Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
Mkuu Mwikimbi,
Umemsahau Paul Kyara
Umemsahau Paul Kyara
Tatizo la Tambwe ni kuwa anatumiwa na CCM kuropoka yale ambayo CCM wanayapanga gizani kwa lengo la kuua upinzani.Kauli ya Tambwe ni ya mwanasiasa uchwara ambapo huwezi kumzania Tambwe kwa kumtizama kwa umbo la nje.
Tanzania haihitaji siasa za vitisho na maneno machafu.Inajulukana wazi kuwa CCM wanawatumia wanasiasa uchwara nje na ndani ya chama chao pamoja na vyombo vya dola kutaka wanatarime na watanzania waamini kuwa Chacha Wangwe aliuwawa na viongozi wa chadema.
Kila mtanzania mwenye hekima hataacha kupuuza kauli rejareja kama hizi za Tambwe.
Ni afadhali kumdanganya mtu anayefahamu kuliko kumdanganya asiyefahamu kwa kuwa siku atakapofahamu kamwe hatadanganyika tena.Watanzania siyo mabwege tena asilani
Mkuu heshima mbele,umepiga bull.Nasisitiza tusitegemee kulishwa habari tujaribu kuchuja na kutafakari kwa kina,halafu tutoe maamuzi.Mtindo wa kulishwa na kumeza kama makinda ya ndege umepitwa na wakati.Mchukia fisadi,
Wajua vita yoyote haikosi kasoro.Katika harakati za kuifikia demokrasia pevu kwa nchi kama yetu kuna milima na mabonde sana.Bahati mbaya wengi wa wanaoingia kwenye siasa ni wabinafsi.Wanaifanya kazi ya siasa kama mradi wa familia hivyo kula yao na vaa yao inatokana na siasa.
Katika hali kama hiyo tusitegemee kila anayejiita mwanasiasa kuwa mwadilifu.La msingi mimi na wewe tujitambue na kuchukua hatua.Uchafu wa mwenzio usiwe sababu ya wewe na mimi kuwa wachafu.Pili pale panapoonekana kuwa na mwelwkeo wa siasa safi na adilifu ndipo ps kuanzia.Kwa wingi wetu na umoja wetu tusitizame wengi wanaotuvunja nguvu bali wachache wanaotutia moyo.
Ni ngumu sana kuunganisha nguvu kisiasa kama mmoja anaweka maslahi ya taifa mbele wakati mwingine anawaza kujaza tumbo lake apate usingizi.Kuna wanasiasa wanadiriki kusema bora wapinzani tukose wote majimbo kuliko chama fulani kipate na sisi tukose.Huko ni kuishiwa kisiasa ndugu.
Mchukia fisadi,

Hivi tangu akina Slaa walipotuhumiwa na Mtikila kuwa wamehusika na kifo cha Wangwe wameshachukua hatua gani?Kama Mtikila alikuwa mzushi (binafsi naamini mwanasiasa huyo mufilisi anatumiwa) kwanini basi Slaa na wenzie hawajaenda mahakamani?Strategy yao ya kunyamazia (au kupuuza) tuhuma hizo doesnt seem to work.Ni dhahiri kwamba Tambwe,na wanasiasa wengine (including Mtikila) wasingeleta hoja ya kifo cha Wangwe kwenye uchaguzi huo iwapo suala hilo lingekuwa mahakamani.
As far as I know,jeshi la polisi lilishatamka kwamba Wangwe alikufa kifo cha "kawaida" (i.e. ajali).Kwa maana hiyo tungetegemea kwamba kauli yoyote inayopingana na tamko hilo la polisi ni sawa na uvunjifu wa amani hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi.Lakini Slaa na wenzie do know better priorities za jeshi letu la polisi.It goes without saying kwamba laiti watuhumiwa wa mauaji ya Wangwe wangekuwa viongozi wa CCM basi mtoa tuhuma hizo angekuwa Segerea muda huu na sio kwenye kampeni huko Tarime.
Ukimya wa Slaa na wenzake katika kushughulikia tuhuma hizi unachangia sana kulikuza jambo hili.Of course ni siasa za majitaka but what if zinaishia kuwa-cost watajwa kwa vile tu wanazipuuza?