Mambo ya Kuzingatia Unaponunua Simu janja (Smartphone)

Goodrich

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
2,091
1,177
Simu ie smartphone, inaweza kuwa na jina kubwa au umbo zuri lakini ikakusumbua kutokana na uwezo mdogo ie uwezo usioendana na mahitaji yako.

Hivyo kuna mambo ya kuzingatia unaponunua simu ili ufurahie mawasiliano.

Vitu vya kuzingatia vipo vingi lakini vya muhimu ni:

1. RAM - Hii ni Random Access Memory ambayo ndio hasa ufanisi wa simu katika matumizi System Apps.
Ili imudu apps zilizopo sasa km vile Whatsapp, Fb, Viber, browsing apps etc, RAM isipungue 1 up to 4GB kutegemea na matumizi yako.

2. Internal Memory - Hapa ndio data na Apps zako zinahifadhiwa. Wingi wa Apps utahitaji IM kubwa. Vinginevyo utalazimika kuwa na apps chache. Internal Memory nzuri ni kuanzia 4-32GB.

3. Screen Resolution - Hii inakusaidia kuona picha na video kwa ubora zaidi. Hutegemea na mahitaji yako. Ni jambo la kuuliza pia unaponunua simu. Kuanzia 960x1200pixels ni nzuri.

Mambo mengineyo ya muhimu ni km vile Operating System (OS), Card Slots, Uwezo wa Camera, Android Version, Battery Talktime, Dimensions, etc etc
 
Hapo kwenye jina mkuu labda kama sielewi, lina umuhimu gani!

Kwani kuna baadhi ya simu majina yake hayajulikani sana lakini simu zao zina hizo specifications ulizotaja na zina perfom vizuri tu, mfano ni simu kama Viwa, Tecno, Itel nk.
 
Shukrani kwa kutupanua wigo wa uekewa! mkuu mi nina samsung galaxy lakini namna ya kuangalia Mambo uliyo yataja nashindwa. Hebu endelea kunipa msaada.
 
Hapo kwenye jina mkuu labda kama sielewi,lina umuhimu gani!Kwani kuna baadhi ya simu majina yake hayajulikani sana lakini simu zao zina hizo specifications ulizotaja na zina perfom vizuri tu,mfano ni simu kama Viwa,Tecno,Itel nk.

Hivi tukiacha ushabiki maandazi kuna tekno yoyote inaweza pafom vyema kuliko Htc? Tukitoa vigezo vya Mwandishi

Mfano phantom kunani yoyote dhidi ya Htc one M8?
 
Dogo kuna hii simu screen kubwa aina ya vodafone vodashop inauzwa laki na themanini, nijitose au ninunue huawei. Mbona TECNO hujaitaja inaaminika ?
 
Kusema kweli haipo ingawa H7 inajitahidi kiasi chake na ni cheap haizidi laki tatu

Mkuu ulichosema ni.kweli hawa tecno kila toleo mpya badala ya kuongeza ubora wanashusha hiyo H7 imezidiwa hata na toleo lililotangulia la P7
 
Asante hapo kwenye RAM umenifunza kitu mkuu, kuna simu nilitaka kuiacha simply ina RAM ya 1GB, kumbe nitainunua sasa

Ila nina swali kuhusiana na hizi Apps: hivi unavyokuwa nazo nyingi hazitumalizie hizi MB zetu za internet?? nikiwa namaanisha zinakuwa updated kila wakati mobile data inapokuwa ON
 
Shukrani kwa kutupanua wigo wa uekewa! mkuu mi nina samsung galaxy lakini namna ya kuangalia Mambo uliyo yataja nashindwa. Hebu endelea kunipa msaada.

Ok mkuu galaxy zipo nyingi ni aina gani?
 
Back
Top Bottom