"Slang" sio kile wanachofikiri

Translator

JF-Expert Member
May 19, 2017
286
297
Mara nyingi mtaani utasikia watu wakisema, “Jamaa anapiga slang si mchezo.”
Wengi hudhani “slang” ni Kiingereza cha Kimarekani.

Lakini maana halisi ya “slang” ni lugha ya mtaani. Ni ile lugha ambayo utajisikia aibu kuitumia mbele ya watu unaowaheshimu. Na mara nyingi huwa ni maneno yanayokaa kwa muda kisha yanapotea.

Hivyo, kila lugha ina slang – iwe Kiingereze, Kiswahili, au lugha za makabila yetu.
Je, ulikuwapo wakati slang hizi za Kiswahili zikiwa kwenye chati? :D:D

Nakitoa …………. naondoka zangu
Nitakufua ………nitakupiga
Manzi …………… msichana
Mshikaji ……….. mpenzi wa jinsi tofauti (siku hizi ni rafiki tu wa kawaida)
Bonga ………….. tongoza (siku hizi ‘zungumza’)
Dingi ……………. baba
Charara ………... ishiwa fedha
Mambo du kinaa .. mambo safi/poa :D:D:D

……………….

Hebu ongeza na mengine.
 
Nimecheka sana kwa uzi huu. Kipindi nipo form 5 tulikuwa kwenye paper, sasa kukawa na swali la kuelezea maana ya Slang, jamaa mmoja acha adundike anavyojua yeye akatoa na mifano anasema, instead of saying "whatsap a person can say Wharrap"
 
Nimecheka sana kwa uzi huu. Kipindi nipo form 5 tulikuwa kwenye paper, sasa kukawa na swali la kuelezea maana ya Slang, jamaa mmoja acha adundike anavyojua yeye akatoa na mifano anasema, instead of saying "whatsap a person can say Wharrap"
ha ha ha ha jamaa alikuwa anapakuwa kutoka kwenye back-up yake ya kichwani. :D:D:D
 
Wanachanganya slang na fluency.
Asante kwa mchango msakaa jr japokuwa fluency hasa inalenga uwezo wa mtu kuongea kwa ufasaha na bila kujiumauma. Lakini watu hawa hudhani tu kwamba slang ni kiingereza cha kimarekani, whether mtu ni fluent au la.
 
Unanikumbusha enzi zangu language advance, sijui ilikuwa language 2 ile au 1 huko. Jargon, bilingual sijui mataka taka gani huko. Duh!!! Kimalkia kimetukomesha kweli kweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom