Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,266
Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua za kisheria wanasiasa ambao wanahubiri vurugu na fujo na kuwahamasisha wananchi uvunjifu wa amani kisiwani zanzibar.
Kauli hiyo nzito ya Serikali imetolewa na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa pili wa Rais Mh Mohamed Aboud wakati akizungumza na askari wa jeshi la polisi akifunga mafunzo ya uongozi mdogo wa cheo cha Ukoplo na Sajenti yaliyofanyika katika viwanja vya polisi messi hapa zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wastaafu wa jeshi hilo na wananchi.
Amesema zanzibar imepania kuwa kisiwa cha amani lakini wako wanasiasa wanataka kuharibu amani hiyo hivyo amelitaka jeshi la polisi kutoacha kuchukua hatua za kisheria kupinga kwa nguvu zote vitendo hivyo.
Katika mafunzo hayo ya miezi mhe Mohamed Aboud aliwatunuku vyeti na kuwavisha askari waliomaliza kozi hiyo ya ukoplo na sajenti huku katika mafunzo hayo jumla ya askari walioshiriki mafunzo hayo na waliomaliza.
Naye Kamishna wa polisi Zanzibar CP Hamdan Omar Makame amewataka wahitimu hao kuingia uraiani kwa kutekeleza mafunzo waliyoyapata na kuweka heshima kubwa ya jeshi hilo katika kuwatumikia wananchi kwa hoja za kisheria na kuepukana na vitendo vya rushwa na ubaguzi.
Chanzo :ITV channel.