SLAA: NEC yacheza mchezo mchafu na masanduku ya kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SLAA: NEC yacheza mchezo mchafu na masanduku ya kura

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by The Informer, Oct 26, 2010.

 1. T

  The Informer Senior Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  DAR ES SALAAM, Oktoba 26, 2010

  Nimetoka kuhudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika Manzese Bakhresa mchana wa leo hii ambapo Dk. Willibrod Slaa alimnadi mgombea wa ubunge wa Ubungo, John Mnyika.

  Mkutano ulifana sana, Mnyika anakubalika sana na wapiga kura. Ni dhahiri kuwa tashinda na hatimaye kuwa mbunge licha ya njama za CCM za kuiba kura. Mnyika kasema kuwa amejipanga kuweka mawakala zaidi ya 3,000 kwenye vitua zaidi ya 1,000 vya kupiga kura jimboni Ubungo ili kulinda kura za ubunge na urais za CHADEMA zisiibiwe.
  Kasema mawakala hawa ambao wamechujwa na kuchaguliwa vizuri ni pamoja na wasomi wa vyuo vikuu, marafiki zake na vijana wengine waliojitolea. Kasema wameapishwa kulinda kura zisiibiwe come what may.

  Kwa upande wake, Slaa alitoa hotuba kali iliyoshangiliwa sana na wananchi wa Manzese.
  Slaa alisema kuwa gari linalotumiwa na Tume ya Uchaguzi aina ya Nissan Patrol, T895 APR, lilionekana kaskazini mwa Tanzania likipita Manyara na jimbo ya Karatu eti wakidai NEC imesahau kusambaza vifuniko vya masanduku ya kupiga kura. Eti wafanyakazi wa NEC wamesambaza masanduku ya kupiga kura kwenye baadhi ya vituo na kusahau vifuniko vyake! Slaa aliwataka wananchi kufanya "Citizens' arrest" kwa kuwakamata watu bila kuwapiga na kuwafikisha kituo cha polisi pale wanapoona kura zinaibiwa au kuna kitendo chochote cha kuvunja sheria.
  "Jukumu la kulinda kura ni letu wote," alisema Slaa huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi wa Manzese, wengine wakiwa juu ya miti na wengine juu ya trailer la takataka ili mradi wamuone Rais mtarajiwa akiongea.
  Mabango ya wananchi yalisema: "Slaa kiboko cha mafisadi" na "Ridhwani, hii si nchi ya kifalme."

  Slaa alisisitiza kuwa akiwa Rais atatoa elimu bure na kushusha bei ya mabati na simenti mpaka kufikia shilingi elfu 5. Alisema kama serikali inaweza kuweka ruzuku kwenye mbolea, haoni sababu ya kushindwa kuweka ruzuku kwenye vifaa vya ujenzi.
  "Nikiwa Rais nitaondoa anasa Ikulu. Mbunge analipwa posho kwa siku ya shilingi 160,000 bila kodi na mshahara wa shilingi milioni 7 kwa mwezi wakati mwalimu analipwa mshahara huohuo wa shilingi 160,000 kwa mwezi na bado ukatwe kodi," alisema Slaa.
  "Mwaka 2005, kilo ya sukari ilikuwa shilingi 400, sasa ni sh 1,800 na watu wameacha kunywa chai. Kilo ya nyama ilikuwa shilingi 800 sasa inafika mpaka sh 3,500," alisema.
  Alisema kuwa kamwe bunduki haiwezi kupambana na nguvu ya umma -- people's power.

  "Kikwete akubali kiume kuwa sasa muda wa kustaafu kiheshima umefika," alisema huku akishangiliwa sana.

  "Serikali ya Kikwete ni serikali ya anasa. Inatenga sh bilioni 30 kwa chai na vitafunio kwenye ofisi za vigogo wakati Watanzania hawana chakula." Alisema serikali ya CCM inaweza kusambaza mabango ya Kikwete nchi nzima bure kwa kutumia kodi ya wananchi, halafu ina jeuri ya kusema kuwa elimu bure haiwezekani.
  "Nimetoka nyumbani kwa Kikwete Bagamoyo, mashimo manne ya vyoo kwenye shule yamejengwa kwa shilingi milioni 700," alisema na kumshutumu Kikwete kwa kukosa dhamira ya kuleta maendeleo kwani anapotoka yeye Bagamoyo bado kuna nyumba za mbavu ya mbwa.
  Slaa alimshangaa Kikwete kwa kuwashika mikono kina Edward Lowassa, Basil Mramba na Rostam Aziz kuwa ni wachapa kazi wakati wana tuhuma nzito za ufisadi.
  Alienda kusisitiza kuwa vurugu au umwagaji damu utafanywa na serikali na CCM kupitia vijana wa green guard ambao wananuliwa pepper spray na pingu pamoja na kupewa mafunzo ya kijeshi.
  "CCM kimekuwa sasa chama cha kigaidi!" Alisema na kuwataka wananchi kutojibu matusi au vurugu za vijana wa CCM na badala yake wapige kura kwa amani.

  (Picha hizo zinaonesha Slaa akiwa Manzese leo)

  Naomba kuwasilisha....
   

  Attached Files:

 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,135
  Trophy Points: 280
  safi sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 3. T

  The King JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 357
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukrani sana kwa kututaarifu na picha.
   
 4. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wadanganyika bana.

  Slaa mwenye anajua Kikwete ndio Rais, haachi kutaja 'Serikali ya Kikwete.....'
   
 5. T

  The Informer Senior Member

  #5
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Picha nyingine hiyo kutoka Manzese leo...
   

  Attached Files:

 6. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Slaa nakupa hiii malizia kazi baba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 7. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Picha zikuzwe ikiwezekana
   
 8. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Zikuzwe JF, kwenye gazeti au kwenye mabango?
   
 9. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu.

  Tafadarini wenye uwezo wazikuze hizo picha!!
   
 10. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Safi asante.
   
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nimemuona Michuzi na yeye alikuwepo. Angalia picha nimeweka alama.

  Alipigwa hotuba hadi akasahau kupiga picha.

  Ila sidhani kama ataweka picha yoyote kwenye BLOG yake au Daily News.

  [​IMG]

  Michuzi.jpg
   
 12. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,919
  Likes Received: 12,106
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 13. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2010
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  hii imetulia nadhani baada ya kutoka mazese amekwenda mwembe yanga maana mida ya saa 7 mchana kulikuwa na msafara wa pikipiki za kutosha zimepaki pale tazara police wakisubiri wenzao na magari mengine yenye bendera
   
 14. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Kweli Tusifanye makosa ya kuchagua Rais mgonjwa nchi ikapata hasara ya kurudia uchaguzi, Dr wa Ukweli anapasua jipu Pwaaaaaaaaaa!
   
 15. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,852
  Trophy Points: 280
  Safari hii CCM na JK watawafahamu watanzania
   
 17. K

  King kingo JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 401
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Asante Mkuu kwa taarifa ila tuna kila sababu ya kutokuwachagua hawa mafisadi wanawezaje kujenga mashimo manne ya vyoo kwa mil 700, huu ni wizi tu
   
 18. R

  RUSHAMAWE Member

  #18
  Oct 26, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hebu mtazame huyo mama mwenye mtoto mgongoni mbele ya michuzi, kwa mtazamo wangu anaomba dr.slaa aingie ikulu mapema ili aepukane na mateso anayoyapata.
   
 19. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  yaani jumapili naona kama haifiki vile
   
 20. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
Loading...