Elections 2010 SMS ya Maandamano nchi Nzima Ijumaa Imeanza

ChingaMzalendo

Senior Member
Nov 9, 2008
192
3
Kuna SMS ya maandamano nchi nzima kuanzia ijumaa amabyao inasambaa kwa kasi mno. Ujumbe wenyewe unasema "Tumeujumiwa miaka 45 imetosha. Kuanzia ijumaa ni maadandamano ya amani nchi nzima" Nawaunga mkono waandamanaji kwa maana ni haki yao ya msingi kuandamana, kwani kikwete na makamba wamezidi kuvuruga amani yetu. Tumefika mwisho wa uvumilivu na serikali yake ya kidhalimu na kiusultani

Kwa maana hiyo, ikiwa damu itamwagika, basi tume ya uchaguzi, Kikwete, Makamba na wengio wabebe mzigo. Wao ndio wanaoanza kuivuruga amani yetu na utulivu wetu kwa kuivamia haki yetu ya msingi. Kupiga kura.
 
Ni wazo zuri kwani panapokuwa na dhuluma ni lazima watu wapinge kwa nguvu zote. Dr. Martin Luther King Jr., alisema "dhuluma popote ni dhuluma pote". Hatuwezi kuongozwa na Tume ambayo kiongozi wake anaendelea kuwepo kwa ajili ya maslahi ya wale waliomteua. Niliwaandikieni kuwa mwaka 2005 katiba ya nchi ilibadilishwa ili kumfanya Makame aendelee kuiongoza baada ya kustaafu kazi ya Ujaji wa Mahakama ya Rufani. Na kwa kweli amefanya kazi hiyo kwa manufaa ya CCM bila aibu.
 
Tutafakari zaidi, nani anatuma SMS isije kuwa Tunampa Mbu kazi ya Kutibu Maralia?
 
message hiyo ni ya kichochezi na haitofautiani na za akina shamte au yoyote ile tuliyokua tunailaani

watanzania tutambue kuwa utu wetu ni zaidi ya momentarily emotions zinazozunguka vichwani mwetu.... miaka mitano si mingi na kwa subira ushindi waweza patikana

nashauri tuache upuuzi huo, tujiunge wote wapinzani na wapenda maendeleo ya nchi

binafsi jumapili ntajiunga rasmi kujiandaa na 2015... sihitaji kupoteza ndugu, rafiki, mke, au watoto wangu kwasababu inayoweza kusubiri

damusi bei rahisi kama inavyotamkwa, ukifa hurudi tena lakini ukisubiri utaona kesho

time heals
 
Ni haki ya kikatiba kufanya maandamano,polisi wanawajibu wa kulinda usalama,ole wao wajaribu kuzuia hapo ndipo matatizo yatakapotokea.
 
Tuwasubiri viongozi wenyewe waseme, unahakika gani kama hii SMS haijatoka kule FINLAND??
 
Siungi mkono tutafute jinsi ya kuelimisha watu wetu wajitokeze kupiga kura kama ni watu mia basi wote mia wapige kura
 
message hiyo ni ya kichochezi na haitofautiani na za akina shamte au yoyote ile tuliyokua tunailaani

watanzania tutambue kuwa utu wetu ni zaidi ya momentarily emotions zinazozunguka vichwani mwetu.... miaka mitano si mingi na kwa subira ushindi waweza patikana

nashauri tuache upuuzi huo, tujiunge wote wapinzani na wapenda maendeleo ya nchi

binafsi jumapili ntajiunga rasmi kujiandaa na 2015... sihitaji kupoteza ndugu, rafiki, mke, au watoto wangu kwasababu inayoweza kusubiri

damusi bei rahisi kama inavyotamkwa, ukifa hurudi tena lakini ukisubiri utaona kesho

time heals

Kwa hiyo unategemea 2015 mambo yatabadilika siyo??? Wenzako kazi ni mbele kwa mbele, come 2015 hata hivyo viti vya ubunge vitapunguzwa tena!!
 
message hiyo ni ya kichochezi na haitofautiani na za akina shamte au yoyote ile tuliyokua tunailaani

watanzania tutambue kuwa utu wetu ni zaidi ya momentarily emotions zinazozunguka vichwani mwetu.... Miaka mitano si mingi na kwa subira ushindi waweza patikana

nashauri tuache upuuzi huo, tujiunge wote wapinzani na wapenda maendeleo ya nchi

binafsi jumapili ntajiunga rasmi kujiandaa na 2015... Sihitaji kupoteza ndugu, rafiki, mke, au watoto wangu kwasababu inayoweza kusubiri

damusi bei rahisi kama inavyotamkwa, ukifa hurudi tena lakini ukisubiri utaona kesho

time heals

thank you acid.
 
