Slaa kuyakataa matokeo!

jjeremiah

Member
Jul 30, 2010
43
13
Hivi Mbowe na Zitto kukubali kuwa viongozi wa upinzani bungeni, na Marando kuwania uspika ina maana wao wameyakubali matokeo ya uchaguzi mkuu tofauti na madai ya katibu wao mkuu ambaye ndiye alikuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho kwamba kura hasa za urais zilibadishwa na kwamba usalama wa taifa ulihusika kufanikisha ubatili huo, sheria inasemaje kuhusu hili, Na je yeye mwenyewe mbona hasikiki, haonekani
 
aonekana wapi na akiwa anafanya nini?muacheni mzee wa watu aendelee kuandika hotuba ya kukataa matokeo na kumkataa JK kwa kuwa ni RAIS MWIZI kaingia madarakani kwa kuiba kura
 
Hivi Mbowe na Zitto kukubali kuwa viongozi wa upinzani bungeni, na Marando kuwania uspika ina maana wao wameyakubali matokeo ya uchaguzi mkuu tofauti na madai ya katibu wao mkuu ambaye ndiye alikuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho kwamba kura hasa za urais zilibadishwa na kwamba usalama wa taifa ulihusika kufanikisha ubatili huo, sheria inasemaje kuhusu hili, Na je yeye mwenyewe mbona hasikiki, haonekani

wewe ulitakaje? slaa ni slaa anasimama na miguu yake na kila mmoja ana maamuzi yake .syo mawazo ya zitto au mbowe ndo aliyonayo slaa.tafakari fikiri.
 
Hivi Mbowe na Zitto kukubali kuwa viongozi wa upinzani bungeni, na Marando kuwania uspika ina maana wao wameyakubali matokeo ya uchaguzi mkuu tofauti na madai ya katibu wao mkuu ambaye ndiye alikuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho kwamba kura hasa za urais zilibadishwa na kwamba usalama wa taifa ulihusika kufanikisha ubatili huo, sheria inasemaje kuhusu hili, Na je yeye mwenyewe mbona hasikiki, haonekani

jjeremiah, ungetumia akili angalau kidogo ungetambua kuwa taasisi ya bunge siyo taasisi ya uraisi. upo uwezekano mtu akapata uraisi lakini chama chake kikawa na wabunge wachache kuliko wa vyama ambavyo havijatoa raisi. Dr. Slaa aliyakataa matokeo ya uraisi na ndiye aliyekuwa mgombea. matokeo ya ubunge yaliyochakachuliwa wagombea husika watayapinga mahakamani. Tofautisha Bunge na uraisi, ni mihimili miwili tofauti. Halafu Dr hakuyakata matokeo bali aliyakataa
 
Haujui hata unauliza nini. Umesikia kwamba anakataa matokeo ya wabunge wote. Matokeo yenye utata ni ya urais na ndiyo anayokataa. Bunge linajitengemea na haliko chini ya rais kwani umesikia wanagombea Uwaziri? Bunge makini ni mwiba kwa rais mwizi kwa hiyo wako sahihi 100%.

Ushauri. Soma katiba ya nchi, au hata vitabu vya uraia wanavyotumia wanafunzi wa shule za msingi ongeza na busara zako utakuwa safi katika kujenga hoja.
 
Ni kelele tu za mlango

Matokeo yameshatangazwa

Kikwete ameshaapishwa
Chapter CLOSED:closed_2:
 
Hivi Mbowe na Zitto kukubali kuwa viongozi wa upinzani bungeni, na Marando kuwania uspika ina maana wao wameyakubali matokeo ya uchaguzi mkuu tofauti na madai ya katibu wao mkuu ambaye ndiye alikuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya chama hicho kwamba kura hasa za urais zilibadishwa na kwamba usalama wa taifa ulihusika kufanikisha ubatili huo, sheria inasemaje kuhusu hili, Na je yeye mwenyewe mbona hasikiki, haonekani

Au leo nimeamka vibaya?
Thread ya pili hii siielewi.
 
HAlafu akishakataa itakuwaje kulingana na katiba mbofu mbofu. Dr. Slaa aliweza tuliza ghasia ambazo CCM na vyombo vyake vya usalama wasingeweza zima. Angalia yaliyotokea Mwanza, SHY na DAR japo kidogo tu na vipi tangazo lingetoka kwa Dr.Slaa.
 
MIHIMILI MIKUU YA DOLA:

1: Serikali - Inaongozwa na Rais, akisaidiana na Baraza la mawaziri.

2: Mahakama - Inaongozwa na Jaji Mkuu kwa msaada wa majaji na mahakimu.

3: Bunge - Inaongozwa na Spika akisaidiana wabunge.
 
J.Jeremiah,NEC ilitangaza kikatiba kuwa kutakuwa na uchaguzi wa Madiwani,Ubunge na Rais. Kutenganisha ivo sio kwamba hawaelewi wanachokifanya. Zingatia kuwa kama diwani wa TLP amechaguliwa,hawezi kugoma kutenda kazi kwa kusema mbunge wa Tlp au Rais wake ameibwa kura. Mtu mzima anaelewa tofauti yake kikatiba. Pata nakala ya katiba utaelewa zaidi.
 
kweli ingekuwa ni balaa,lakini asikae kimya basi atoe hata tamko kwa kuwashukru wannchi wote waliomchagua na watanzania kwa uijumla.:israel:
HAlafu akishakataa itakuwaje kulingana na katiba mbofu mbofu. Dr. Slaa aliweza tuliza ghasia ambazo CCM na vyombo vyake vya usalama wasingeweza zima. Angalia yaliyotokea Mwanza, SHY na DAR japo kidogo tu na vipi tangazo lingetoka kwa Dr.Slaa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom