Smz kupunguza gharama za ujenzi wa banadari mpya kwampigaduri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Smz kupunguza gharama za ujenzi wa banadari mpya kwampigaduri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 28, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Wizara ya mawasiliano na miundo mbinu imesema inatafuta njia mbadala za kukwepa gharama kubwa za ujenzi wa bandlari mpya eneo la Mpigaduri zinazofikia dola za Marekani milioni 800.
  Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi naibu waziri wa wizara hiyo Issa Haji Gavu amesema gharama hizo zilizopenekezwa na kampni ya ujenzi ya CRB kutoka China ni kubwa, hivyo serikali inaendelea kutafuta njia za kupata unafuu zaidi.
  Amesema katika kipindi cha miaka mitano iliyopita wizara ilikisia ujenzi wa maradi huo utagharimu dola za Marekai milioni 400 ambapo kwa sasa ulihitaji ongezeko la asilimia 10 sawa na dola milioni 500.
  Hata hivyo Gavu amesema wizara imeshakamilisha upembuzi yakinifu wa ujenzi wa bandari hiyo uliofanywa na kampuni ya CRB na hatua za ujenzi zitaanza mara baada ya fedha kupatikana.
  Aidha Gavu amesema fedha za ujenzi wa mradi huo zitatokana na mikopo au misaada kutoka kwa wahisani.
  Ujenzi wa bandari hiyo utakaojengwa kwa awamu tofauti itakauwa na uwezo wa kufunga gati meli tano kwa wakati mmoja, lakini awamu ya kwanza utaanza na ufungaji wa meli tatu.
   
Loading...