Smart phones nyumba za ibada, no please!

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,704
Usasa una yake mazuri na ya kuchukiza. Ya nuruni na ya sirini. Yote hayakwepeki. Kuna moja lililo wazi. Hata kama hatutapenda kulijadili kwa unafiki na uzandiki wetu. MFUMO KRISTO UNATAWALA DUNIA.

Mwezi uliopita tulipata msiba mtaani kwetu. Jamaa yetu jirani (mlevi mzuri wa 'pure' namba one alipata ajali na kufariki hapohapo! Aligongwa na gari mitaa ya mbezi akitoka kutoa lock. Msiba ulikuwa na kila aina ya vituko kutokana na aina ya maisha aliyokuwa nayo marehemu na aina ya kampani yake. Hii sio kesi kabisa!
Alizikwa kwa imani yake ya Kiislam.

Ustaadh aliyeongoza ibada ile ya mazishi alikuwa kijana wa makamo lakini wa kileo sana. Pale makaburini aloliongoza ibada ile ya mazishi kupitia iPad kali aliyokuwa kabeba. Juzuu, mistari na utaratibu mzima wa mazishi yale, alitumia version ya mtandaoni kupitia iPad. Quran for Android ya mtandaoni.

Kuna wakati alipata usumbufu wa nadhani jumbe za WhatsApp na za kawaida na kama mara mbili alipigiwa simu alizokata ili uweze kuwa na mwendelezo wa ibada bila bughudha. iPad ile alitumia password kuifunga na kuifungua. Nikajiuliza Ustaadh anajua kweli maana ya password?

Imani yangu ni mkristo, huwa nasali makanisa tofauti.. Kuna baadhi ya makanisa, maaskofu, wachungaji na wahubiri wao huona ni sifa na usasa kutumia downloaded Bible toka kwenye simujanja zao na ipads kusoma neno na nukuu mbalimbali.

Nina ukakasi mkubwa kwenye hili. Tunaishi kwenye ulimwengu wa namba ya siri... 666. Namba ya MFUMO KRISTO mpinga KRISTO, lakini wengi wetu hatulitambui hilo.

Siku hizi makufuli na vitasa havina nguvu na thamani kivile. Maisha yetu yametawaliwa na namba ya siri kuanzia:

Mitandaoni
Huduma za kifedha
Huduma za bank
Huduma binafsi
Simu zetu
Anuani zetu
Manunuzi yetu
Miamala mbalimbali
Shughuli za kijamii
Shughuli za kidini nknk
Hata miamala na malipo mbalimbali serikalini yanakutambua kwa namba maalum ya mlipa kodi yenye namba ya siri.

Yote juu ya yote simu janja yako (smart phone) uliyo download msahafu kwa imani yako.. Unathubutu vipi kuitumia kwenye nyumba takatifu ya ibada!? Una
Jumbe za mapenzi
Una mapicha ya aibu
Una video za kutia kinyaa
Una calls na mapenzi uhasama na visasi
Una vitu vingi vinavyowakilisha ulimwengu wa giza, sahau nyimbo za mapenzi na Ujinga mwingine, michepuko hata ulozi... Unapata wapi uthubutu wa kuvichanganya hivi na msahafu unaoheshimika na kujaa utakatifu?

Hupaswi kulaumiwa kwakuwa hujui, wala Kiongozi wako wa dini hapaswi kulaumiwa kwakuwa hana uwezo wa kulizuia hili. Dunia inatawaliwa na namba ya siri... Ambayo ni 666. Namba ya mpinga KRISTO. Imo mpaka kwenye nyumba za ibada. Zaka na sadaka kwa tigo pesa, mpesa nknk.

Ikubali uishi, ikatae ufe. Namaanisha namba ya siri 666. Hata kondom zako 3 ni kiwakilishi cha namba ileile ya siri. Matumizi yake unajenga na kuimarisha madhabahu unayojaribu kuipinga. Utabaki kuwa mjinga.

Lala salama!

