Slaa: Watanzania ipuuzeni CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa: Watanzania ipuuzeni CCM

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rugemeleza, Oct 11, 2010.

 1. R

  Rugemeleza Verified User

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  • Asema imeonyesha dalili za kufa

  na Mwandishi wetu

  MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amewataka Watanzania kupuuza ujumbe mfupi wa maneno (sms) unaosambazwa kupitia simu mikononi kuwa ni ujanja wa Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuona kimekabwa koo kila kona. Akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Kalinzi, Dk. Slaa alisema CCM imekabwa koo kila idara hivyo imelazimika kutuma ujumbe kuwahadaa Watanzania ili waamini uongo unaosambazwa.

  "Nimesikia wanasambaza ujumbe kwenye simu za mikononi wanasema mimi ni mropokaji… nawaambia Watanzania wenzagu, wapuuzeni CCM hii ni dalili tosha kwamba tumewakamata kila kona wanahaha kujinasua…hizi ni porojo za CCM; zinaonyesha wazi sasa wameanza kutapata kama mtu anayetaka kufa, imeonyesha sasa ni kama inapumulia mashine," alisema Dk. Slaa.

  Alisema kutokana na hali hiyo, CCM imekuwa bingwa wa kumzushia mambo mbalimbali ambayo hayana ukweli wowote mbele ya jamii.

  Akizungumzia suala la yeye kuambiwa anataka kwenda Ikulu kwa njia ya kumwaga damu, Dk. Slaa alisema amekuwa mbunge wa jimbo la Karatu kwa kipindi cha miaka 15 bila kumwaga damu ni kitu ambacho hakiwezekani hata siku moja.

  "Nimekuwa mbunge wa Karatu kwa kipindi cha miaka 15, sikumwaga damu… sasa hiyo damu itatoka wapi? Kwa vile tumefanikiwa kuwabana wanahangaika kujinasua," alisema Dk. Slaa.

  Alisema pamoja na yeye kuitwa mropokaji, anakubali kwa vile uropokaji huo umezaa matunda kipindi chote alichokuwa bungeni.

  "Wananiita mropokaji, mimi nasema sawa nimeropoka na matunda yangu yameonekana, niliwataja watu kama Basil Mramba, Gray Mgonja na Daniel Yona mbona wamefikishwa mahakamani? "Kama nisingefanya hivi wangeendelea kutafuna fedha za walipa kodi wa nchi hii….nawaambieni jamani hata wakati ule nilimtaja Rais Jakaya Kikwete mbona hawajanikamata kama ulikuwa uongo?" alihoji Dk. Slaa na kushangiliwa na maelfu ya wananchi.

  Akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Dk. Slaa alimmwagia sifa kutokana na shughuli za maendeleo alizozifanya jimboni kwake.

  Akihutubia mikutano ya kampeni eneo la Kagunga, Dk. Slaa alimmwagia sifa mbunge huyo anayetetea nafasi yake katika uchaguzi mkuu ujao kuwa ni jembe linalorahisisha kazi ya mkulima, kutokana na alivyoshirikiana na wananchi kutatua kero na matatizo yanayolikabili jimbo lake na mkoa wa Kigoma kwa ujumla.

  "Zitto amejipambanua kama mbunge anayejua majukumu na wajibu wake kwa wapiga kura, amekuwa akiisukuma kweli kweli serikali kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye jimbo lake na pale alipoona serikali inasuasua alitumia uwezo wake binafsi kama alivyofanya katika mradi wa umeme Kagunga kwa kuzungumza na serikali ya Burundi ili mpate umeme kutoka huko …nimepata taarifa kuwa mazungumzo yamefikia pazuri," alisema Dk. Slaa.

  "Huyu ni mbunge na mgombea unayemnadi kifua mbele siyo kama wengine ambao ukifika majimboni mwao unaogopa na kujifikiria utaanzia wapi kuwanadi," alisema Dk. Slaa.

  Aliwahakikishia wakazi wa kijiji hicho kuwa wataondokana na adha ya kutegemea mawasiliano ya simu za mkononi kutoka mitandao ya nchi jirani ya Burundi.

  Miradi mingine iliyofanikishwa kijijini hapo kwa msukumo wa Zitto ni ujenzi wa bandari ya kisasa inayoziunganisha nchi za Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Tanzania.

  Dk. Slaa alirejea ahadi yake ya elimu bure hadi kidato cha Sita ili kuwapa uwezo watoto wa Tanzania kuhimili ushindani katika soko la ajira la Afrika Mashariki na kutoa mfano wa watoto wa nchi jirani ya Burundi wanavyoweza kuongea kwa ufasaha lugha ya Kifaransa tofauti na wa hapa nchini ambao baadhi yao wanaohitimu elimu ya msingi bila kuwa na uwezo wa kuongea Kiswahili ambayo ni lugha ya taifa.
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Safi sana,

  Pasha pasha hadi Oct. 31. Ni moto chini, hakuna kula, hakuna kulala kweli!!
   
 3. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwi kwi kwi maji kushingo wanatafuta pa kupumulia hawapaoni. Kifo cha CCM kinazidi kukaribia. Hongera sana Dr Slaa kwa kampeni nzuri sana
   
 4. B

  Benny condrad New Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hebu tuwe tunatafakari sio kila taarifa unabeba hasa kipindi hiki cha uchaguzi. Tuache kuzoa propaganda na kuzipost tu hovyo hovyo kwa kuwa tu wewe ni mwanachama wa chama fulani. Unauhakika gani hizo msg zimeandikwa na CCM? Si propaganda ili useme kuwa wamekushindwa sasa wanatumia ujumbe kupotosha? Hebu tuwe wachambuzi jamani tusidandie kila unaloambiwa unalibeba.
   
 5. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwi kwi kwi kwi zimeandikwa na TLP maana Dr Slaa anatishia vitumbua vyao! Halihitaji kuumiza kichwa hili ili kujua ni nani wanaotuma jumbe hizo.
   
 6. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Hutaki kuamini? kama hicho kirusi bado hakijakufikia ni vema ukasikiliza ushauri humu ndani jinsi ya kukabiliana nacho maana kitakufikia mda sio mrefu!. Madhara yake ni kukuaribu uwezo wako wa kufikiria na kupembua mambo (Utaanza kuwasifia MAFISADI na hata kuwapigia kura) na hatimaye upofu wa ubongo!!!

  Karibu JF naona ndio post yako ya kwanza!
   
 7. M

  Mtuwamungu Senior Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 21, 2007
  Messages: 110
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Benny, chambua basi utuambie unachoamini ndio ukweli. Ukifanya hivyo, wana JF watachambua hoja yako kama ina mshiko.
   
 8. G

  Gofu Zulu Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 15, 2009
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Bwana ianwezekana huyo ni Post yake ya Kwanza.Si unajua tena Mtoto akianza kujifunza kutembea.....?Anasema tuwe wachambuzi wakati yeye mwneyewe uwezo wa kupambanua mambo hana....huyu naona kaja leo kabisa. Ni maoni yake anyway tuachane naye.
  Slaa uko juu endelea mwendo ni huo huo.Asiyekusikia na kukuelewa tutasaidia kumwelimisha.
  Slaa Juuuuuuuuuu!
   
 9. R

  Rugemeleza Verified User

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii ni kauli yake Dr Slaa kama ilivyo kwenye kitabusura chake:

  Watanzania msidanganyike: Watakaomwaga damu ni wao, ili wabakie madarakani!


  by Dr. Wilbrod Slaa on Sunday, October 10, 2010 at 4:04pm

  Hatari inayoikabili Tanzania haiko kwa watu wasio na madaraa, majeshi wala vyombo vya usalama katika amri ya vinywa vyao. Hatari hiyo haiko mikononi mwa upinzani usio na silaha za moto hata moja zaidi ya nguvu za hoja zake na ukweli wa ajenda yake. Hatari ambayo iko katika uchaguzi huu imo mikononi mwa viongozi walioshindwa ambao katika mikono yao zimo silaha za moto. Hawa ndio watatumia nguvu kubakia Ikulu na madarakani licha ya kukataliwa na wananchi. Tusiogope!

  Ndugu Watanzania, uamuzi uliopo mbele yenu ni uamuzi unaohitaji ujasiri wa maono, uthabiti wa moyo, na umakini wa fikra kuweza kuchagua kati ya viongozi tuliopo mbele yenu. Hata hivyo msikubali kutishwa na kiongozi yeyote mwoga ambaye ameshashindwa kuwashughulikia wahalifu na utawala wake siyo tu umewakumbatia lakini umefika mahali unawapigia debe wachaguliwe watuhumiwa wa uhalifu mbalimbali nchini. Kwa vitendo vyao wao wenyewe ndio wamesababisha kukataliwa na wananchi.

  Lakini ni wao vile vile ambao mikononi mwao hatima ya amani ya nchi hii imo. Kwa vile hadi hivi sasa wamekataa kuweka mazingira ya uchaguzi kufanyika katika uwazi na kwa vile hadi hivi sasa hawajatoa kauli yoyote ya kuahidi kukubali kwa njia ya amani kushindwa (watakaposhindwa Oktoba 31) tunabakia na jawabu moja tu; watafanya lolote ili wabakie Ikulu na hili ni pamoja na kutumia nguvu.

  Watanzania wenzangu, tusikubali CCM wabakie madarakani kwa sababu wanaona haya kuanguka kwenye sanduku la kura; tusikubali CCM ifanye Ikulu ni haki yake ya kuzaliwa na kuwa sisi sote ni matokeo ya mapenzi yake. CCM haijautengeneza upinzani wa Tanzania, na haijaruhusu upinzani kuwepo kwani haiwezi kuuzuia hata kama wakitaka. Upinzani wa Tanzania katika udhaifu wake wote umejengwa na wapinzani wenyewe bila ya msaada wa CCM au baraka zake na utaendelea kuwepo hata kama CCM na makuwadi wake wa ufisadi watataka iwe vinginevyo.

  Kauli mtakazoendelea kuzisikia kutoka kwa uongozi wa CCM na makada wake ni kauli zenye lengo la kuchezea akili za Watanzania, kupandikiza hofu na kuwafanya watu wapige kura si kwa sababu ya matamanio ya mioyo yao bali kwa sababu ya hofu inayopandikizwa kwanza na jeshi, na sasa na Rais Kikwete na kina Kinana. Watanzania wawe na uhakika kabisa kuwa Chadema ni chama ambacho hakijawahi kutumia nguvu na hakitatumia nguvu kufikia malengo ya kisiasa lakini kitatumia mbinu zote za kiraia na kidemokrasia kushinikiza watawala wawe tayari kuheshimu matokeo ya uchaguzi.

  Nawasihi Watanzania wasidanganyike wala kutishwa na manabii wa umwagikaji damu ambao wanatumia majukwaa ya kisiasa na ofisi zao ili waje baadaye kuutumiza unabii huo potofu. Uchaguzi huu utakuwa ni wa amani, na CCM na serikali yake licha ya mbinu mbalimbali ambazo tumedokezwa zinajaribiwa kutumiwa ili wabakie madarakani hawatakuwa na nafasi hiyo kwani wameshakataliwa katika mioyo ya mamilioni ya Watanzania ambao watalithibitisha hili kwa kutuingiza madarakani ili tusafishe miongo karibu mitano ya madudu ya utawala ulioshindwa wa CCM.

  Nawasihi mtuunge mkono, msidanganyike na pamoja tutaweza! Huu ni wakati wa mabadiliko na hii ni saa yetu!

  Naomba ueneze ujumbe wangu huu kwa marafiki zako. Asanteni.
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hebu toa upumbavu wake hapa
   
 11. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,938
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  SMS hiyo imejidhihirisha kwenye sehemu ya hotuba ya JK pale uwanja wa Maji Maji jana; hivyo ameituma JK!
   
Loading...