SMZ: Kura za maoni zitafana hata bila wahisani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMZ: Kura za maoni zitafana hata bila wahisani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 8, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), imesema itahakikisha kuwa kura ya maoni na uchaguzi mkuu,zinafanyika hata bila ya fedha za wahisani.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk Mwinyihaji Makame Mwadini, alipokuwa akitoa muhtasari wa bajeti ya mwaka wa fedha wa 2010/2011, inayotarajiwa kusomwa kesho, mjini Zanzibar.

  Dk Mwinyihaji alisema mafaniko ya kura ya maoni na uchaguzi ni miongoni mwa mipango ya serikali katika mwaka ujao wa fedha, lengo likiwa ni kujenga demokrasia ya kweli na utawala bora, ndani ya Zanzibar.

  "Tumejiandaa hata kama wafadhili watachelewesha au kutotoa misaada kwetu. Ujenzi wa demokrasia ni vitu muhimu katika maendeleo ya nchi, natoa wito kwa watu wote, mashirika ya umma na ya taasisi binafsi kusaidia harakati hizi za kujenga taifa," alisema waziri huyo bila kutaja kiwango cha fedha kinachohitajika kwa shughuli hizo.

  Akielezea mwelekeo wa bajeti ya serikali katika mwaka wa fedha wa 2010/11, Dk Mwinyihaji alisema hali ya uchumi katika mwaka ujao wa fedha, inatarajiwa kuimarika zaidi kwa kuzingatia maeneo yaliopewa kipeumbele.

  Alitaja maeneo ambayo yamepewa kipaumbele katika bajeti hiyo kuwa ni pamoja na kuimarisha huduma za afya ya jamii, elimu na ujenzi wa makazi bora.

  Kuhusu shughuli zilizopewa kipaumbele katika kuimarisha uchumi, ni pamoja na sekta ya utalii, kilimo cha kisasa, kuimarisha ujasiriamali, miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege.

  Waziri huyo pia alisema katika bajeti ya mwaka ujao, serikali ya CCM itathmini mafanikio yaliofikiwa katika utekelezaji wa sera zake katika kuimarisha uchumi na mapambano dhidi ya umasikini.

  Alisema katika mwaka wa fedha unaomalizika Zanzibar, imepiga hatua kubwa za kimaendeleo kutokana na mageuzi katika sekta ya kilimo, kuongezeka kwa idadi ya watalii wanaoingia nchini kutoka 128,445 mwaka 2008 hadi kufikia watalii 134,954 mwaka jana.

  SMZ: Kura za maoni zitafana hata bila wahisani
   
Loading...