Jr
 
Usasa una yake mazuri na ya kuchukiza... Ya nuruni na ya sirini.. Yote hayakwepeki... Kuna moja lililo wazi...! Hata kama hatutapenda kulijadili kwa unafiki na unafiki wetu... MFUMO KRISTO UNATAWALA DUNIA....!
Mwezi uliopita tulipata msiba mtaani kwetu... Jamaa yetu jirani (mlevi mzuri wa 'pure' namba one alipata ajali na kufariki hapohapo!!! Aligongwa na gari mitaa ya mbezi akitoka kutoa lock... Msiba ulikuwa na kila aina ya vituko kutokana na aina ya maisha aliyokuwa nayo marehemu na aina ya kampani yake... Hii sio kesi kabisa!
Alizikwa kwa imani yake ya kiislam... Ustaadh aliyeongoza ibada ile ya mazishi alikuwa kijana wa makamo lakini wa kileo sana... Pale makaburini aloliongoza ibada ile ya mazishi kupitia iPad kali aliyokuwa kabeba... Juzuu, mistari na utaratibu mzima wa mazishi yale, alitumia version ya mtandaoni kupitia iPad.. Quran for Android ya mtandaoni
Kuna wakati alipata usumbufu wa nadhani jumbe za WhatsApp na za kawaida na kama mara mbili alipigiwa simu alizokata ili uweze kuwa na mwendelezo wa ibada bila bughudha... IPad ile alitumia password kuifunga na kuifungua... Nikajiuliza Ustaadh anajua kweli maana ya password?
Imani yangu ni mkristo, huwa nasali makanisa tofauti.. Kuna baadhi ya makanisa, maaskofu, wachungaji na wahubiri wao huona ni sifa na usasa kutumia downloaded Bible toka kwenye simujanja zao na ipads kusoma neno na nukuu mbalimbali
Nina ukakasi mkubwa kwenye hili... Tunaishi kwenye ulimwengu wa namba ya siri... 666... Namba ya MFUMO KRISTO mpinga KRISTO, lakini wengi wetu hatulitambui hilo...
Siku hizi makufuli na vitasa havina nguvu na thamani kivile... Maisha yetu yametawaliwa na namba ya siri kuanzia
Mitandaoni
Huduma za kifedha
Huduma za bank
Huduma binafsi
Simu zetu
Anuani zetu
Manunuzi yetu
Miamala mbalimbali
Shughuli za kijamii
Shughuli za kidini nknk
Hata miamala na malipo mbalimbali serikalini yanakutambua kwa namba maalum ya mlipa kodi yenye namba ya siri...
Yote juu ya yote simu janja yako (smart phone) uliyo download msahafu kwa imani yako.. Unathubutu vipi kuitumia kwenye nyumba takatifu ya ibada!? Una
Jumbe za mapenzi
Una mapicha ya aibu
Una video za kutia kinyaa
Una calls na mapenzi uhasama na visasi
Una vitu vingi vinavyowakilisha ulimwengu wa giza, sahau nyimbo za mapenzi na Ujinga mwingine, michepuko hata ulozi... Unapata wapi uthubutu wa kuvichanganya hivi na msahafu unaoheshimika na kujaa utakatifu!!?
Hupaswi kulaumiwa kwakuwa hujui...wala Kiongozi wako wa dini hapaswi kulaumiwa kwakuwa hana uwezo wa kulizuia hili.... Dunia inatawaliwa na namba ya siri... Ambayo ni 666.... Namba ya mpinga KRISTO.... Imo mpaka kwenye nyumba za ibada... Zaka na sadaka kwa tigo pesa, mpesa nknk....
Ikubali uishi... Ikatae ufe... Namaanisha namba ya siri 666... Hata kondom zako 3 ni kiwakilishi cha namba ileile ya siri... Matumizi yake unajenga na kuimarisha madhabahu unayojaribu kuipinga.... Utabaki kuwa mjinga....

Lala salama...!!!

Jr
Umenena Mshana Jr. Maneno yako ni ya kufikirisha.

Hakika tubadilike kuanzia viongozi wa dini na waumini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Limeeleweka somo.

Ila mimi simu yangu App zote ni takatifu so naruhusiwa kuweka "airplane mode" na kuingia nayo church ili niweze kutumia misahafu yangu ya kidigital?

N.b situmii password kuunlock simu.
 
Limeeleweka somo.

Ila mimi simu yangu App zote ni takatifu so naruhusiwa kuweka "airplane mode" na kuingia nayo church ili niweze kutumia misahafu yangu ya kidigital?

N.b situmii password kuunlock simu.
Uko sahihi, uko vizuri

Jr
 
Back
Top Bottom