Slaa: Pinda toa taarifa ya Michango ya Wahanga wa Mafuriko Kilosa,Dar na wa Mabomu Mbagala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa: Pinda toa taarifa ya Michango ya Wahanga wa Mafuriko Kilosa,Dar na wa Mabomu Mbagala

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtanke, Aug 17, 2012.

 1. M

  Mtanke JF-Expert Member

  #1
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 19, 2011
  Messages: 282
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Baada ya kutembelea waathirika wa Mafuriko huko Kilosa akiwa katika Operesheni Sangara inayoendelea katika Mkoa wa Morogoro, Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Wilbrod Slaa amemtaka Waziri Mkuu kutoa taarifa ya michango iliyotolewa na Libya ya nyumba, hela zilizochangwa kwa mitandao ya simu, Serikali kupitia kitengo chake cha maafa,Taasis na watu binafsi kwani Waathirika hao bado wanaishi kwenye Mahema na wengine waliambulia bati moja, mbao moja na cement mfuko mmoja katika mgao wa michango inayodaiwa kukusanywa. Nyumba alizotoa Gadafi kabla ya kuondolewa Madarakani wajanja wamegawana baada ya Gadafi kufa. Mkurugenzi yeye amejijengea Hotel yake Kubwa hapa hapa Kilosa na akina Mkulo wanajua walichofanyia na mgao wao
  .Slaa: Pinda toa taarifa ya Michango ya Wahanga wa Mafuriko Kilosa - YouTube
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Aug 17, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Mwaka huuu Pinda atajuta walahi kila kona maswali magumu ambayo anayajibu kama anaota vile,sidhani kama miaka ijayo watakodi ndege kukimbilia form dodoma;ujinga unaendelea kututoka taratibu!na utafikia mwisho soon !ukombozi waja,bado Mbagala na Gongo la Mboto.....kote wamechakachua na jibaba moja bingwa kuacha kifua wazi mzee mzima!
   
 3. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #3
  Aug 17, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Katika ripoti ya CAG ilionyeasha ufisadi mkubwa katika mfuko wa maafa ambao upo chini ya ofisi ya waziri mkuu.ukiachilia mbali wahanga wa kilosa,kuna mbagala,gongolamboto na jangwani wote wamelambishwa reli walionufaika ni maofisa wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa dar waliokuwa wanaratibu shughuli za kuwasaidia wahanga.
   
Loading...