Elections 2010 Slaa: Mashushushu watawanywa mikoani kuhakikisha ushindi kwa CCM

Tuijali nchi yetu. CCM ipumzishwe mwaka huu. Binafsi nitajitahidi kushawishi watu wengine zaidi ya kumi ili wamchague Dr. Slaa, huu ndiyo mchango wangu kwa nchi yangu Tanzania.

Na huu ndio mchango uliotukuka. Wenzetu walioendelea walifahamu maana ya neno mabadiliko.....ni vizuri na wengine wakapewa nafasi ya kutuongoza ili tuwe na adabu katika kazi ya uongozi.

Hivi cheo ni dhamana au CCM wanataka iweje???? kwamba cheo ni roho hata ukifa unaondoka nayo????

Ili uchaguzi 2015 uwe na maana.....ili tuone maendeleo kwa Taifa hili miaka 5, 10, 15....200 n.k ijayo...ni lazima CCM ing'oke 2010.

JK angeweza kufaa kwenye ukatibu wa chama cha mafisadi ngazi ya kata lakini si urais wa nchi kama Tanzania.......hawezi. Hii nchi kwa miaka mitano iliyopita imeharibiwa mno....yaani Taasisi za serikali na vyombo vya ulinzi na usalama ndio vimeongoza Taifa hili tangu 2005.

Ni kwamba JK ni mmoja wa watu wanaoamini kuwa ukiwa Rais basi huna kazi.....kwa kuwa chini yako kuna watu wanakufanyia kazi...kwa hiyo kazi yako wewe ni kula na kulala, kuzunguka zunguka na kutalii nchi za kigeni, kufanya anasa za kila rangi na aina na mengineyo mengi....sasa kama huu sio upunguani ni kitu gani. Ukiongoza mazuzu hili linawezekana.

Urais ni kazi ngumu sana tofauti na watu kama JK wanavyodhani.

Watanzania naomba mjue kuwa JK ameboronga mno na hili litathibitika atakapotoka madarakani....na ndio maana anaogopa mno kung'oka. Na hata 2015 tayari anataka kupandikiza mtoto wa swaiba wake...Rais wa Zamani ili kwa miaka mingineyo 10 hadi 2025 asiwepo wa kuhoji kuboronga kwake.
 
Mkuu ingependeza kama ungekanusha maelezo yangu kama sio sahihi...

Shem siku ukiachana na Kidumu Chama Cha Kifisadi utakuwa bomba sana! Nakuombea sana ufahamu ukweli, hebu niambie kuhusu Chifu Mwangupili na Chifu Mwailemale! Tunaelekea wapi kama taifa
 
Ng'wanangwa ACHA UDINI KWANI hichi kitengo cha usalama wa taifa jeshini si kinaongozwa na Wakristo na tayari jamaa wako mpaka Zanzibar kwenye mahoteli wanakula kuku na wanaonekana kwenye mikutano wa CUF kila siku na wanajulikana ingawa wanajichanganya kama symapthetic wa upinzani pia idara ya Usalama wa Taifa ik o kila kwenye majimbo ambayo CCM ina upinzani mkali haimati kuwa mgombea ni muislamu au mkristo ikiwa uko upinzani wao ndio wanatoa ushauri wa kuingia kwenye inner circle ya mgombea na kuwanunua wasaidizi wake hilo mulijue jimbo la Slaa la Zito Kabwe na NDesamburo yote hayo ni target kama alivyosema Kinana.
 
Huyo Slaa kajaza mafisadi tokea ngazi ja juu ya chama chake hadi chini... Mbaya zaidi yeye mwenyewe ni fisadi kiwembe...
Josephine%20kuhutubia.JPG
Bibie Josephine akimpiga tafu slaa..


Chagua Slaa kiongozi bora.

Achana na Kikwete bora kiongozi.
 
Shem siku ukiachana na Kidumu Chama Cha Kifisadi utakuwa bomba sana! Nakuombea sana ufahamu ukweli, hebu niambie kuhusu Chifu Mwangupili na Chifu Mwailemale! Tunaelekea wapi kama taifa
Hayo mambo ya uchifu, ukamanda na mengineyo kama hayo ni vikwelembezo tu vya uchaguzi havina uhusiano wa moja kwa moja na mwelekeo wa Taifa.
 
Hawa ni usalama wa mafisadi na si usalama wa Taifa wangekuwa wanalinda usalama wa Taifa mafisadi wote wangekuwa lupango na siyo kuendelea kutanua uraiani.
 
Jamani vyombo vya usalama mko kuzini kulinda maslahi ya Watanzania wote. Fanyeni kazi yenu kwa kufuata viapo mlivyokula, na kuacha mapenzi ya watanzania for once kusimama.

Mambo yaliyotokea kenya na watu kupoteza maisha kwa sababu ya tamaa ya watu wachache msituletee TZ.

Wananchi watakachoamua, Tumwombe Mungu ndio kiwe.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Dah, JF hatujambo kwa kushabikia udaku, hatujapata habari kamili tayari tumeshaanza kurauana!!
 
Back
Top Bottom