Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,180
- 664
`SMZ rudisheni hati za kusafiria`
2008-06-28 11:23:00
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imeshauriwa kurejesha matumizi ya hati za usafiri kati ya Tanzania Visiwani na Tanzania Bara ili kuepusha ongezeko la wimbi la uhalifu na kuenea kwa Ukimwi visiwani humo.
Ushauri huo ulitolewa jana na Mwakilishi wa Viti Maalum (CUF), Bi. Zakia Omar alipokuwa akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha, aliyowasilisha katika Baraza la Wawakilishi, Alhamisi iliopita.
Alisema kuondolewa kwa matumizi ya hati hizo za kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa pande hizi mbili za Jamhuri ya Muungano kumesababisha wimbi la uhalifu Zanzibar katika siku za karibuni.
Alisema pamoja na kuongezeka uhalifu, kama wizi wa kutumia silaha, vile vile kumechangia ongezeko la maambukizi ya Ukimwi kwa vile watu wanaingia kiholela na kuishi hapa bila ya kupimwa afya zao.
``Kisiwa chetu ni kidogo. Ushauri wangu ni kwa utaratibu wa kutumia hati za kusafiri urejeshwe. Unapokutana na watu watano huwezi kutofautisha yupi ni Mkenya na nani ni Banyamulenge,`` aliongeza.
Mwakilishi huyo alisema pamoja na kurejeshwa kwa matumizi ya hati za usafiri ni vizri kwa serikali ikafikiria kuanzisha utaratibu wa kupima afya za watu wanaoingia Zanzibar mara wanapofika katika viwanja vya ndege na bandarini.
Alisema wale watakobainika kuwa wanaishi na virusi wa Ukimwi warejeshwe wanakotoka ili kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa huo visiwani hapa.
Alisema huenda Zanzibar ikalalamikiwa kwa kufanya hivyo, lakini zipo nchi ambazo zinatumia utaratibu huo na matokeo yake maambukizi ya maradhi ya Ukimwi yameweza kudhibitiwa kwa kiasi fulani.
Bi. Zakia alisema zamani ukisikia kelele za mwizi, mwizi, basi mmoja alikuwa akijua kwamba mwizi huyo ameiba kuku, lakini wizi wa siku hizi ni wa majambazi wanaofyatua risasi na kuua watu na kupora fedha na mali.
Aliielezea Zanzibar kama nchi yenye hali ya kusikitisha pale vijana wengi wanapoonekana wakiwa wameathirika na matumizi ya dawa za kulevya.
Alipowasilisha bajeti yake, Waziri kiongozi alisema Zanzibar hivi sasa ina jumla ya watu wapatao 10,000 wanaoishi na virusi vya Ukimwi.
SOURCE: Nipashe
Tuma Maoni Yako