Small scale beer production

shamamona

Member
Nov 9, 2015
35
8
Habari wadau wa JF..
Mimi ni mkulima wa kati wa mpunga (sio mkubwa sana wala mdogo sana). Kwa mwaka naingiza wastani wa gunia 1000 za mpunga. Huwa natenga kiasi kama gunia 10 kwa chakula cha familia na the rest nauza ktk miezi ya 12 na Januari pindi amabapo bei iko juu kiasi kwa maslahi zaidi. Kwa kipindi kirefu nimekua nikifikiria namna ya kuongeza thamani ya bidhaa yangu hii ya mpunga kabla ya kumfikia mteja wangu. Nimefanikiwa kwa kiasi flan kupata majibu lkn sio kwa 100%. Moja ya mambo nilifikiri kufanya ni





(1)Kujikita na utengenezaji wa vyakula mbalimbali kwa kutumia unga wa mchele mf(keki, etc) in a small scale home industry





(2) Kusafirisha nje ya nchi within east Africa kwa sbabu ya soko huria ingawa najua haliko kwa 100% by now.






(3) Beer crafting (utengenezaji wa bia) kwa kutumia mchele ambayo ni nzuri sana kiafya kuliko bia za kawaida. Nimejaribu kufanya research kidogo na kubaini kwamba inawezekana kutengeneza whats called (malted rice beer) ambayo kwa sasa inatengenezwa na (Spanish craft beer Institute in Spain). Siyo lazima kuanza kwa large scale production lkn unaweza kuanza na kiwanda kidogo kinachoweza kugharimu kama 50 millions only. nikijaribu kuangalia kwa haraka haraka ktk Tanzania yetu hakuna viwanda vidogo vya usindikaji wa bia zaidi ya viwanda vikubwa kama TBL na SBL. Naomba nieleweke ninapoongelea small scale beer production simaanishi local beer..
Mimi nimekua interested sana na uzalishaji wa bia kwa kuwa naona viwanda vidogo vya uzalishaji hakuna na kama vipo basi ni kidogo sana, kwa maana hiyo naweza nikapata faida nyingi kufanya uzalishaji ktk kiwango kidogo kama kupata interaction directly na customers wangu, management n.k ingawa najua large industries za bia hapa TZ ni kama monopoly kwa kua ziko kubwa chache.






Nimejaribu kuchanganua namna gani ntaanza na kukutana na changamoto nyingi kama






(1) elimu ya uzalishaji bia mimi sina kwa hiyo lazima ntahitaji mtu/watu waliobobea ktk secta iyo.(proffessionals) na siyo proffessionals tu watahitajika lkn lazima awe mwenye kujua/kubobea ktk aina iyo ya bia.






(2)market(soko) ukizingatia nafanya uzalishaji along those large firms..






Kama mdau wa hili jukwaa la ujasiriamali naomba ushauri wenu, hasa hasa kwa hizo changamoto hapo juu na changamoto zingine unazoweza kuzifahamu, Au ushauri wa namna gani naweza kuongeza thaman ktk hili zao la mpunga kuliko kila siku kuuza punje tu....

naomba kuwasilisha
 
Dah mkuu nimependa wewe unamtaji mkubwa sana kuliko hivyo ulivyonavyo sasa
 
Heshima kwako mkuu!!,wazo lako ni zuri sana,kiasi kwamba mimi ningekuwa na Mamlaka Watu km nyie dawa ni kuwawezesha kwa Mikopo yenye riba nafuu sana ili mzalishe zaidi ya kile mnachokitarajia kwani mnaongeza sana fursa za ajira hivyo kuipunguzia serikali mzigo.
 
fantastic idea. je hiyo bia itakuwa na kilevi? au kinywaji kikitwa bia lazima kiwe na kilevi.
 
Mkuu,
Kifupi nikwamba, rice beer itakua ni new product katika nchi yetu, watu walio bobea kwenye maswala ya marketing watakusaidia namna ya kufanya product penetration na mengine ya kufanana na hayo uweze kuuza.product yako.


Rice beer inawezekana kutengenezeka pale utakapo shirikiana na wataalamu, ndio kazi zetu.

Kama small scale producer, baadhi ya changamoto ninazoweza kukujuza kwa sasa ni pamoja na;

*Kuandaa team ya utafiti itayo weza kukubainishia excellent formula ya bidhaa yako,

*Kuwatembelea NEMC pamoja na OSHA kuhusu mahali unapo taka kufanyia uzalishaji wako,

*Ujenzi wa eneo lako la uzalishaji,
NB. Jengo la uzalishaji linatakiwa liwe la umbo la Herufi "L" au "I"


* Product and premises registration,

*TBS product certification


Changamoto zote hizoo zinatatulika. Kwa wepesi zaidi, unaweza pitia mwamvuli wa SIDO Utapunguza baadhi ya gharama.
 
Mkuu,
Kifupi nikwamba, rice beer itakua ni new product katika nchi yetu, watu walio bobea kwenye maswala ya marketing watakusaidia namna ya kufanya product penetration na mengine ya kufanana na hayo uweze kuuza.product yako.


Rice beer inawezekana kutengenezeka pale utakapo shirikiana na wataalamu, ndio kazi zetu.

Kama small scale producer, baadhi ya changamoto ninazoweza kukujuza kwa sasa ni pamoja na;

*Kuandaa team ya utafiti itayo weza kukubainishia excellent formula ya bidhaa yako,

*Kuwatembelea NEMC pamoja na OSHA kuhusu mahali unapo taka kufanyia uzalishaji wako,

*Ujenzi wa eneo lako la uzalishaji,
NB. Jengo la uzalishaji linatakiwa liwe la umbo la Herufi "L" au "I"


* Product and premises registration,

*TBS product certification


Changamoto zote hizoo zinatatulika. Kwa wepesi zaidi, unaweza pitia mwamvuli wa SIDO Utapunguza baadhi ya gharama.
Shukrani sana mkuu ubarikiwe...nathamini sana mchango wako
 
fantastic idea. je hiyo bia itakuwa na kilevi? au kinywaji kikitwa bia lazima kiwe na kilevi.

Yah kikiitwa bia lazima kiwe na kilevi. lakini kwa WINE siyo lazima iwe na kilevi na kwa kukupanua zaidi zipo pia wine zitokanazo na rice ambazo zina kilevi
 
Napenda kuwashukuru wadau wote waliojitolea muda wao kunipa support kwa mawazo yao hadi sasa ndani na nje ya JF. Mungu awabariki nyote.




lakini sina budi nirudi kwenu nikiomba kupata mawazo yenu kwenye mambo kama




(1) Roughly figures kwenye??? ni watu gani hasa wanaohusika na research ya formular ya bidhaa hii, muda ambao wanaweza kutumia kumaliza utafiti wao, costs ambazo zinaweza kutumika kufanya utafiti huu (at maximum.)



(2) Complications ambazo zinaeweza kutokea ktk shughuli nzima ya utafiti



(3) At a small scale nnaweza nikahitaji wataalamu wangapi kuendesha uzalishaji .. Cheap labour is not a problem..
 
Watu kama nyie serekali ingetakiwa iwasaidie maana mambo mengine huko mbele kiza ...kama hizo research si pesa yako itaishia huko?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom