Slaa ni living nyerere!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa ni living nyerere!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by chidide, Dec 21, 2010.

 1. c

  chidide Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema njia ipo nyeupe kwa viongozi na wanachama wanaotaka kuondoka katika chama hicho kwa sababu ya kutoridhishwa na mgawo wa viti maalum vya wanawake katika Bunge. [/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Akizungumza jana katika mkutano wa Baraza la Ushauri la Chadema jijini hapa, Dk. Slaa alisema tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, yamejitokeza malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi na wanachama kwamba mikoa yao haijapata wabunge wa viti maalum licha ya kuwapo wabunge wa majimbo.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema miongoni mwa mikoa inayolalamika ni pamoja na Mbeya, ambao umepata wabunge wawili wa kuchaguliwa, lakini haukupata mbunge wa viti maalum.[/FONT]
  “[FONT=ArialMT, sans-serif]Watu wa Mbeya mnalalamika sana kuhusu suala la viti maalum wakati Karatu tumeibeba Chadema toka mwaka 1995 hadi sasa, lakini hatujawahi kupewa viti maalum vya ubunge. Mbeya ni juzi tu ndiyo mmeanza kuibeba Chadema, halafu mnasema mnataka kuondoka kwenye chama. Tunasema ondokeni njia nyeupe kwa anayetaka kufanya hivyo,” alisema Dk. Slaa.[/FONT]
  [FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema viongozi wasioelewa kuhusu utaratibu wa utoaji wa viti maalum wanakuwa na ubinafsi wakati Chadema viti maalum havitolewi kama zawadi na wala siyo hisani kama wanavyodhani baadhi ya watu, bali vina malengo yake.[/FONT]
  CHANZO: NIPASHE

  Slaa ni my Living Nyerere. Haumi maneno, kwake ni bora watu wamchukie kwa kusimamia ukweli.Na hii ndio moja ya vitu vilivyofanya Nyerere apendwe na aaminike. Kwa kweli kwangu mimii huyu ni mwanasiasa bora wa Taifa kwa sasa na itakuchukua muda mrefu kutokea mwanasiasa mwingine kama yeye. Fikiria aliona ni bora AKAE kimya baada ya matokeo yake kuanza kuchakachuliwa, kama angekuwa mbinafsi Tanzania leo ingekuwa kama Ivory Coast. SLAA wewe ni mwanga kwenye GIZA NENE!!!
   
 2. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  He is indeed, a living nyerere.
   
 3. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Slaa amepambana kwa mengi hata hao SISI M wanajua ndio maana hata mkuu wa nchi na baadhi ya mawaziri walikuwa wanatekeleza aliyokuwa anayasema kwa kifupi miaka mitano iliyopita ndiye alikuwa akiongoza nchi.
  Slaa ni my Living Nyerere wa kweli amini usiamini. Harembi maneno, kwake kusimamia ukweli tu.Na hii ndio moja ya vitu vilivyofanya Nyerere apendwe na aaminike. Tukubalu tusikubali huyu ni mwanasiasa bora wa Taifa kwa sasa itachukua muda mrefu sana kupata mwanasiasa mwingine kama yeye. Fikiria aliona ni bora AKAE kimya baada ya matokeo yake kuanza kuchakachuliwa, kama angekuwa mbinafsi Tanzania leo ingekuwa kama Ivory Coast. Lakini yeye kwa busara akatulia na kuongea kwa hekima
   
 4. s

  skeleton Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa Dr. Slaa hakuna kama yeye, si mbinafsi, si mnafiki , hana tamaa! Yuko tayari kufa kwa ajili ys nchi yake.
   
 5. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Long live Doctor Wa Ukweli
   
 6. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  sawa kabisa, hasa suala la kukaa kimya baada ya kuibiwa ushindi na CCM, tena alisema hawezi kwenda Ikulu kwa damu kumwagika. Sasa CCM kwa mambo ya Umeya wa Arusha na Mwanza inaonyesha jinsi gani hamkuwa tayari kuaachia serikali kwa Chadema. Tena nasikia JK akiwa pale Arusha katika ufungizi wa hotel ya Mount Meru alitamka Meya wa Arusha atoke CCM.... sasa kuna umsemo kwamba matakwa ya mkubwa ni amri.....
   
 7. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  Ni slaa tu kwa sasa mwenye uthubutu alokuwa nao nyerere
   
 8. N

  Nancy Tweed Senior Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I have no idea what strain of cannabis do these posters take.
   
 9. n

  nyantella JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Muulize Prof Lipumba! kichuguu tangu lini kikafananishwa na Mlima Kilimanjaro? huwezi kuwa hujalewa hadi kufananisha usingizi na kifo!
  Nyerere hawezi hata kidogo kufanata na Slaaaaa! this is just another crap!
   
 10. r

  roby m Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Ndo viongozi wanotakiwa Tanzania!!!
   
 11. w

  warea JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huu ni wivu tu! Kwa nini Nyerere asifananishwe na Slaa. Mie nafikiri Slaa amemzidi Nyerere. Wapi Nyerere alifanya kama Slaa! Kuwataja watuhumiwa wa Ufisadi "List of Shame" inayomjumuisha na rais wa Nchi. Wakati akiwa rais mstaaf Nyerere mbona hakufanya hivyo? Slaa alikuwa mbunge tu, akamtaja rais wake kuwa ni miongoni mwa mafisadi. Slaa bado ana nafasi ya kufanya zaidi. Nyerere aliua demokrasia kwa kuiweka CCM kama serikali! Nyerere aliona mambo yamemshinda akasema anang'atuka. Siasa zake zimeshindwa na zimekufa. Slaa akipewa urais atafanya makubwa zaidi.
   
 12. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono chidide, Hatuwezi kumpata kiongozi ka Dr.Slaa kwa wakati huu maana hapendi kusema uwongo hata kidogo, na yuko kwa ajili ya maslahi ya watu na si yake kama wengine wanavyofanya.
  Kumbuka alikuwa ni mbunge wa kwanza kutaka mishahara ya wabunge ipunguzwe.

  Peoples power
   
 13. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Humu JF hatutaki chuki binafsi kama wewe uko makini hata lipumba alikiri baada ya uchaguzi Dr.Slaa si kichuguu baada ya waTZ kumpa kura nyingi za kutosha , CCM wakaiba hadi zikabaki 2.26mil, Tutake radhi
   
 14. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tupe msimamo wa Lipumba rais wa CCM-B ili tumfaninishe na kifusi. Aliishia wapi kwenye uchaguzi; vumbi jepesi
   
 15. mapango

  mapango Member

  #15
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nakubalina na wewe kuwa "slaa ni living Nyerere", kwani Nyerere aliwaambia hivyo hivyo wana CCM wenziwe waliotaka mabadiliko ndani ya CCM, kumbuka akina Seif Sharif na wenzake miaka 1987-1989 walipokuwa wanapigania mabadiliko ndani ya CCM, kumbuka pia G55; kundi la wabungu 55 wa CCM waliodai serikali tatu bungeni, wote hawa waliwaambiwa kuwa wapinge chama wakiwa nje ya chama Hivyo. Mimi kwangu kumfananisha na Nyerere kwa kuwataka watu watoke chamani kuonesha kutoridhika maana yake ni Dictator kama alivyokuwa Nyerere, Nyerere aliziona fikra zake ndio kila kitu, na leo ndio tunalia na kero za muungano, hizi sio kero za muungano bali ni "kero za Nyerere".
   
 16. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kuna chizi mmoja kwa habari hii hii alimwita dicteta
   
 17. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Hebu nijibu haya maswali ili nami niweze kuamini hayo uyaaminiyo
  1. Je Nyerere alipendelea kuwapa watu madaraka?
  2. Je Nyerere alichukua /kupora mke wa mtu?
  3. Je Nyerere alihubiri udini kwenye uchaguzi?
  4. Je Nyerere alikuwa mchochea vurugu ?
   
 18. d

  dotto JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kinachoongelewa hapa siyo mambo binafsi na mepesi kama ulivyoorodhesha. Mbona uko hivyo!! Uwezo wako wa kufikiri ni mdogo mno mno tu. Nahisi hauko sawa. tafakari kabla ya kufanya jambo. Dr. Slaa huwezi kumlinganisha na kiongozi yeyote wa sasa hapa Tanzania. Jaribu ulinganishe Dr.Slaa na Dr. Kikwete. Mfano: CCM kuogopa kumtuma Dr.Kikwete kwenye midahalo ya Urais na wenzake ni kuwa haaminiki kabisa.
   
 19. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Ningeomba title ikae ivi: mwl. Nyerere afanana na Dr.Slaa. Mwl alimtangulia slaa lakini anayofanya slaa mwl.aliyaogopa mwl kabla ajaacha mwili alikuwa akichukia na kuiponda ccm na ufisadi kwa mafungo,alifika hatua akataka kurudisha kadi ila si hadharani,mwl aliwaogopa sana wenzie ila leo dr.anasema kamwe Cdm haiko tayari kuona kiongoz mwandamizi wa chama akivunja taratibu,wanaonyana hana kwa hana. Huu ni ujasiri mkubwa. Mwl alisema jeykey ajakomaa kifikra na kimawazo kuikokota nchi na Edward Lowasa ni mchafu,je alishindwa kuueleza umma kuwa ni mafisadi?mtanzania wa darasa la nne akisikia kuwa mtu ni mchafu anaoji kwa nini asioge,ila angeambiwa ni mdokozi wa umma kamwe leo angekuwa anafuga kuku monduli. Leo dr.anasema hawa ni mafisadi mapapa! Kweli nyerere afanana na Slaa,tofauti ni nani alitangulia tu! Dr Slaa tunakuamini!
   
 20. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #20
  Dec 23, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ni lazima tu uyaamini maana
  1. Nyerere hakupendelea kuwapa watu madaraka kama Slaa asivyopendelea!
  2. Nyerere hakuchukua/kupora mke wa mtu kama Slaa ambavyo hajapora mke wa mtu bali amechumbia mwanamke aliyeachika!
  3. Nyerere hakuhubiri udini kwenye uchaguzi kama Dr. Slaa bali kikwete ndiye Mdini kwa kutumia misikiti
  4. Nerere hakuchochea vurugu kama Dk Slaa ambavyo amekuwa akihimiza watu kutulia na kuwaacha CCM wakiiba kweupe bila kuitisha maandamano ya kulaani uchakachuaji.
   
Loading...