SMZ yaeleza mabadiliko mambo ya muungano yanavyofanyika

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Mabadiliko katika orodha ya mambo ya Muungano yamekuwa yakifanyika kwa kuzingatia Katibana sheria kwa madhumuni ya kuimarisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, MohammedAboud, wakati akijibu swali la Mwakilishi Saleh Nassor Juma wa Jimbo la Wawi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea, Chukwani Zanzibar.
Alisema ipo hati ya makubadiliano kuhusu mambo ya muungano na marekebisho yake yamekuwa yakifanyika kwa ridhaa ya Bunge kama chombo cha wawakilishi wa wananchi wapande mbili za muungano.
“Mheshimiwa Spika mabadiliko yote yaliofanyika katika orodha ya mambo ya muungano yamefanyika kihalali kwa kuzingatia Katiba na sheria kwa madhumuni ya kuimarisha muungano wenyewe.” alisema Waziri Aboud.
Hata hivyo, alisema tangu kufikiwa kwa Muungano mwaka 1964, Zanzibar imetoa nafasi ya Waziri Mkuu mara moja pamoja na Mwenyekiti wa Bunge mwaka 2005 hadi 2010.
Alisema wadhifa wa Waziri Mkuuumewahi kushikwa na Mzanzibari, Salim Ahmed Salim, sawa na wadhifa wa Mwenyekiti wa Bunge, Zuberi Ali Maulid, ambao walionyesha uwezo mkubwa katika kutumikia Taifa.
“Mheshimiwa Spika Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hadi sasa ndiyo inayotuongoza haikusema vigezovya uteuzi wa Waziri Mkuu bali imetoa mamlaka ya uteuzi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,” alisema Waziri Aboud.
Hata hivyo, aliwaeleeza Wawakilishi kuwa Zanzibar haijawahi kutoa nafasi ya Spika wa Bunge wala Naibu wake, lakini wabunge kutoka Zanzibar na Tanzania wote wanahaki sawakugombea nafasi hiyo.
Waziri Aboud alisema kwamba serikali imeamua kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba ya Muungano kwa malengo ya kuondoa kero za muungano na kuwataka wananchi kupitia mabaraza ya katiba na Bunge kutumia nafasi hiyo ili kufanikisha kupata katiba mpya.
CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom