SMS za chagua CCM: Je hii haivunji haki ya "privacy?" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SMS za chagua CCM: Je hii haivunji haki ya "privacy?"

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MILKYWAY GALAXY, Oct 15, 2010.

 1. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  :A S angry::A S angry::A S angry:
  Ndugu zangu,

  Nimepokea sasa hivi SMS isemayo:

  "Vyama vya siasa vilivyoandikishawa nchini Tanzania ni 18 lakini hakuna hata chama kimoja ukiviweka kwenye mizani kitakachofikia CCM. Chagua CCM, Chagua KIKWETE".

  Je huku sio kuingilia faragha ya mtu?

  Je hii ni haki?

  Je makampuni ya simu za mkononi ni agenti wa CCM?

  Imenikera sana.
   
 2. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Daaaah haya makampuni ya simu na TCRA inabidi waweke mikakati madhubuti ya kudhibiti hali hii, huu ni uhuni na sioni maan ya kusajili namba hpa kama mtu anaweza kuaccess namba yako na kukutumia ujumbe.Huu ni UPUMBAVU mtupu na kitu cha kukemewa kabisaaaaaa. Pole kaka hii ndio bongo na CCM ndio CHAMA CHA MAJAMBAZI.
   
 3. asam.thegunner

  asam.thegunner Member

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi sioni tatizo la hiyo sms. Ni ccm ndio wenyewe wanavyoona kwa kutumia vigezo vyao. sasa kama sio kweli basi vyama vingine vitoe majibu ya hiyo sms. Kumbuka lengo la chama chochote cha siasa ni kuingia ikulu kwa hiyo kila anayetumiwa hiyo sms atapima ukweli wa hiyo sms. Tutalalamika hadi lini jamani?
   
 4. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Vodacom (ya Rostam), ndio wanafanya huu upuuzi wa kutoa namba za wateja wao kwa hawa mahaini...
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Tunacholalamikia ni utaratibu; sms zinakuja kiharamu kwa kutumia codes tofauti zikionyesha za nje wakati si kweli.hapa watu wanajadili integrity ya katika kusambaza sms kwa kampuni husika.Hatuwezi kukaa kimya wakati sheria zinavunja hapa tunajaribu kupaza sauti ili hizo irregulalities zisirudiwe, kumbuka leo ni sms za kisiasa kesho zikitoka za kighaidi utasema nini?? Tunachosema mamalaka husika zitoe tamko ili hali hiyo iachwe.
  Labda nikukumbushe kule MAREKANI SIKU MBILI KABLA OSAMA HAJAFANYA MAMBO zilikuwa zinatoka sms zilisema "there will a big match in America tommorrow cha ajabu CIA walifanya-ku-ignore yaliyowapata kesho yake hawatasahau.So we are trying to waken up the system so they should take the necessary preventions than waiting for cure.

  Ni hayo tu
   
 6. MANI

  MANI Platinum Member

  #6
  Oct 16, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,412
  Likes Received: 1,871
  Trophy Points: 280
  "Vyama vya siasa vilivyoandikishawa nchini Tanzania ni 18 lakini hakuna hata chama kimoja ukiviweka kwenye mizani kitakachofikia CCM. Chagua CCM, Chagua KIKWETE".

  Ni kweli MG kwani wakati vyama vingine vinapiga vita ufisadi wao wanakumbatia, Wenzao wanasema huduma za jamii zinaweza kutolewa bure wao wanasema haiwezekani,Wenzao wanasema umasikini wetu ni matumizi mabaya ya rasilimali na fedha za umma wao kupitia mwenyekiti wao anasema hata hajui kwa nini tu masikini. Kwa hiyo ni wajibu wetu kuwatosa kwa kuangalia hayo hapo juu wao wanaona wana jijenga kumbe ndio wanaharibu.
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Oct 16, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  ooh nimekuelewa basi ni kweli!!
   
 8. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  MKUU, punguza jazba basi manake kauli za aina hii ndizo zinazowatisha watu!! Mbona SMS na email sawa na hizo watu tulikuwa tunazipokea zikitutaka tuipigie kura CHADEMA na kwamba CCM ni chama cha mafisadi?! Waungwana tulizipotezea tena hata bila ya kuwakashifu wale waliotufowadia!!!
   
 9. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi naona siyo sawa mimi kutumia ujumbe kutoka ccm wakati sijawahi kuiandikisha simu yangu kwao. Napinga sana utapeli waliotufanyia TCRA wa kutulaghai kuwa lazima simu zote zisajiliwe kumbe wanataka tuwape habari zetu ili watutibue nyongo.

  Akina sisi hatuliweki neno uungwana kwenye sentensi moja na neno ccm isipokuwa linapokuwa limetanguliwa na maneno hakuna, siyo, au mengine ya aina hiyo, mtu akinitumia ujumbe unaosifia ccm au kitu kinachohusiana na ccm najua mtu huyo si muungwana na hastahili heshima
   
 10. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #10
  Oct 16, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Issue sio content ya meseji, isipokuwa mdau analalamika iweje mtu apate namba yako na kukutumia meseji bila ridhaa yako! CCM au mtu anayeishabikia CCM atakuwa amefanya huo ugaidi kwa kushirikiana na kampuni ya simu husika, kitu ambacho kinatishia privacy ya watumiaji wa simu nchini.
   
Loading...