Hii ni njia ya kuichafua CHADEMA.

Hizo msg ni planted tu,, kama zile za kipindi cha kampeni.
 
sawa kabisa maandamano yaje, ccm imemwaga mboga wananchi kuanzia ijumaa tunamwaga ugali, mbwai mbwai bwana, tumechoka ala! nasisitiza: Ni bora nife nimesimama kuliko kuendelea kuishi huku nimepiga magoti.
 
Kwa hiyo unategemea 2015 mambo yatabadilika siyo??? Wenzako kazi ni mbele kwa mbele, come 2015 hata hivyo viti vya ubunge vitapunguzwa tena!!
mkuu nielewe kidogo tu

1995 - hatukua hata na avenue za kujua kieneleacho, nakumbuka ya mrema na dar, tulirudia uchaguzi wote mkoa huu wa dar
2000 - tulianza kugundua hayo lakini sauti haikua kubwa
2005 - walicheza mapema na kila kitu kikawa offside
2010 - tunayajua haya kwani hata walio ndani ya CCM hawapendezwi
2015 - kila sehemu itakua imefikiwa, lazima ukubali coverage ya chadema haikuzidi 50% na hata huko ukerewe waliposhinda ni nguvu ya upepo wa mwanza na hulka ya watani zangu

upepo huu ni mkubwa sana na hauzimiki tena, CCM wanajua na utasiki 2012 watavyosambaratika... na ili kutumia opportunity hiyo basi cha maana ni kutulia

kumbuka ukiandamana wewe, wataokufa ni wanawake na watoto, na wana haki ya kuishi

siungi mkono jitihada zote za kuvunja amani kwani naamini with or without siasa tanzania ipo
 
Ebwana eehee? Hata kama meseji ni planted inachozungumza ni chaukweli na ni wajibu wa kira anaeona ameibiwa kuandamana hyo ijumaa, cjui itakuwa sangapi?
 
Adanganywe atoke m2,hapo mtajuwa kweli FFU wapo ajili yawakorofi kama nyie,mcdhani hapa ni Kenya,ila mjue vyombo vya dola vimejipanga,mpinzani akiona kashindwa hujitweka uwana mapinduzi,muambieni SLAA Afanye mapinduzi kwake nyumbani the Karatu,sio kukimbilia madaraka akadhani tunataka tawaliwa na KANISA,Nyepesi nikuwa kampeni za CHADEMA Zinadhaminiwa na Kanisa la America,tena la mahanith and Roma,vip Tz itawaliwe na mfwasi wa mahanithi

NYambafu!!! Hatutaki udini kwenye jamvi la Great Thinkers!!! Hatutaki damu imwegikwe; I am sure message sent to them!!! Let us implement Plan B!!!
 
Ivi maandamano manake fujo?
Kuna watu umu kama ingekuwa paper washaferi kushiliki kwenye maandamano ya amani sio tatizo jamani.
Tz kwa uoga mpaka mnakera.
Kama ni tamko toka CHADEMA tuko pamoja
 
Kwa maana hiyo, ikiwa damu itamwagika, basi tume ya uchaguzi, Kikwete, Makamba na wengio wabebe mzigo. Wao ndio wanaoanza kuivuruga amani yetu na utulivu wetu kwa kuivamia haki yetu ya msingi. Kupiga kura.
Twendeni polepole tunaandamana kwa sababu ipi......na maandamano ya amani ya kushinikiza nini?

Chadema wanatakiwa watoe takwimu za kututhibitishia kwanza ni nani kashinda chaguzi hizi kabla ya kuandamana......vinginevyo tunaandamana kwa sababu zipi?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom