Slaa na Lema wametofautiana kauli, wawachanganya wanachama wa CHADEMA

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
579
- Ni kuhusu wanachama wa chama hicho kuhudhuria mkutano wa amani.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Wilbrod Slaa na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wametofautiana kauli kuhusu wanachama na wafuasi wao kuhudhuria mkutano wa amani kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha leo.

Wakati Dk Slaa akiwahamasisha wahudhurie, Lema aliwataka wasihudhurie kwa sababu Jiji hilo lina matatizo mengi yanayohusiana na uvunjifu wa amani na bado Serikali haijayapatia ufumbuzi.

Mkutano huo umeandaliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi akitaka uvishirikishe vyama vyote vya siasa, viongozi wa dini na wananchi wa Jiji la Arusha kwa ujumla.

Akiwa kwenye Uwanja wa TCD Wilayani Kahama, Dk Slaa alisema kuwa ni nafasi kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wa vyama vya siasa kuhudhuria mkutano huo kwa kuwa si wa chama kimoja bali ni wote.

"Napongeza hatua ya kuitisha mkutano, amani inatafutwa kwa njia mbalimbali, sasa hili ningependa kuona wote wanashiriki," alisema.

Wakati Dk Slaa akisema hayo, Lema aliwahamasisha wanachama na wafuasi wa Chadema kutoshiriki mkutano huo hadi hapo Serikali itakapotoa majibu ya msingi ya chanzo cha kuibuka migogoro katika Jiji la Arusha.

Alisema chanzo cha migogoro ya Arusha ni uchaguzi wa meya ambao CCM ilicheza rafu kwa kumwingiza Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda kuwa mmoja wa madiwani wa jiji hali ya kuwa ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga.

Matukio mengine, alisema: "Kuna mauaji ya Januari 5, mwaka 2011, kuna mauaji ya Soweto yote haya tuliomba tume huru sasa leo wanataka mkutano wa amani hili hatukubali kwani ni mchezo mchafu...nawaomba wakazi wa jiji kutohudhuria mkutano huu," alisema Lema.

Wakati huo huo, Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Bavicha) limesema siku ya maadhimisho ya uhuru, Desemba 9, mwaka huu litafanya kongamano kujadili miaka 52 tangu Tanzania kupata uhuru imefikia wapi.

Pia, Bavicha imesema siku hiyo haitajali kuwa maadhimisho hayo yatafanyika kitaifa na kupigwa mizinga ila wao watafanya kongamano na Watanzania wenyewe ndiyo watapima wapi pakwenda kusikiliza vitu vinavyojadiliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Bavicha, Deogratias Munishi alisema viongozi wakuu wa Chadema watazungumza kwenye kongamano hilo na kwamba kila Mtanzania anaruhusiwa kushiriki ili kujua muelekeo wa nchi yake.


Mwananchi: Dk Slaa, Lema wasigana kauli.
 
Ww ndugu tupe habari za kigoma bana si upo huko? Au mambo hayajawa kulingana n mipango yenu?
 
Toka mwamzo niliwaambia kuwa Godbless J Lema ni mtu mwenye upeo mdogo wa kufikiri na anachojua yeye ni kuropoka tuu si kingine.

Hivi kama mtu mwenye utimamu wa akili anawazuia watu wasiudhulie mkutano wa amani atashindwa vipi kuwambia watu wa chome ofisi zao?

Mtu huyu atashindwa vipi kuwa shawishi watu kuingia msituni?

Hivi kama lema hataki amani kwanini tusiseme anataka vita.

Hivi kwa nini mtu kama lema asifurahie kuona nchi inaingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa nini wana arusha wanachagua kuwa na mtu wa namna hii?

Ni wazi chadema kuna tatizo kubwa la watu fulani kuogopwa hasa lema, lema ni mtoto kwenye siasa ana hitaji kuongozwa kabisa.

Lakini majanga haya yana lelewa na dr slaa mwenyewe kwani anamuogopa sana lema.
 
Last edited by a moderator:
Lema anawaingiza wafuasi wake chaka. kwenye mkutano uliofanyika Naura springs na Jaji Mutungi akiwepo. Lema alisaini hati ya maridhiano na kukubali kushiriki kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika sheikh amri abeid. Nashangaa baada ya siku tatu anaruka kimanga tena. kitu anachokiongea kwenye mikutano ya hadhara na alichokiongea Naura hotel ni vitu viwili tofauti.
 
TUNTEMEKE
Mkuu naona CHADEMA inakuumiza kichwa maana post zako nyingi ni hizo tu. Huna mambo mengine ya maana ukapost humu. What is Chadema by the way? Ife au isife wewe utapata nini au utapoteza nini. Unajihangaisha bure tu
 
Last edited by a moderator:
TUNTEMEKE ni kweli Arusha hakuna amani? Mbona tunafanikisha sherehe za harusi, ubarikio na kipaimara kwa kuchangishana bila kuulizana itikadi za vyama? Mbona tunapeana kazi bila kuulizia itikadi ya mtu?

Arusha tuko na amani sana labda viongozi wa kisiasa wao ndio hawaivii chungu kimoja lakini wananchi wala hatuna walakini sisi kwa sisi
 
Last edited by a moderator:
Hivi Lema ni waziri kivuli wa sector gani? Au ndo anatarajiwa kuchaguliwa kwenye baraza jipya kivuli
 
chademaa ni majanga.

Hamuheshimu kabisa Katibu Mkuu wao. Hivi unategema nini kwa mtu aliyekosa maadili? ni nani atamuheshimu?
 
Huwezi kuwa na jumuiya ambayo inaongozwa na heche halafu ikawa na manufaa kwa jamii haiwezekani.
 
Hadema wao mipango yao ni kumwaga damu kuandamana na kutoka kwenye vikao vya bunge mengine hawayajui kabisa.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom