Slavery Industry in Dar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slavery Industry in Dar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dua, Oct 17, 2007.

 1. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  The house-girl ’slavery’ industry in Dar.
  Sheria zetu za wafanyakazi wa nyumbani ni hafifu sana na swala hili ni lazima serikali ilishughulikie ingawaje wengi wa watuhumiwa ndio wafanyakazi wa serikalini ambao kipato chao sio kikubwa. Lakini madhara yake ni makubwa kwa taifa. Naomba tulijadili hili kwani wengi wanaodhurika hawawezi hata kujisemea.
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Oct 17, 2007
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  ndiyo maana tukipata nafasi katika balozi zetu baadhi yetu tunaleta watumishi wa ndani na kuwatendea kama watumwa...
   
 3. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hili kwa muda mrefu inanisikitisha mimi. Watanzania wengi
  sana wana hawa wafanyakazi wa ndani lakini hawawatendei haki.

  Kuna watu niliwahi kuwaambia wanachofanya ni makosa, hawakuongea na mimi kwa muda mrefu.

  Watoto wengi ni wadogo na wanatakiwa kuwa shuleni badala ya kufanyishwa kazi za majumbani.
   
 4. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  i guarantee you ni kesi moja tu ya yule balozi aliondoka, Daraja, kulikoni kugeneralize mzee ? Au kuna balozi mwingine aliyefanya hayo mambo ? hivi mama Maajar naye anafanya hivyo hivyo ?
   
 5. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2007
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,596
  Likes Received: 6,757
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli hii ishu ni serious sana!,
  Wafanyakazi wa ndani kwa majumba yaliyo mengi is absolutely an open slavery!

  Kwanza wengi hawaweki mikataba ya kikazi wanapoanza kazi, hivyo hii inatoa uhuru kwa mwajiri kufanya uamuzi wowote bila kumshirikisha house girl.

  Pili kazi wanazotakiwa kufanya haziwi specific, yaani mfanyakazi wa ndani atatikiwa kufanya kazi yoyote itakayoletwa mbele yake na Mwajiri, hakuna time table ya kazi, yaani lilomo katika akili ya mwajiri ndo hilo hilo twende

  Wengi hawapewi uhuru wa kutosha wa kufanya mambo yao binafsi, yaani wengi wanageuzwa kama wafungwa wakati mwingine, mathalani mfanyakazi wa ndani anapotaka kwenda kuwaona ndugu, jamaa na marafiki, ama kutembea zake ama kufanya mambo mengine kama vijana wengi "walio huru" watakavyo, mara nyingi bosi hamkubalii.

  Pili unyanyasi wa halia ya juu, Mabosi wengi wa kiume huwataka kimapenzi wafanyakazi wa ndani kwa kutumia njia za kinyanyasaji,
  wengi hutishiwa kufukuzwa kazi iwapo hawakubali matakwa ya mabosi wao. pia kutokupewa mishahara yao kwa wakati muafaka na wakati mwingine kutokupewa kitu kabisa,

  Pia kutokuzingatia umri wa mfanyakazi wa ndani mwenyewe,
  unakuta mfanyakazi anahesabika kisheria kama mtoto "under 18" lakini anapewa kazi za kulea familia ,kulea watoto wenzie, kazi lukuki zisizo mithilika.

  Actually jamii ya watanzania inabidi tulitizame hili swala kwa makini sana, iwapo tunalalamikia mambo tuliyofanyiwa na wazungu enzi hizo, haifai na sisi kuwafanyia binadamu wenzetu, hata kama kijuu juu itaonekana kama ni makubaliano ya watu wenyewe
   
 6. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Dua,
  Hizo sheria zipo, lakini kutokana na hali halisi hazitekelezeki. Unajua hata hao wanaofanyiwa mambo hayo akiangalia ni wapi akimbilie, kwao ambako hakuna umeme, maji, hata kununua nguo na chakula ni isee, au kukaa Mjini ambako maisha ni better japo yana uchungu, anaona ni afadhari akae mjini. Nina mfano wa msichana aliyechukuliwa kutoka Iringa kuja Dar, aliporudishwa Iringa baada ya kujirusha na mume wa mtu, baada ya mwezi mmoja karudi dar, aliyokuwa anafanya hayakuwa masafi lakini, ndiyo yaliyomuwezesha kuishi na kuachana na kadhia ya kijijini, Ni vigumu lakini ni hali inalazimisha hivyo.
   
 7. Dua

  Dua JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2007
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 2,481
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Bongolander

  Nafikiri kama sheria zipo tuanze sasa kutuma wachunguzi kwenda kwenye nyumba na kupata ushahidi. Kwanza nafikiri kama sheria zipo ziwekwe kwa uwazi walipwe kiasi gani na masaa ya kazi yaanikwe, haiwezekani mfanyakazi kufanya kazi round the clock wakati halipwi hivyo. Kuna mahali lazima tuanzie ndio changamoto hii JF members watoe madukuduku yao. Karne ya 21 utumwa upo mbele ya macho yetu na sisi tupo kimya.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...