Slaa na Wenzake Kukamatwa ndani ya 3 months-Tambwe Hiza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa na Wenzake Kukamatwa ndani ya 3 months-Tambwe Hiza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by jmushi1, Oct 3, 2008.

 1. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #1
  Oct 3, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Tambwe atishia CHADEMA

  na Kulwa Karedia

   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Oct 3, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Tambwe anasema watakamatwa baada ya miezi mitatu...Hii ni karata ya kisiasa kwasababu baada ya miezi mitatu uchaguzi utakuwa umekwisha....Kwanini wasikamatwe kabla ya uchaguzi ili tujuwe ukweli?
  Mimi naona uchaguzi huo wa Tarime usimamishwe hadi hapo ukweli utakapowekwa wazi ili kuwa protect wananchi.
  Wananchi wa Tarime waruhusiwe kuujuwa ukweli kabla hawajapiga kura kwa mtu asiyependa maendeleo yao.
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Oct 3, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Tambwe kumbe ni mtupu namna hii ? Do we have a room for scare politics ?Tarime sawa na Moshi mjini .Tambwe kweli ameshindwa kuelewa kwamba hata kama Slaa atakamatwa bado Slaa si wa Tarime na wale wataendelea kumchagua kiongozi wa Chadema ambaye ni Mtarime mwenzao anaye gombea Ubunge ?

  Hivi haya madai kama hayawezi kutokea Slaa hana haki ya kwenda Mahakamani ama kwa kuwa Mahakama ni za CCM ? Hivi kweli JK na CCM wanaweza kudiriki kutumia habari hizi kuomba kura za wananchi wa Tarime ? Ni CCM kuzidiwa ama do I smell something stinky ?
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Oct 3, 2008
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tatizo tz watu siasa wanachukulia kama usanii wakati its a serious profession.
  Sasa hayo ndo mambo ya kuongea mbele za watu kweli.
  Why after 3month?
  Bongo kazi ipo
   
 5. M

  Masatu JF-Expert Member

  #5
  Oct 3, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kaka salama lakini kaka?
   
 6. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #6
  Oct 3, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Wakamate kwanza mafisadi au hii si sawa?
   
 7. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #7
  Oct 3, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Oct 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  GT,
  Mwaka huu unao tu!
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  GT Mkuu ana itikadi za chama?
  Anyways..Hili kwa kweli si la kukenulia mapengo kwa kusema ukweli...Hujasikia wanasiasa walevi wa chadema na ccm wamechomana visu kwa mujibu wa kamanda Rwambow?
   
 10. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Natabiri mpasuko mkubwa CCM wakishindwa Tarime. Na ole wao CCM wanshindwe huko. tusubiri tuone. Hizi lugha sizo kabisa. Hawana tofauti na mtikila
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Oct 4, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  wamefilisika.Maji yapo shingoni watasema chochote,wataua Mbwa,kuku,watanunua shahada,wata-end up kumwagiwa pilipili na kuangukia pua siku ya motokea.poor CCM!
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Upinzani wametu let down. Kwa kutoungana kwa ajili ya kupigana na nunda sisiemu tumekwisha. Najua hii ni habari mbaya lakini habari ndiyo hiyo.
  Unajua kwa nini sisiemu walituma mwana sisiemu kwenda kununua kura za Chadema tena ofisini kwao?
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,556
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Kusema baada ya 3 months ndiyo fishy....Kisaikolojia wananchi tayari watakuwa wanajuwa ama kuamini kuwa kina Slaa walimwua Wangwe...Kwa maana hiyo wananchi wanasubiri tu muda wa uchaguzi upite ili Slaa akamatwe...What a PITTY.
  Hii ni HATARI sana na mimi nadhani kuna uwezekano wa machafuko zaidi kama siasa za namna hiyo zisipowekwa kando.
  Kuanzia wakati Dk Slaa akitowa habari za ufisadi huko bungeni..Marmo naye alileta madai hayo hayo kuwa watamkamata...Yani wameona hawa watu wanaweza kuchukuwa nchi na sasa desparation imekuwa unbelievable na kwa kweli tutaona mengi sana.
  Nawaombea Mungu wale wote ambao maisha yao yamo hatarini wakati huu mgumu kwenye historia ya Taifa letu na dunia kwa ujumla.
  Watanzania we should rise to the occassion and confront the evil when ever possible.
  This time we should do it ONCE AND FOR ALL.
   
 14. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,290
  Likes Received: 598
  Trophy Points: 280
  Kwa CCM na serikali yake, kushinda uchaguzi mdogo Tarime ni kitu muhimu sana bila kujali kama ushindi huo utapatikana kwa gharama ya maisha ya watu au la. Ku "counter" matukio ya watu kunyunyiziwa pililpili, leo magari yanayorusha maji ya kuwasha yameingia Tarime. Kwa mambo yanavyoendelea, kuna kila dalili kuwa CCM wamepania kulazimisha ushindi. Muhimu hata hivyo, inatakiwa kutafakari kitakachofuata iwapo CCM watalazimisha ushindi. Mbunge takayepatikana bila ridhaa ya wapiga kura atakuwa katika nafasi ipi mbele ya wapiga kura wake ukizingatia na ujasiri wa wapiga kura hawa? CCM na serikali yake bado watakuwa nguvu ya kumwaga huko baada ya miaka miwili uchaguzi utakapofanyika nchi nzima?
   
 15. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #15
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la Tambwe ni kuwa anatumiwa na CCM kuropoka yale ambayo CCM wanayapanga gizani kwa lengo la kuua upinzani.Kauli ya Tambwe ni ya mwanasiasa uchwara ambapo huwezi kumzania Tambwe kwa kumtizama kwa umbo la nje.

  Tanzania haihitaji siasa za vitisho na maneno machafu.Inajulukana wazi kuwa CCM wanawatumia wanasiasa uchwara nje na ndani ya chama chao pamoja na vyombo vya dola kutaka wanatarime na watanzania waamini kuwa Chacha Wangwe aliuwawa na viongozi wa chadema.

  Kila mtanzania mwenye hekima hataacha kupuuza kauli rejareja kama hizi za Tambwe.
  Ni afadhali kumdanganya mtu anayefahamu kuliko kumdanganya asiyefahamu kwa kuwa siku atakapofahamu kamwe hatadanganyika tena.Watanzania siyo mabwege tena asilani
   
 16. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #16
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mchukia fisadi,

  Wajua vita yoyote haikosi kasoro.Katika harakati za kuifikia demokrasia pevu kwa nchi kama yetu kuna milima na mabonde sana.Bahati mbaya wengi wa wanaoingia kwenye siasa ni wabinafsi.Wanaifanya kazi ya siasa kama mradi wa familia hivyo kula yao na vaa yao inatokana na siasa.

  Katika hali kama hiyo tusitegemee kila anayejiita mwanasiasa kuwa mwadilifu.La msingi mimi na wewe tujitambue na kuchukua hatua.Uchafu wa mwenzio usiwe sababu ya wewe na mimi kuwa wachafu.Pili pale panapoonekana kuwa na mwelwkeo wa siasa safi na adilifu ndipo ps kuanzia.Kwa wingi wetu na umoja wetu tusitizame wengi wanaotuvunja nguvu bali wachache wanaotutia moyo.

  Ni ngumu sana kuunganisha nguvu kisiasa kama mmoja anaweka maslahi ya taifa mbele wakati mwingine anawaza kujaza tumbo lake apate usingizi.Kuna wanasiasa wanadiriki kusema bora wapinzani tukose wote majimbo kuliko chama fulani kipate na sisi tukose.Huko ni kuishiwa kisiasa ndugu.
   
 17. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #17
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  It really a pitty Jmushi lakini tufike mahali watanzania tuwazoee sisiemu kuwa pale wanapoona wanazama wako tayari hata kuua sembuse kuzusha maneno kama hayo.
   
 18. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #18
  Oct 5, 2008
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Kama maneno haya yametoka mdomoni mwa Tambwe kwelikweli, basi jamaa huyu ni pumbavu kweli kweli kwani amekosa hata diplomacy ya kiuongozi.
   
 19. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mnaweza mkaungana katika maana kwamba wote mnapigana kuelekea upande mmoja. Lakini kuungana pekee yake bila ku Define vizuri adui yenu ni nani kunaweza wanyima ushindi vile vile.
  Adui wa nje siku zote ni rahisi sana kumtambua na kupanga mbinu za kupambana naye, tatizo ni pale azukapo adui katikati ya kundi lenu.

  Mtamtambua vipi? na mkimtambua mtapiga vipi?

  Adui ni pamoja yule mmoja wenu apiganaye kwa maslahi yake binafsi na yule apiganaye kwa mshahara na si kwa lengo la pamoja.

  Kuna maadui wengi ndani ya vyama vya upinzani.
  Maadui waliopandikizwa na CCM kupitia usalama wa Taifa.
  Pia maadui waliozaliwa ndani kwa ndani walio tayari kuwa vibaraka, wasio na matako wala kikao, hawana jinsi, wako tayari kutumika kama nguo ya ndani ili maradi tu malengo yao binafsi yatimie.

  Maneno ya kubuni toka kambi moja kamwe hayawezi kuivunja kambi nyingine, labda tu kambi husika iwe ni kambi via na kugeuka kuwa kambi tegemezi kimawazo, kimtizamo na kimwelekeo.

  Mtu mwovu siku zote hujidhihirisha kwa maneno na matendo yake mwenyewe.
   
 20. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  na maadui wa upinzani siyo ccm peke yao, ni pamoja na james mbatia wa nccr, mtikila wa dp, na hso akina chipaka wanaozungumzia uchaguzi wa tarime wakiwa peackcok hotel dsm
   
Loading...