SMS tu zingetosha kuokoa uwaziri wa Mathayo, Kagasheki, Nchimbi na Nahodha!

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Teknolojia ya habari na mawasiliano kwa kaisi kikubwa imeleta changamoto za haraka kwenye siasa za Tanzania. Sio siri tena, watendaji wa serikali "wanapelekwa" na upepo wa kwenye mitandao, huu wa JF ukiwa namba moja.

Kinachonishangaza ni pale mawaziri na watendaji wengine wanaposhindwa kutumia faida ya maendeleo ya sekta ya mawasiliano kurahisisha kazi zao.

Mathalani, mawaziri hawa wanne, pamoja na akina Chiza (ambaye hakutafuta suluhu katika mizani ya kuuzia mahindi!), wangeepuka fedheha hii kama wangeanzisha mawasiliano ya MOJA KWA MOJA na wananchi.

Najua kupokea simu za watanzania wote wenye matatizo ni ngumu. Lakini kwa nini kila waziri asitoe, na kuitangaza namba ya simu ambayo kila mwananchi mwenye kero au tatizo la dharura anatuma sms? Namba hiyo ikiunganishwa kwenye iPad ya waziri, na waziri akajipa kautaratibu ka kusoma msg kwa dakika 60 kila siku (tena anaweza kufanya hili hata akiwa safarini), huu uzembe wa kipuuzi puuzi usingetokea.

Kwa mfano operesheni tokomeza ujangili ilitekelezwa kwa zaidi ya siku 25, ni wazi kwamba mawaziri husika wangekuwa wa mwanzo kupata kilio cha wananchi, na kwa haraka sana wangeingilia kati na kuhakikisha yale mapungufu yanarekebishwa.

Sasa mawaziri mnategemea wasaidizi wenu na JF kutapa updates. Sio vibaya lakini mjue kwamba humu JF wengi wetu ni watu wa level ya kati ya maisha na tukaa mijini. Itakuwa ngumu sana kupata zile taarifa za kule ndani kabisa kwa wakati. Mitandao ya simu imeendea hadi vijijini siku hizi. Anzisheni mawasiliano ya moja kwa moja na wananchi sasa kwa kutumia simu za mikononi, mtaweza kudeal kiurahisi zaidi na changamoto zinazozikumba wizara zenu.

MSIWAAMINI, na narudia tena, msiwaamini wasaidi wenu. Wengi wao tuko nao huku mjini, wako bize wanasimamia biashara zao za mabasi, malori, maduka, mahoteli na mabaa... Ripoti nyingi wanazowapa kwenye mikutano ya hapo wizarani ni za uongo.


Ingawa wengine ni wapinzani lakini sio vibaya tukawashauri, maana tumechoka kila siku baraza jipya la mawaziri. Nchi itaendelezwa saa ngapi?...
 

vyuku

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
501
225
Kufukuzwa haitoshi mi nilitaka washtakiwe pia,wanajiskia sana na dharau kibao,hasa huyo shamsi.
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Ukiangalia mtu kama Lyatonga, enzi zake japokuwa simu za mikononi hazikuwa zimeenea, lakini alitumia mbinu tofauti kupata taarifa moja kwa moja kutoka kwa wananchi, na hiyo ilimuwezesha kutenda kazi zake kwa ufanisi mkubwa...
 

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
13,689
2,000
... na waziri akajipa kautaratibu ka kusoma msg kwa dakika 60 kila siku (tena anaweza kufanya hili hata akiwa safarini), huu uzembe wa kipuuzi puuzi usingetokea. ...
Yeah, badala ya kusinzia kwenye VX, muda huo autumie kupitia sms!
 

Bob G

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
2,352
1,500
Akili hio kwa mawaziri wetu haiko, wako bize na ufisadi na kupanga mikakati ya kitoto ya kuimaliza CDM
 

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,100
1,195
ila nchimbi wanga na majibu ya nyodo na dharau sanaaaaaaa, mungu amempa staili yake.
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Akili hio kwa mawaziri wetu haiko, wako bize na ufisadi na kupanga mikakati ya kitoto ya kuimaliza CDM

Mawaziri wanajifanya miungu watu. Wanafunga vioo vya ma vx yao na ukienda ofisini umuone utaonekana uchafu. Lakini yakiwakuta wanaanza kulialia. ..
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
ila nchimbi wanga na majibu ya nyodo na dharau sanaaaaaaa, mungu amempa staili yake.

Juzi wakati anasema kwa dharau kuwa serikali haina mpango wa kuunda tume ya kuchunguza bomu la Soweto alikuwa anajiona mkubwa kama malaika...
 

Bulesi

JF-Expert Member
May 14, 2008
8,741
2,000
Hawa mawaziri wa magamba ni vimeo kwani hawajui jinsi ya kurahisisha kazi zao kwa kutumia tekinolojia!! Tibaijuka kwa mfano hata ukimpelekea e-mail hajibu sasa sijui hiyo e-mail yake ni ya kazi gani!!! KUFANYA KAZI KWAKE U.N. HAKUJAMSAIDIA KUWA RELATIVELY MORE EFFICIENT KULIKO WENZIE AMBAO HAWANA EXPOSURE KAMA WAKINA kOMBANI/gHASIA!!!
 

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Hawa mawaziri wa magamba ni vimeo kwani hawajui jinsi ya kurahisisha kazi zao kwa kutumia tekinolojia!! Tibaijuka kwa mfano hata ukimpelekea e-mail hajibu sasa sijui hiyo e-mail yake ni ya kazi gani!!! KUFANYA KAZI KWAKE U.N. HAKUJAMSAIDIA KUWA RELATIVELY MORE EFFICIENT KULIKO WENZIE AMBAO HAWANA EXPOSURE KAMA WAKINA kOMBANI/gHASIA!!!

Anasubiri yamfike akaanze kulia bungeni...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom