Slaa, Lissu, List of shame na stori ya Albert Eistein kuhusu physics (tofauti ya physics na siasa)

Labrujita

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
399
126
Unaweza ukaona ni kama kamchezo fulani lakini huo ndio ukwelikwamba kati ya mafahali hawa wawili mmoja ni mwanasayansi na mwingine ni mwanasiasa. List of shame iliandaliwa na Tundu Lisu (mwanasayansi) kwa vigezo vya kisayansi yaani Logic na misingi ya rationality huku vigezo vikitajwa kwa kila mlengwa. Baadae list hiyo ilisomwa na Dr Slaa (Mwanasiasa) na sasa inaendelea kutumiwa na mwanasiasa huyu kuuangamiza umma kwa kuyapinga mabadiliko nje ya CCM ambayo kimsingi ndio lengo kuu la msingi ambalo vyama vya upinzani vinapigania.

Jambo hili limekuwa likipambwa na hoja dhaifu ya Richmond ambayo ndio iliyopelekea Lowassa kuwepo kwenye list hiyo na ambayo tayari imetolewa ufafanuzi ambao kimsingi unamfanya asiwepo tena katika list ile huku vyombo vya dola ikiwemo ripoti ya CAG navyo vikibainisha kutohusika kwa Lowassa katika Richmond zaidi ya UWAJIBIKAJI wa KISIASA

Ni dhahiri kwamba yatupaswa tujiuleze hivi mwanasayansi aliyetengeneza bomu na anayejua kulitegua na mwanasiasa ambaye anaishia kulipua bomu ni nani anayepaswa kulaumiwa kwa kwa athari ya mlipuko?

RETHINK
kuhusu watu wenye nia ya kuturudisha nyuma na wenye nia mbaya na mabadiliko ambayo watanzania wamebakiza robo ya safari yao kuyafikia. Albert Eistein aliwahi kuulizwa swali na profesa na kujibu ifuatavyo


"[When asked "Dr. Einstein, why is it that when the mind of man has stretched so far as to discover the structure of the atom we have been unable to devise the political means to keep the atom from destroying us?"] "That is simple, my friend. It is because politics is more difficult than physics."
 
Umemdharau wewe unayeshabikia fisadi na jzi lowas anayetakiwa kufa kwa kuchomwa moto

Heee apewe adhabu aliyopewa Balali kwa kosa gani? vipi kuhusu adhabu ya aliyesababisha ufisadi wa zaidi ya bilioni 200 zilizotajwa na PPRA katika wizara ya ujenzi? hivi kulinunua Mtanzania la tarehe 07/10/2015 mlitumia sh ngapi?
 
Lakini kiukweli kabisa, kwanini Lowassa alikataliwa na Nyerere?
 
acha kujifariji slaa anaminika kuliko mtu yeyote wa chadema

Mchango na heshima yake ndani ya CHADEMA akiwa kama katibu mkuu wa chama itadumu na haitapotea lakini tujiulize anaaminika kuliko mtu mwingine yeyote kwa lipi hasa? kwani yeye na asiwe Mnyika, Ndesamburo, Prf Safari na wengineo?
 
Lakini kiukweli kabisa, kwanini Lowassa alikataliwa na Nyerere?

Kwan Nyerere ni nan haswa wa kuwakataa na kuwakubali watu??? alikuwa ni kiumbe tu km ww na alikuwa na interest zake km mwanadam mwingine yyte,acha uoga taifa haliwez kuishi kwa kutegemea maono ya marehem bn,sisi ni watu na tinafikir km alivokua yy na hiz ni zama tofauti ndo mana yy ni marehem na ss ni watu hai!
 
acha kujifariji slaa anaminika kuliko mtu yeyote wa chadema

Km anaaminika mchukueni ccm ili awasaidie kugawa kura za ukawa,wakat zitto anataka kutimuliwa mlisema asifukuzwe ni mtu makin,ss nyie hamtaki watu makini huko kwenu si muwachukue?!
 
Narudia kwa kusema "Kura yangu nitampa LOWASSA kwa kuichukia CCM."
Wala sihitaji kuzungusha maneno..
 
...Jambo hili limekuwa likipambwa na hoja dhaifu ya Richmond ambayo ndio iliyopelekea Lowassa kuwepo kwenye list hiyo na ambayo tayari imetolewa ufafanuzi ambao kimsingi unamfanya asiwepo tena katika list ile...
Huyo Lowassa asingejiunga na Chadema bado angekuwa katika hiyo List of Shame. Msingetumia muda wenu kumsafisha kama mnavyohaha sasa. Tatizo lenu mnafikiri watu wengine tuna akili za kitoto (rahisi kudanganywa). Jidanganyeni wenyewe huko huko ukawani.
 
Kipindi kile Nyerere kama binadamu alikuwa na mtu wake; kama ambavyo Kikwete naye alikuwa na mtu wake mfukoni...!!

hata hivyo kwa sasa sio rahisi kuzuia mabadiliko ambayo naweza yafananisha na mimba iliyokomaa isivyofanyiwa mchezo
 
Jana Dr. Mihogo alisema tunachagua mtu na sio chama. Swali ni je hivi Tanzania tuna mgombea binafsi?? na je fisiem inawezaje kujitenga na Mapadlock au yeye kujitenga na fisiem?
 
[RETHINK kuhusu watu wenye nia ya kuturudisha nyuma na wenye nia mbaya na mabadiliko ambayo watanzania wamebakiza robo ya safari yao kuyafikia. Albert Eistein aliwahi kuulizwa swali na profesa na kujibu ifuatavyo

“[When asked “Dr. Einstein, why is it that when the mind of man has stretched so far as to discover the structure of the atom we have been unable to devise the political means to keep the atom from destroying us?”] “That is simple, my friend. It is because politics is more difficult than physics.”[/QUOTE]

Dr. Slaa alitegemea CDM ifanye siasa zile zile zilizoshindwa kutwaa dola kwa namna ile ile na kutegemea kutwa dola sasa. HAIWEZEKANI, katika siasa ni lazima kubadili mbinu.

Na kwa kweli kama mbinu hii ingeungwa mkono na wadau wote wa CDM kwa moyo mmoja akiwemo Slaa na wengine ambao wana wasiwasi, hakika ukombozi ungekuwa mwepesi sana mwaka huu na CCM ingeachia nchi kirahisi.

Iwe iwavyo, kwa mwamko wa wananchi wa kutaka mabadiliko, CCM inaondoka this time hata kama ni kwa margin ndogo.

 
km anaaminika mchukueni ccm ili awasaidie kugawa kura za ukawa,wakat zitto anataka kutimuliwa mlisema asifukuzwe ni mtu makin,ss nyie hamtaki watu makini huko kwenu si muwachukue?!
haisaidii ccm anaisaidia nchi yake kwa kubainisha ubaya wa mafisadi
 
Back
Top Bottom