baadaye, isipokuwa naweza kusema serikali ipo makini katika matumizi ya fedha za umma,`` alisema.

Alifafanua kuwa hali ya huduma ya usafiri kwa viongozi serikalini ilikuwa mbaya hasa kwa Kisiwa cha Pemba na Tanzania Bara ambako baadhi ya viongozi walikuwa wakilazimika kukodi teksi kwa ajili ya safari zao.

``Mfano gari langu lilikuwa likipita mitaani likipiga kelele kama kuna panya ndani na ofisi ya Waziri Kiongozi Pemba haikuwa na gari hata moja na walilazimika kuazima Idara nyengine kwa ajili ya shughuli za kikazi``, alisema.

Tamko hilo la Serikali ya Zanzibar limekuja kufuatia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)kuilalamikia SMZ kwa kufuja fedha kwa kununua mashangingi badala ya kutumia kuboresha huduma jamii ikiwamo afya na elimu.

SOURCE: Nipashe

Haya ni matokeo ya kuwa na viongozi wenye uelewa mdogo mno kimawazo. Nasikia aibu kujiita Mtanzania... Maana kama mtu aliyeaminika na kupewa madaraka makubwa kuwaongoza watanzania ana ufinyu mkubwa wa kufikiri to this extent then how about yule mtanzania wa kawaida anayelima karafuu kule kijijini?

I think kuna haja ya viongozi kuhojiwa kuangalia intelligence zao kabla ya kuwapa madaraka makubwa. Ningependekeza kahojiano ya namna hii yawe live kwenye TV.
 
Hivi hawawezi kusema kitu bila kuingiza Tanzania Bara? Sitashangaa wakibanwa wakija sema kuwa walinunua hayo mashangingi kutokana na shinikizo kutoka serikali ya Muungano!
:D
SMZ ina ofisi kadhaa huko Tanzania Bara, hivyo nao ni muhimu kukumbukwa katika neema kama hizi.
 
Kwa Tarifa zenu hiyo ndiyo SMZ mimi binafsi nimeridhika na majibu ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma. Ndugu zetu hawa wanayo website ya majibu kwa lolote lile hakuna cha kushangaza hapo wamesamehewa madeni wakahisi kwa vile kuna baadhi ya magari ya Viongozi wa SMZ kama alivyokwisha sema Mr Hamza Hassan Juma kwaMfano gari llake lilikuwa likipita mitaani likipiga kelele kama kuna panya ndani
 
Mwiba,
Mkuu hilo swali zuri sana!... yaani wee acha tu..
Tanzania kweli hatuna viongozi...duh! bila aibu mtu mzima anakuja na maelezo ambayo hata mtoto mdogo hawezi kuyapokea! Ujinga gani huu...ati fedha imetokana na msamaha wa madeni, ndfio yale yale ya EPA - fedha sio za wananchi sijui zilifikaje Benki kuu!
 
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema haijatumia fedha za umma kununulia magari ya kifahari maarufu kama mashangingi bali yamepatikana kupitia msamaha wa madeni.

Ring a bell ? Heard similar quotes before ? Remember Mustafa Mkulo on EPA ? What's wrong with our leaders - one thing I know for sure, they are definitely not a reflection of me !! And here I am, sitting and thinking there's still something to be salvaged - no, the system is rotten to the core - it's beyond repair, it should be dumped at its rightful place - garbage pit.
 
Kwa Tarifa zenu hiyo ndiyo SMZ mimi binafsi nimeridhika na majibu ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Kiongozi, Hamza Hassan Juma. Ndugu zetu hawa wanayo website ya majibu kwa lolote lile hakuna cha kushangaza hapo wamesamehewa madeni wakahisi kwa vile kuna baadhi ya magari ya Viongozi wa SMZ kama alivyokwisha sema Mr Hamza Hassan Juma kwaMfano gari llake lilikuwa likipita mitaani likipiga kelele kama kuna panya ndani

Hilo gari la huyu mheshimiwa linalopiga kelele lina umri gani? Nini service record yake? Magari yanapiga makelele kwa sababu hatujui maana ya maintenance. Kisingizio cha barabara mbovu hakina mantik. Kama barabara ni mbovu kwa nini mtu uendeshe mwendo wa kasi? Tunapenda mno vitu vipya badala ya kutunza tulivyonavyo. Hata haya mashangingi yakikosa maintenance baada ya muda mfupi yatapiga kelele kama kuna panya ndani!

Amandla.......
 
Ndugu yangu unafahamu mantiki ya maintenance, unafahamu nini uchakavu. Jee unafahamu kuwa ku-maintain gari chakafu ni bora kununua mpya ukaachana na chakafu.Jee una fahamu kuwa life-span ya magari (hasa haya yanayotengenezwa siku hizi) ni miaka isiyozidi mitano. Jee unajua hayo magari anayozongumzia Mh. Hamza yana umri gani? (wa uchakavu) Na hata hayo mashangingi wanayopanda Mawaziri na makatibu Wakuu (Toyota Crecida nyeupe na za bluu zilizonunuliwa tokea wakati wa awamu ya kwanza ya Salmin) zina umri gani?. Unajua kuwa Toyota Company sasa hata Crecida hawatengenezi tena. Usilaumu tu angalia pande zote.
 
Pamoja na yote SMZ kununua Magari haya ni very irresponsible act! Kama zimepatikana fedha za msamaha ilitakiwa zitumiwe katika kuboresha mambo yaliyo muhimu zaidi, angalia matokeo ya form 4 utapata picha kamili kwamba SMZ inaongozwa na watu wasiojua where to prioritise?
It is about time for SMZ Leaders to come clean and be hold accountable!
Utakuta Gari la Waziri ama Mwakilishi nje ya saa za kazi na ndani ya hilo gari hata waziri wenyewe hayumo? Iweje Gari la Mh. waziri ukalione sijui kwenye rusha roho limemleta Mamsap na ma-besti wake wakonge roho?
 
Ndugu yangu unafahamu mantiki ya maintenance, unafahamu nini uchakavu. Jee unafahamu kuwa ku-maintain gari chakafu ni bora kununua mpya ukaachana na chakafu.Jee una fahamu kuwa life-span ya magari (hasa haya yanayotengenezwa siku hizi) ni miaka isiyozidi mitano. Jee unajua hayo magari anayozongumzia Mh. Hamza yana umri gani? (wa uchakavu) Na hata hayo mashangingi wanayopanda Mawaziri na makatibu Wakuu (Toyota Crecida nyeupe na za bluu zilizonunuliwa tokea wakati wa awamu ya kwanza ya Salmin) zina umri gani?. Unajua kuwa Toyota Company sasa hata Crecida hawatengenezi tena. Usilaumu tu angalia pande zote.

Hilo gari la huyu mheshimiwa linalopiga kelele lina umri gani? Nini service record yake?

Si ndiyo maana nikauliza hilo gari lina umri gani? Mbona badala ya kujibu unaniuliza swali nililouliza? Pamoja na huo umri, swali langu lingine lilikuwa maintenance record ya hayo magari kama ipo? Sisi tunajijua, hatuthamini maintenance hata siku moja. Kuanzia magari mpaka majengo yetu. Ndiyo maana nikauliza hilo swali. Umri si hoja. Watu bado wanaendesha Ford Model T itakuwa hiyo Cressida!

Amandla........
 
Pamoja na yote SMZ kununua Magari haya ni very irresponsible act! Kama zimepatikana fedha za msamaha ilitakiwa zitumiwe katika kuboresha mambo yaliyo muhimu zaidi, angalia matokeo ya form 4 utapata picha kamili kwamba SMZ inaongozwa na watu wasiojua where to prioritise?It is about time for SMZ Leaders to come clean and be hold accountable!
Utakuta Gari la Waziri ama Mwakilishi nje ya saa za kazi na ndani ya hilo gari hata waziri wenyewe hayumo? Iweje Gari la Mh. waziri ukalione sijui kwenye rusha roho limemleta Mamsap na ma-besti wake wakonge roho?
Magari anayozungumzia huyo Waziri ni vitendea kazi- hivyo ni neccessity na siyo luxury. Magari naamini kuwa ni vitendea kazi kama ilivyo simu, kalamu na vyenginevyo hivyo magari (yanayoendesheka) ni muhimu kwa Watendaji wa Serikali, ili Serikali ifanikishe majukumu yake. Kuhusu priorities kama za Elimu . Hiyo ina programme yake ya muda mrefu na mfupi. Hebu durusu alelezayo Mh. Waziri wa Elimu (Bw. Haroun) . Lipo hata la kuboresha Karume Tech. College iwe Chuo Kikuu cha Ufundi. Mipango yote hiyo inaratibiwa na ina mafedha yake kutoka ndani na kwa Wafadhili. Sasa itasimamiwa na kutekelezwa vipi ikiwa Bw. Haruna mwenyewe anategemea usafiri wa mkweche? Bw. Mkweli kuwa Mkweli na uone Ukweli.
 
Mkuu Pakacha mimi sio mwanasiasa kwa hio sitoingia huko katika siasa ila naeleza lile nililoliona kwa macho, nimekueleza:
Matokeo ya form 4 zanzibar wamefanya vibaya huu ndio ukweli, sote tunajua Gari ni kitendea kazi na hakuna anaetegemea kwamba Bwana Haruna aende kazini na Baiskeli? Magari mengi ya SMZ yanatumiwa vibaya kwa shughuli zilizo nje ya Kikazi na sio kwa kumpeleka Mheshimiwa kazini na kurudi. SMZ inaingia gharama nyingi zisizo na msingi kwa matumizi mabaya ya haya magari, kuanzia mafuta, service na mileage zisizo na msingi. Laiti kama zitapigwa hesabu gharama za kuyahudumia hayo magari 80 ukitoa zile za kumpeleka Muhusika kazini ama kwenye mradi basi naamini zinaweza kupatikana fedha za kununua vitabu japo kwa shule moja ama kupeleka madawa kule Mnazimmoja.
Na niliposema gari la Mh. Waziri kwenda kumpeleka mamsapu rusharoho ni kwamba hili nimelishuhudia kwa macho yangu.
Kwa hio mkuu punguza munkari ya siasa na tujadili jinsi ya kupeleka maendeleo kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom