Smg (abunge) za chadema waanza kazi waliyotumwa na wananchi

DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
57
WALK THE TALK ALWAYS -
1. Kama walivyotekeleza kilio cha wananchi pale mjengoni kwa kumpa feedback mwenyekiti wa ccm Taifa, Hon.Kikwete kwamba hakufurahishwa na udikiteta uliotekelezwa na nec na usalama wa Taifa na hivyo kuhitaji forum ya katiba mpya, tume huru (NEC) na tume huru kuchunguza kasoro nzito za mchakato wa uchaguzi na kuicha nchi nzima ikitisika ikiwa ni pamoja na wasio na akili kulaani hatua ya MEJEMADALI wa wananchi. Kazi ya MAJEMADALI hao inaendelea ikiwa ni pamoja na kuhakikisha virusi vya ccm havipewi nafasi.

2. MAKAMANDA hao wamevamia majimbo yao na kuanza kazi kwenda mbele mfano ni mpiganaji Tundu Lissu ametoa elimu ya uraia kwa wananchi kwamba sheria ya kuwatosha ushuru walalahoi kodi za mazao ya misitu ilishafutwa tangu mwaka 2002 na hivyo kuweka vizuizi na kuendelea kuwatoza watanzania huku mabilioni yakipoytea kwenye magogo na vitaru vya uwindaji ni kuwanyonya na kuwanyanyasa wananchi maskini nchini mwao-kutokana na elimu hiyo ya uraia wananchi wa singida wameng'oa vizuizi vilivyoweka kwa malengo hayo, nakwambia moto utawaka.

3. Wapiganaji Wenje na Hynes(Mwanza) Lema(Arusha) waliong'oa mizimu na mizinga ya ccm wapo kwenye mchakato wa kumpata meya wa jiji la mwanza kwa lengo la kutekeleza ilani ya chadema jijini mwanza na arusha -hii itakuwa mifano ya majiji yanayoongozwa na chadema -elimu bure, afya bure na miundombinu, na vita dhidi ya ufisadi ni vipa umbele walivyoweka mbele kuvishugulikia kazi mdundo.

4. Wapiganaji wengine wote wako wanamalizia workplans zao na kuzisubmit kwa kiongozi Dr.Slaa amabae atakuwa anamonitor utendaji kwa kuwa na one on ones on monthly basis, quarterly review na mid year review, nakwambia moto si mchezo vijana wamesukwa na wanaenda kulipua mabomu mjengo utawaka moto.

Hongera CHADEMA, hongera Dr.Slaa, Hongera CC CHADEMA, hongera kiungo mchezeshaji baba mbowe -vita ni vita mura
 
Umemsahau yule wa Mbulu tayari anaendesha semina kwa madiwani wateuli
 
Habari from people from Mwanza ni Kwamba Wenje ameingia Mwanza Tuko Juzi na kukuta mgawo wa umeme usioeleweka..... Mgao wa bila kutangaziwa, jamaa zangu wasema aliwahoji hawa Tanesco, na kuwaambia kama ni mgao inabidi wawatangazie wananchi. Wanasema Thank god from jana anagalao wanapata umeme
 
Nakwambia hawa ni makamanda wa vita wera wera moto unawaka halima mdeee kisha vamia mabarabara ya vichochoro anawaunganisha wananchi barabara zinachongwa sasa nakwambia mambo ni mdundo wera wera nakwambia
 
Mwenye contacts za wenje tafadhari... tushirikiane kuijenga nyamagana kimawazo kama wenzetu wa ubungo na mnyika, pia mlio karibu na wabunge wa chadema wahimizeni wote kujiunga mitandaoni muwaeleze kuwa hii ndio silaha yetu kuu chadema na njia mbadala ya kupunguza matumizi yanayo epukika (usafiri)
 
mweee.hivi kwa nini uchaguzi tusiwe tunafanya kila mwaka? au NEC wabadili utaratibu tuwe tunafanya uchaguzi kwa semester
 
Naomba kufahamishwe, wamepata fungu wapi wakati bajeti ya serikali itapangwa June 2011? Swali lanyongeza, kila jimbo moja huunda halmashauri? Mfano, Kawe
 
Nafikiri hili Mtanzania aka Mwakalinga alishawahi kulisema mara nyingi sana.

Halmashauri za Wilaya/Majimbo hupewa hela nyingi sana. Kyela kwa mfano hupewa kama bilioni 20+.

Huko analalamika kuwa ndiko kuna ulaji mkubwa sana na EPA ni cha mtoto.

Inatosha tu kufuatilia hela zilizopo kwenye halmashauri basi wanaweza kufanya maajabu.
Naomba kufahamishwe, wamepata fungu wapi wakati bajeti ya serikali itapangwa June 2011? Swali lanyongeza, kila jimbo moja huunda halmashauri? Mfano, Kawe
 
duh hilo la umeme linakera sana , hata hapa nipo gizani wk ya pili sasa tunakatiwa umeme saa 12 jioni mpk asubuhi
 
Hakuna kulala, vijana chapeni kazi ili wananchi waone thamani ya kura zao walizowapa na wale ambao hawakuwapa wajute kuwapigia wezi wa CCM. Jengeni imani kwa wapiga kura wenu, wafahamisheni haki zao , nimefurahi kwa alichofanya Tindu Lisu, maana ni sawa na kumkamua panya huku ng'ombe aliyenona maziwa yake yanaachwa yakipotea ovyo.
 
Naomba kufahamishwe, wamepata fungu wapi wakati bajeti ya serikali itapangwa June 2011? Swali lanyongeza, kila jimbo moja huunda halmashauri? Mfano, Kawe
Budget ipo ya mwaka huu,ilishapitishwa last july. Watakachofanya ni kubadilisha vipaumbele tu. Ccm vipaumbele huwa ni kupeana ulaji kwanza ndo sbb wanataka kunyonyana macho kwenye umeya! Kawe haiwezi kuwa halmashauri peke yake ipo pamoja na ubungo na kinondoni zikiunda manispaa ya kinondoni. Kawe peke yake ina mgawo wa billion 4 kwa mwaka za barabara za vichochoroni na ndiyo ameanza nazo mh Mdee,mbona watakoma this time!
 
Kuna hela nyingi kwenye halmashauri kuanzia kodi mbalimbali wanazokusanya wenyewe hadi ile ruzuku inayotoka serikali kuu. Kweli Katika halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA, onyesheni mifano na isiwe hapa mwanzoni tu bali wakati wote. Muulizeni Dr. Slaa kule Karatu alikuwa anafanyaje? Huko kila kitu kilienda kama kilivyopangwa na ndiyo maana tukataka utekelezaji huo aulete ngazi ya Taifa. Tunataka uchaguzi ujao kila mtu aseme niichague CHADEMA ili niwe kama halmashauri fulani. MSITUANGUSHE.
Nakubaliana na wazo la wabunge wote wa CHADEMA na MADIWANI wote wajiunge katika mtandao huu wa JF, kwani humu tutawaeleza ukweli wote - mazuri yao na mabaya yao pia ili wawe wanayarekebisha kabla ya ngwe inayofuata.
 
Wakati hayo yakifanywa na Wabunge wa CHADEMA, wale wa chama kileee wanaendelea na matafrija ya kujipongeza hadi baada ya X-mas kisha wataanza na kuandaa mpango wa kazi huku wakisubiri maelekezo ya jinsi ya kutekeleza sera za chama (hii inaweza kufika May 2011)kutoka kwa Katibu mkuu wao YM. Hakuna haja ya haraka sana kwa vile uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika 2014 hivyo hata kama kazi za maendeleo zikianza 2013 wananchi watawaona tuu. Wasiwasi wa nini na wao ndio Chama Twawala?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom