Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikristo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa, Mbowe waweka wazi mrengo wao wa kikristo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sokomoko, Jun 25, 2011.

 1. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Si jambo la tetesi tena kwamba sera na mrengo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ni ule wa Kikristo. Hii ni kutokana na hatua yake ya kuweka wazi urafiki wake wa karibu na Chama cha Kikristo cha Ujerumani, Christian Democratic Union (CDU). Kutokana na urafiki huo, CDU kimesema kuwa kitawapa nafasi za mafunzo nchini Ujerumani vijana na viongozi wa Chadema, kusomea maadili na uongozi.

  Maadili na uongozi ambao kwa mujibu wa mtizamo na sera za CDU ni yale ya Kikristo kama yalivyobuniwa na mwasisi wa chama hicho Konrad Harman Joseph Adenauer. Taarifa zilizotolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa Chadema Mhe Freeman Mbowe zinasema kuwa fursa hiyo imetolewa kwa chama chake baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na ujumbe wa CDU uliokuwa ukiongozwa na Rais wa zamani wa Ujerumani Profesa Dk. Horst Kohler. Mazungumzo hayo yalimshirikisha katibu mkuu wa chama hicho Dk Wilbrod Slaa na viongozi wengine wa juu.

  Mbowe meviambia vyombo vya habari kuwa katika mazungumzo yao Kohler alisema dhamira ya kuwapa nafasi za masomo vijana viongozi wa Chadema inalenga kuwafanya wawe viongozi wenye maadili mazuri kwa taifa lao. "Tumekubaliana ambapo tutapata nafasi za masomo kwa vijana ambao ni viongozi wa Chadema kwenda kusomea uongozi na maadili chini Ujerumani" alisema. Kwa hapa nchini imeelezwa kuwa Chadema itafanya kazi kwa karibu na kwa kushirikiana na taasisi ya Conrad Adenauer Foundation ambayo ni ya taasisi ya Kikristo iliyo chini ya Chama cha CDU.

  CDU kikiwa kimeanzishwa mwaka 194, ni chama cha Kikristo kilichowaunganisha Wakatoliki na Protestant kikilenga kujenga Ujerumani yenye maadili ya Kikristo katika siasa, kijamii, maadili na kila kipengele cha maisha.Mwanzilishi wake Konrad Hermann Joseph Adenauer anatajwa kuwa mfuata Ukatoliki aliyekuwa tayari kuufia Ukatoliki wake na ambaye amefanya kazi kubwa kutaka kuona maadili ya Kikristo yakitawala na kuongoza siasa za Ujerumani na Kimataifa. Anatajwa kutoa mchango mkubwa katika kujenga Ulaya mpya ya Kikristo na umoja chini ya NATO baada ya vita Kuu ya pili ya dunia.

  Kwa upande mwingine rekodi zinaonyesha kuwa Konrad alichangia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa taifa la Israel, jambo lililoenda na kuporwa ardhi ya wapalestina na kudhalilishwa hadi hii leo.

  Ujerumani ikitajwa kama nchi ya Kikristo hii leo, mchango mkubwa unatokana na Konrad Hermann Joseph Adenauer na chama chake cha CDU pamoja na ile taasisi yake Konrad Adenauer Foundation ( Konrad - Adenauer - Stiftung ) (KAS). Hii ni taasisi iliyo chini ya chama rafiki wa Chadema, yaani CDU ambayo iliundwa mwaka 1956 ikiwa taasisi ya Kikristo ya kutoa elimu ya siasa na kiraia kwa mtizamo wa Kikristo. Awali ilipoanzishwa mwaka 1956 ilijulikana kwa jina la "Society for Christian Democratic Education Work" ndio mwaka 1964 kikapewa jina la Konrad Adenauer kwa heshima ya mwanzilishi wake.

  Ni taasisi ambayo ina miradi 200 katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo hii ya kutoa elimu ya siasa, maadili, uongozi na hata uchumi kwa vyama vya siasa ambavyo vinakubaliana na sera zake za Kikristo. Kwa upande wa chama cha CDU ambacho ni rafiki wa Chadema inaelezwa wazi kuwa "is Christian- based applying the principles of Christian democracym and emphasizes the Christian understanding of humans and their responsibility toward God" Kwa japo wale ambao sio wakristo wanaruhusiwa kujiunga na chama hicho lakini wajue misingi yake ni kinafuata maadili na kanuni za Kikristo katika siasa zake na namna ya kumwelewa binadamu na wajibu wake kwa "Mungu"

  Kutokana na msimamo wake huo wa kikristo chama tawala cha Ujerumani CDU kimekuwa mstari wa mbele madhubuti kupinga Uturuki isikubaliwe kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Uturuki inaonekana kama nchi ya Kiislamu kwa vile wananchi wake karibu wote ni Waislamu. Wakristo wa ndani ya Uturuki ni wale wahamiaji. Hata hivyo, pamoja na jitihada za CDU na Konrad yake kufanya juhudi za kujenga jamii ya Kikristo Ujerumani, Ulaya na Ulimwenguni dalili zinaonyesha kuwa Ujerumani inazidi kusilimu kila uchao. Hali hiyo imepelekea kiongozi wa nchi hiyo Chancellor Angela Merkel kutoa kauli akiwazindua Wajerumani wenzake kwamba nchi yao hivi sasa inakimbilia kuwa ya Kiislamu. Akinukuliwa na vyombo vya habari mwaka jana Kansela Angela amesema kuwa Wajerumani (Wakristo) wameshindwa kugundua jinsi Waislam walivyojipenyeza na kupenyeza dini yao Ulaya jambo ambalo limebadili hali ya mambo. Akasema kutokana na hali hiyo sasa itabidi Wajerumani wajifunze kuona Misikiti mingi zaidi ya Makanisa waliyo kuwa wamezoea kuyaona huko nyuma. Kwa mujibu wa gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung, si muda mrefu misikiti Ujerumani itakuwa mingi kuliko makanisa.

  My take

  Wasio kuwa vijana viongozi wa wakristo jiandaeni kufundishwa maadili ya kikristo nawatakieni kila la heri.
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  kama ni maadili mazuri yakutokupora rasilimali za nchi i have no comment, hata mashehe wanaweza wakadhamini mafunzo yoyote ya kumjenga binadamu yeyote kimaadili. mbona vipo vyuo na shule nyingi tu za kiislam au kikatoliki na dini zote wanasoma huko bila ubaguzi?? acheni unafiki wa kupandikiza chuki za kidini hapa ni jukwaa la siasa tu mkuu. jumuia ya kiislam leo na itoe udhamini wa aina hiyo kwa CDM kama hawataenda kusoma.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  so?? mbona mnapeleka watoto weu kwenye seminary ? magari ya kijerumani sio ya kikristo? mbona mnayatumia ?acha udini
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hizi ni propaganda nyingine za kipuuzi kabisa. Wewe unajua kama viongozi waislamu wengi walioko madarakani hivi sasa walisoma katika shule za Kikristo? Je watengwe na jamii ya waislam kwa kuwa tu walisoma katika shule za kikristo? Huku ni kukosa hoja kabisa, kukiita CHADEMA ni chama cha Kikristo eti tu kwa sababu kina mahusiano na chama cha kikristo cha ujerumani? Kwa hiyo kwa vile Tanzania inapata support kubwa kutoka Uingereza na Marekani ambazo zote zina mrengo wa kikristo, tuiite Tanzania ni nchi ya Kikristo? Hapa bado hujafanikiwa kutubadilisha mkuu, kalete hoja nyingine. Lakini hii iliyopo hapa haina mshiko. sanasana wivu ndo unawasumbua baada ya kuona viongozi wa chadema wanapata nafasi ya kufundishwa maadili ya uongozi bure, wakati wale wa CCM na vyama vingine hawana nafasi hiyo.
   
 5. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo kwa mtazamo wako hupo ni kwamba mwislam akiwa na rafiki ambae ni mkristu ni kitu kibaya?Halafu kichwa cha habari yako ni tofauti na maelezo cause unasema Mbowe na Slaa wameweka wazi mrengo wao wa kikatoliki lakini hakuna mahali ambapo Mbowe au Slaa wamelizungumza hilo.Ninachokushauri nenda kasome katiaba ya CHADEMA sura ya tatu "B" utakuata ufafanuzi wa Mrengo wa CHADEMA ni upi.Hizo propaganda zenu za udini hazina nafasi katika nchi hii hasa wakati huu ambao watanzania wengi wamefunguka macho, masikio na akili zao,huu sio wakati wa mwanzo wa vyama vingi ambapo mlikuwa mnawahadaa watu kwa kuwawekea mikanda ya vita kuonyesha kwamba wakichagua upinzani kutakuwa na vita.Those days are over my friend, we cant listen to those propaganda's while our Nation is perishing.
   
 6. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Ikiwa kinatoa mafunzo yamaadili na si kusilimusha kuwa mkatoliki hakunatatizo ila tatizo niwewe mleta mada usiye jua uandikalo kwani pamoja CDU kusha utawala ujerumani hatujasikia wanawasilimusha waislamu kuwa wakristo zaidi ya kuona uislamu unashamiri kwa kiwango kikubwa
   
 7. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #7
  Jun 25, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  magamba wameshikwa pabaya, kila wanapojaribu wanachemka, leo hii nenda kinondoni muslim au MUM km hakuna wakristo wanaosoma huko, nina ushahidi kifungiro girls alikuwepo mtoto wa marehemu omary ally juma wakati huo mimi nilikuwa magamba sekondary, sasa sijui hawa wanaoneza udini wanatumia nini kufikiri!! halafu kwanini simsikii mkristo hata siku moja akisema kuna udini??
   
 8. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #8
  Jun 25, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  mod hapa kuna upotoshaji mkubwa naomba muifute hii thread au muihamishe jukwaa la dini, ama kichwa cha habari kibadilishwe.
   
 9. R

  Rweza Member

  #9
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 18, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mantiki ya ujumbe mzima ni nzuri sana ila hayo maneno uliyomalizia nayo hayakubaliki hata kidogo kwenye jamii yetu ya kitanzania.
  Acha kabisa udini, elimu huwa ni nzuri haijalishi imetolewa na Sheikh au Askofu.
  Acha udwanzi kabisa.
   
 10. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #10
  Jun 25, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ni nani kawaambia Mbowe ni Mkatoliki, hiyo habari imeandikwa na Gazeti la wadini Annur, ambalo husomwa na watu ambao kwao wanadhani kuongea na viongozi wa Chama cha Kikristo basi nanyi mnamafungamano na ukristo wao, ni wavivu kufikiri wanaweza kushabikia habari za kishabiki kama hizo. ni Ukengeufu wa akili
   
 11. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #11
  Jun 25, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Ugonjwa wa akili huanza pole pole!

  Kuokota makopo ni hatua ya juu ya upunguani, haya bana!
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Vijana wa Napeat work! Hongera kaka maana umeingiza siku. Sasa kamwonyeshe Nape akupe tshirt, kofia na kanga za kijani ujifunge!
   
 13. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #13
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Sokomoko hii album ya udini sasa hivi haiuzi kabisa sokoni raia hawataki kununua, wewe siunaona hata malaria sugu sasa hivi ameachana nayo
   
 14. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #14
  Jun 25, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mi nilifikiri SOKOMOKO ni katuni ya kwenye gazet, kumbe upo kweli kweli.
  Siku ukiacha kunywa GONGO akili itatulia utaandika vitu vyenye maana.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  @Sokomoko,

  Kwanza Mbowe sio Mkatoliki, ni mlutheri. Pili, kama CHADEMA wamekuwa na uwisiano wa kikazi kati yao na CDU inawafanya wao chadema wawe na mrengo wa kikristu basi kwa formula hiyo hiyo tunaweza kusema uhusiano kati ya ccm na chama cha kikomunisti cha china kinawafanya ccm wawe ma-budhists?

  Ni watu wa aina Sokomoko ndio wasiojua kwa karne hii CDU is only a name (historically) kama ilivyo kwa Bank ya CRDB-cooperative Rural Development Bank au PPF- Parastatal Pensions Fund. Vyombo hivi vilianzishwa kwa matakwa na mazingiria ya nyakati 'hizo' hata hivyo kama ambavyo dunia imekuwa inabadilika kumekuwa na mabadiliko ya kimsingi (fundamental changes) lakini wamebakia kutumia jina (kama jina tu) kwa sababu tayari umma umeshalizowea lakini hata kwenye Acts (legal basis) wanakuwa wameshabilisha kanuni na taratibu za kuendesha vyombo hivi. Nani asijuwa kuwa Ujerumani watu wako watu wengi wasio amini kwamba mungu yupo (athists) let alone christians?

  Kwa hiyo Sokomoko CDU hawawezi (hata kama wangetaka) constitutionally kufanya siasa kwa kanuni za ki-kristu, na hata kama wangefanya kwa kufuata u-kristu watakuwa wakistristu wakatoloki? au lutheran? au evangelism? Kwa kifupi ulichoandika ni hadhithi kama ulivyosimuliwa na babu yako lakini cha ajabu hukutaka kushughulisha ubungo wako kujuwa kama kweli all the founding princples still hold!

  Mwisho, ni wapi au ni kitabu gani au ni mstari gani kweny manifesto yaCHADEMA unayozungumzia UKOTOLIKI. Ili theory yako ikubalike you have to have concrete evidence or should I say 'mutliple' evidence all pointing towards one direction, that is CHADEMA are preaching catholism.

  Next time try to update your knowledge.
   
 16. D

  Duma Member

  #16
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kama uliyo andika yanatoka rohoni mwako kwa uaminifu kabisa utokanao na imani ya kiislam ninasema kuwa kwangu hauna hatia kabisa hata kama maandishi yako ni ya kibaguzi na yanachochea chuki lakini kama maandishi haya yana ajenda ya siri nyuma yake ila unatumia dini kufanikisha ajenda ya siri basi unatenda dhambi kubwa mno hisiyostahili msamaha mbele ya Allah maana madhara yatokanayo na chuki za kidini ni makubwa mno ikiwemo machafuko makubwa yanayoweza kusababisha umwagaji wa damu mkubwa sana ambapo waathirika wa machafuko hayo ni sisi sote waislam na wakristu na wewe ukiwemo. Maelezo yako yamenifanya niamini kuwa lengo lako ni kuwafanya watanzania waichukie chadema kama ni hivyo basi tumia njia nyingine sio hii ya udini. Mambo unayofanya ni kinyume kabisa na Quran Tukufu pamoja na Biblia Takatifu.
   
Loading...